Uchaguzi 2020 Hoja ya CHADEMA kwamba wahudhuriaji wa mikutano ya CCM kwamba wanabebwa kwenye magari naifananisha msemo wa usilolijua sawa na usiku wa giza

Uchaguzi 2020 Hoja ya CHADEMA kwamba wahudhuriaji wa mikutano ya CCM kwamba wanabebwa kwenye magari naifananisha msemo wa usilolijua sawa na usiku wa giza

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2020
Posts
358
Reaction score
271
Kwanza niwaulize hao wanaouzulia mikutano yenu wanatokea umbali gani? Kama wanatokea nje ya miji au katikati ya miji wanatumia nauli zao au zenu?

Mna uhakika gani kama wamejiandikisha au lah!, mnajuaje kama wote wamekuja kwa lengo la kuwapenda maana watanzania ni kawaida yao kuhudhuria kila jambo baya au zuri.

Niwafaamishe tu kuwa CCM ina wanachama wanaotambulika kindakindaki, CCM damu kila kitongoji, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda na Taifa wapatao Milioni 18 wakati huo huo waliojiandikisha wapo Milioni29.

Mnaweza kuona hesabu rahisi kabisa hivyo sisi tunawawezesha wanachama wetu kufika kwenye kampeni kwa wakati na tunaobeba tunajua wazi ni wanachama hai na wana kadi na kama hamuamini subirieni 28/10/2020.

Hhamjiulizi kwanini watu wanavaa sare na wanakubali kubebwa. Zimwi likujualo halikuli likakumaliza hivyo msije kujidanganya ni umaskini wenu ndio unaowafanya mshindwe kusomba wapiga kura na ingekuwa inaruhusiwa kuwabeba wanachama siku ya kupiga kura ndio mngezimia zaidi.

Chama chochote kinachojitambua kamwe hakiwezi kuacha kuwajali wanachama wake wanaowaweka madarakani, nasisitiza hapa tutawabeba wanachama wetu hai nchi nzima hatuwezi kuwasikiliza watu walioishiwa hoja.

Huwezi kujisifia kuwa watu wanakupenda na huku unashindwa kuwapa usafiri wa kufika mikutanoni. Chama chochote mtaji wake ni wanachama sio wahuni au watu wasiotabilika kama mnaamini siasa ni imani basi sisi tuna wanaotuamini Milioni 18 na wana kadi na watampigia Rais kura na tutashinda kwa kishindo, nyie endeleeni kusema tunabeba watu kwenye mikutano ilihali mnashindwa kujua ndio wanachama kindakindaki na ndio wapiga kura wa uhakika.
 
Ni kweli na wazi kuwa CCM hutumia pesa nyingi na vyombo mbali mbali vya usafiri kuwabeba watu ili kuhudhuria mikutano yao ya kampeni. Hilo halina ubishi, kila mtu anajua hivyo. CCM wao wenyewe wanasema huo ndio utamaduni wake.

Kwa mwaka huu, Mama Maria Nyerere ndio amekuwa mfano mzuri wa kukiri hilo. Na mama wa watu hakufurahishwa nalo, maana alisema kwa kuwa aliletwa kuja kujaza uwanja, akalazimishwa apande jukwaani kuzungumza, na aliposema hana cha kuzungumza, basi akakarishwa maneno ya kwenda kusema!!
 
Endeleeni kujidanganya mama maria anaweza kutoka kwa miguu kutoka kijijini mpaka musoma mjini tunazungumzia wapiga kura wa uhakika akiwemo mama maria nyerere.
 
Acha propaganda. Shule zinafungwa ili watoto wetu wahudhurie mikutano ya CCM, wafanyakazi tulazimishwa eti tusipohudhuria tutachukuliwa hatua za kinidhamu. Unataka kutudanganya sisi hawa hawa tunaolazimishwa kuhudhuria mikutano ya CCM? Hata Mama Maria Nyerere utasema aliongopa kwenye TV mubashara, usivyokuwa na aibu.
 
Kuna maembe huwa yanaiva kwa kuvundikwa kwenye majivu, mleta mada ni embe la aina hiyo, limelazimishwa kuiva.
 
ni uongo hata mtoto anakataa.tatzio la sisi tupo mitandaon kweli.kucheza na picha .in really ty wananchi wenyewe hiwa ndio wanaenda bila kubebwa wala nin
 
Ni
Acha propaganda. Shule zinafungwa ili watoto wetu wahudhurie mikutano ya CCM, wafanyakazi tulazimishwa eti tusipohudhuria tutachukuliwa hatua za kinidhamu. Unataka kutudanganya sisi hawa hawa tunaolazimishwa kuhudhuria mikutano ya CCM? Hata Mama Maria Nyerere utasema aliongopa kwenye TV mubashara, usivyokuwa na aibu.
Ninakupa takwimu za uhakika M18 si mchezo M29-18=11, Hiko hivi wenye viti vitongoji,vijiji nchi nzima+watu wanaowaongoza =M25 .
 
Acha propaganda. Shule zinafungwa ili watoto wetu wahudhurie mikutano ya CCM, wafanyakazi tulazimishwa eti tusipohudhuria tutachukuliwa hatua za kinidhamu. Unataka kutudanganya sisi hawa hawa tunaolazimishwa kuhudhuria mikutano ya CCM? Hata Mama Maria Nyerere utasema aliongopa kwenye TV mubashara, usivyokuwa na aibu.
Wacha uongo kenge wewe
Me mtumishi wa umma mbona sikulazimishwa kuhudhuria hizo kampeni na wala hakuna kilichobadilika na ninaendelea na kazi na account ina soma?
Kweli CHADEMA uzushi ni jadi yenu na Yuda wenu.
Mtaendelea kupiga miayo miaka nensa rudi
Nyambafuu kabisa mbuzi wew😯😯😯😯
 
Yaani huu uandishi wa kiboya unachosha watu tu. 'Wanaouzulia' ndio nini. Kwa ujinga wenu unadhani kwenye daftari la wapiga kura walikuwa wanaandikisha kwa vyama. Au na wewe unatoa siri zenu kwamba mlishachukua kadi za wapiga kura.
 
Shame on u!! Nilichokishuhudia katavi wakati wa ujio wa lisu, kilichokuwa kina fanywa na ccm ni aibu, ki ukweli kumbe pesa ya kuchezea ipo ila ya kumsaidia mwananchi haipo!! Mimi mwenyewe nilikula 10,000 ya bure kabisa eti tusiende kumuona LISU!!!! hizo ni akili matope
 
Back
Top Bottom