PreGE2025 Hoja sita CHADEMA, Madai ya makada wake kukamatwa na kupigwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
"Niseme hatua kadhaa ambazo tunataka zichukuliwe (kutokana na kile ambacho CHADEMA inadai kuwa Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro imetoa taarifa za uongo kuhusu madai ya viongozi na makada wao kukamatwa, kupigwa na kuteswa mnamo tarehe 24/04/2025) ni pamoja na:

Pia soma Muliro awakana Makada wa CHADEMA wanaodai kuteswa, kutupwa porini

(i) Kamanda wa Polisi Jumanne Muliro kwa kuongoza zoezi hilo na kwa kusema uongo hadharani mamlaka yake ya uteuzi na nidhamu imchukulie hatua ya kumuondoa kwenye Kanda Maalum ya Dae es Salaam,

(ii) Kwa kuwa Jeshi la Polisi limeshasema uongo mara kadhaa tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) kama haya matendo hayana baraka zake, ajitokeze yeye mwenyewe atoe taarifa kwa umma juu ya matukio ya kutekwa, kupigwa na kuumizwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMa akitaja idadi halisi,

(iii) Kwa sababu Kamanda Jumanne Muliro amehusika yeye binafsi katika zoezi hili, chama tumeshawaelekeza Mawakili wa chama wachukue hatua za kisheria juu ya Jumanne Muliro yeye binafsi,

(iv) Chama vilevile kimeshaelekeza na kuwaomba Mawakili wa chama kufungua mashauri katika vyombo mbalimbali vya kimataifa vya Haki za Binadamu Afrika na Dunia kutokana na matukio yaliyotokea April 24.2025,

(v) Natoa mwito kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiwia ni Amiri Jeshi Mkuu kuchukua hatua,

(vi) Natoa wito kwa vyombo vyetu vya ndani, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ipitie matukio yote ya tarehe 24/04/2025, masumulizi ya tarehe 25/04/2025 na masimulizi ya leo, tume ichukue hatua kwa upande wake" -Mnyika

Ni sehemu ya yale aliyozungumza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Mnyika mbele ya wanahabari leo, Jumatano Aprili 30.2025, Dar es Salaam
 
yaani molilo achukuliwe atua?hii serikali ya huyu mwanamke haina uwezo huo maana wote wanalindana alafu ujue toto baya ila c kwa mamaye
 
Nani wa kumchukulia hatua sasa

Ova
 
hakuna mtu alitupwa porini ,na bora hivyo wameokoka kama wangekamatwa na kupelekwa rumande basi wangeunganishwa na kesi ya uhaini.

Chadema jifunzeni kuweka mapaparazi haswa kunapotokea valangati la mshike mshike kamata kamata hata mnaweza kuweka kamela fiche huko kwenye machaka ya mabwepandwe ,mkaziweka kwa wingi tu ,na hao waliosema wametupwa na kuludishiwa kamela zao kwa nini hawakupiga picha sehemu ,

Hizi gari kwa wenyeji walioziona Bwagamoyo kwa nini hawakuzipiga picha,kuna mtu alihojiwa na kusema alijuwa kuna jambo,

Na nyinyi mkiona watu wanatoweka toweka katika mshike mshike kwa nini hamkuweka doria maeneo husika wanayotupwa watu ,sio mnavaa magwanda ya mgambo halafu badala ya kuingia nayo huko mnapnda nayo kwenye majukwaa.

Mheshimiwa Magu alizuia mambo haya kwani alijua kuna watu ni wakorofi watamsababishia matatizi,

Bibi Samia mwenye huruma ,huruma zake sasa zinamponza ni bora akapiga nyundo kuzuia mikutano mpaka bado miezi mitatu kwa uchaguzi mkuu.
 
wahalifu nyie lazima mpigwe tu hamna namna hatuwezi kuvumilia mnaharibu amani ya nchi kijinga namna hiyo mtapigwa tu
Ukipewa kuchagua kati ya AMANI na haki UTACHAGUA NN?
Ukiulizwa kati ya WALIOUZA Mali za umma mfano bandari, madini na viwanda wa lumumba na kina mnyika wanaodai haki ya uchaguzi huru wa haki na wa kuaminika mhalifu ni nani?
Ukiulizwa useme hao wavunjifu wa amani waliivunja wapi na lini unaweza kujibu?
Acha uchawa
 
"Niseme hatua kadhaa ambazo tunataka zichukuliwe (kutokana na kile ambacho CHADEMA inadai kuwa Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro imetoa taarifa za uongo kuhusu madai ya viongozi na makada wao kukamatwa, kupigwa na kuteswa mnamo tarehe 24/04/2025) ni pamoja na:

Pia soma Muliro awakana Makada wa CHADEMA wanaodai kuteswa, kutupwa porini

(i) Kamanda wa Polisi Jumanne Muliro kwa kuongoza zoezi hilo na kwa kusema uongo hadharani mamlaka yake ya uteuzi na nidhamu imchukulie hatua ya kumuondoa kwenye Kanda Maalum ya Dae es Salaam,

(ii) Kwa kuwa Jeshi la Polisi limeshasema uongo mara kadhaa tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) kama haya matendo hayana baraka zake, ajitokeze yeye mwenyewe atoe taarifa kwa umma juu ya matukio ya kutekwa, kupigwa na kuumizwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMa akitaja idadi halisi,

(iii) Kwa sababu Kamanda Jumanne Muliro amehusika yeye binafsi katika zoezi hili, chama tumeshawaelekeza Mawakili wa chama wachukue hatua za kisheria juu ya Jumanne Muliro yeye binafsi,

(iv) Chama vilevile kimeshaelekeza na kuwaomba Mawakili wa chama kufungua mashauri katika vyombo mbalimbali vya kimataifa vya Haki za Binadamu Afrika na Dunia kutokana na matukio yaliyotokea April 24.2025,

(v) Natoa mwito kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiwia ni Amiri Jeshi Mkuu kuchukua hatua,

(vi) Natoa wito kwa vyombo vyetu vya ndani, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ipitie matukio yote ya tarehe 24/04/2025, masumulizi ya tarehe 25/04/2025 na masimulizi ya leo, tume ichukue hatua kwa upande wake" -Mnyika

Ni sehemu ya yale aliyozungumza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Mnyika mbele ya wanahabari leo, Jumatano Aprili 30.2025, Dar es Salaam
View attachment 3320496
Mamlaka gani?
 
wahalifu nyie lazima mpigwe tu hamna namna hatuwezi kuvumilia mnaharibu amani ya nchi kijinga namna hiyo mtapigwa tu
Anaeharibu amani ya nchi ni nani? Anaeenda mahakamani kusikilza kesi au yule anaeteka kupiga na kuua watu?
 
hakuna mtu alitupwa porini ,na bora hivyo wameokoka kama wangekamatwa na kupelekwa rumande basi wangeunganishwa na kesi ya uhaini.

Chadema jifunzeni kuweka mapaparazi haswa kunapotokea valangati la mshike mshike kamata kamata hata mnaweza kuweka kamela fiche huko kwenye machaka ya mabwepandwe ,mkaziweka kwa wingi tu ,na hao waliosema wametupwa na kuludishiwa kamela zao kwa nini hawakupiga picha sehemu ,

Hizi gari kwa wenyeji walioziona Bwagamoyo kwa nini hawakuzipiga picha,kuna mtu alihojiwa na kusema alijuwa kuna jambo,

Na nyinyi mkiona watu wanatoweka toweka katika mshike mshike kwa nini hamkuweka doria maeneo husika wanayotupwa watu ,sio mnavaa magwanda ya mgambo halafu badala ya kuingia nayo huko mnapnda nayo kwenye majukwaa.

Mheshimiwa Magu alizuia mambo haya kwani alijua kuna watu ni wakorofi watamsababishia matatizi,

Bibi Samia mwenye huruma ,huruma zake sasa zinamponza ni bora akapiga nyundo kuzuia mikutano mpaka bado miezi mitatu kwa uchaguzi mkuu.
1000053029.jpg

Mbuzi wewe
 
CDM chama changu kinayumbishwa kwa kila namna kinakosa cha kusimamia.

No reform no election
Mwenyekiti yupo ndani
Makamu anakamatwa
Wanachama wanapigwa

Mwisho wa siku kunabaki matamko na harakati za mtaani kufikia wanachama znashindikana.

Ccm hawezi kuwaonea huruma.

Rais huyu huyu mnayesema hataweza simamia uchaguzi kwa haki bila rerform mnamuomba amtengue Muliro.

Hizi ni ndimi mbili.
 
Hivi IGP ni nani? Maana hasikiki popote pale, Murilo ndiye anaonekana kama IGP.

Huyu IGP yupo kwenye low key sana, aache uoga. Ataoe muelekeo wa jeshi la polisi wasijisahau. Sisi wananchi tunataka kusikia msimamo wake juu ya matendo ya polisi.
 
Back
Top Bottom