hakuna mtu alitupwa porini ,na bora hivyo wameokoka kama wangekamatwa na kupelekwa rumande basi wangeunganishwa na kesi ya uhaini.
Chadema jifunzeni kuweka mapaparazi haswa kunapotokea valangati la mshike mshike kamata kamata hata mnaweza kuweka kamela fiche huko kwenye machaka ya mabwepandwe ,mkaziweka kwa wingi tu ,na hao waliosema wametupwa na kuludishiwa kamela zao kwa nini hawakupiga picha sehemu ,
Hizi gari kwa wenyeji walioziona Bwagamoyo kwa nini hawakuzipiga picha,kuna mtu alihojiwa na kusema alijuwa kuna jambo,
Na nyinyi mkiona watu wanatoweka toweka katika mshike mshike kwa nini hamkuweka doria maeneo husika wanayotupwa watu ,sio mnavaa magwanda ya mgambo halafu badala ya kuingia nayo huko mnapnda nayo kwenye majukwaa.
Mheshimiwa Magu alizuia mambo haya kwani
alijua kuna watu ni wakorofi watamsababishia matatizi,
Bibi Samia mwenye huruma ,huruma zake sasa zinamponza ni bora akapiga nyundo kuzuia mikutano mpaka bado miezi mitatu kwa uchaguzi mkuu.
Magufuli Wananchi wengi walimpenda maana hakua mnafiki .
Akisema anachukia matumizi makubwa ya Serikali ni kweli hapendi .
Akisema hataki ufisadi ni kweli hataki.
Akisema hapendi safari za nje kweli hapendi ,Akisema hataki misaada ya magaidi kweli hapendi .
Akisema hataki waekezaji uchwara kweli hataki .
Magufuli akisema hataki rasilimali za nchi zichukuliwe na wageni kweli hataki .
Akisema hataki mikataba mibovu ya Bandari kweli hataki .
Akisema anajenga reli ya kisasa kweli anajenga .
Akisema hataki umeme wa michango kweli hataki.
Akisema hataki umeme ukatike kikichongo kweli hataki .
Akisema hataki ujanja wa halmashauri kujenga barabara kimichongo na kuanzisha Tarura kweli alianzisha .
Akisema hataki kukosolewa kwenye maamuzi yake ya kizalendo kweli hataki na hana unafiki .
Akisema atafuta upinzani wa kupiga dili kweli alikusudia kuufuta .
Mtu kama huyo hata wapinzani wake wanajihadhari kuishi naye ndio maana walikimbia nchi .
Sasa huu unafiki wa kusema hadharani sasa najenga demokrasia .
Rudini tufanye siasa .
Tukae mezani tujenge nchi .
Nitafanya maridhiano na kufanya Reform ili tufanye siasa za kistaarabu .
Fanyeni mikutano ya hadhara .
Tuvumiliane .
Hadharani ni mwema gizani anakua kama vile aliwawekea samaki chambo yenye ndoana ili wakimeza iwanase na kuwakamata .
Ni aliahidi mwenyewe kufanya Reform sasa watu wanataka arejee kwenye kauli yake yeye kama Rais .
Zamani uimara na ukuu wa mfalme ulitokana na kusimamia kauli zake bila kubadilika .
Mtu anayeahidi jambo bila kulitekeleza ni mtu hatari na mnafiki asiyefaa kuwa kiongozi wa juu maana kuna siku atatoa amri bila maandalizi na kuleta maafa makubwa sana kwenye taifa .
Kinyonga killipewa mwendo mdogo sana kwa sababu ya uwezo wake wa kubadilika badilika . Kinyonga kingekuwa na speed na sumu kama Koboko kingeleta madhara makubwa sana .
Unapobadilika badilika basi Mungu anakuhesabu katika wale wanafiki walioshushiwa aya ya kuonywa kwa unafi wao.
Leo hii Lisu asingerudi kama angejua kuwa Mama Samia alikua anamvuta kwa kumtegea ili amnyonge kwa kesi ya mchongo.
Huenda Nabii Godbless Lema angebaki Canada kwenye maombi ili Mungu aamue ugomvi huu mpaka nchi iwe shwari ndio arudi . angeendelea na