Hoja ya maslahi ya watumishi wa Umma inavyopotosha na Wapinzani

Na Bwanku M Bwanku

Hekaheka na pilika za kampeni zinaendelea kutimua vumbi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi kwa wagombea wa Urais, wabunge na madiwani kunadi Sera na Ilani zao wanazoenda kuzitekeleza kwa miaka mitano ijayo kama wananchi wakiwapa ridhaa yao.

Kwa bahati nzuri sana nimeendelea kufuatilia kwa kila jambo linaloendelea kwenye kampeni hizi na leo kwa uchache kidogo nitazungumzia kwa uchache tabia ya upotoshaji inayotumiwa na kuota mabawa kwa baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali.

Ukiachana na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kuwakashfu kwa kutweza utu na heshima ya watumishi wetu wa umma wote wanaofanya kazi kubwa usiku na mchana kwa kuwaita watu waliokotwa majalalani lakini zaidi nimesikia mara kadhaa wagombea haohao wa vyama vya upinzani wakipotosha kuhusu maslahi ya watumishi wa umma na mambo mbalimbali yanayowahusu watumishi wetu.

Nimewasikia wakipotosha waziwazi kuhusu hoja ya maslahi kwa watumishi wa umma bila hata ya kuogopa kama maneno yao yanaweza kuichonganisha Serikali, jamii na watumishi wetu wanaofanya kazi kubwa sana. Sasa njia ya muongo ni fupi na wala hakawii kuumbuka.

Kimsingi Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt. John Pombe Magufuli imeshughulikia maslahi ya watumishi wa umma kwa kiasi kikubwa sana tangu iingie madarakani Novemba 2015 hadi sasa.

Zifuatazo ni hatua mbalimbali na chache tu kati ya nyingi zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya 5 kushughulikia changamoto na maslahi ya watumishi wa umma wote nchini. Nayasema haya ili kuondoa huu upotoshaji wa wachache wasiolitakia mema Taifa letu. Twende pamoja.

1. Malipo ya malimbikizo ya mishahara.

Mpaka Novemba, 2020 Serikali imelipa Tsh. Billioni 137 kwa watumishi 76,332. Kati ya watumishi hao walimu ni 41,385 waliolipwa Tsh. Bil. 45.5 na watumishi wasio walimu ni 34, 947 waliolipwa Tsh. 91.6. Haya ni malimbikizo yaliyokuwa kero kwa watumishi kwa miaka na miaka. Halafu mtu anakuja kupotosha kuhusu maslahi ya watumishi hapa. Hapana! tutaongea ukweli.

Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha malipo ya malimbikizo kufanyika kwa kipindi cha miaka mitano katika historia ya nchi yetu.

2. Watumishi kupandishwa vyeo na madaraja.

Serikali ya awamu ya tano hadi August, 2020 imewapandisha madaraja na vyeo watumishi wapatao 246,637. Kati ya watumishi hao, walimu 161,655 walipandishwa vyeo na kulipwa Tsh. Billioni 33.28, watumishi wasio walimu ni 91,982 waliolipwa Tsh. 27.47.

Serikali yoyote duniani ni lazima itambue watumishi wake, na kuwathamini kwani ndio nyenzo na kichocheo cha maendeleo katika nchi. Serikali imekusudia kuendelea kupandisha vyeo watumishi wake watakaokidhi vigezo kama inavyohitajika zaidi.

3. Nyongeza ya mwaka ya mshahara (Annual Increment).

Baada ya zoezi la uhakiki wa watumishi kukamilika Serikali ilitoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wa umma 505,985 kwa mujibu wa utaratibu. Jumla ya Tsh. bilioni 72.8 ziliongezeka, kati ya kiasi hicho Tsh. 37.2 zililipwa kwa walimu 270,878 na Tsh. bilioni 35.7 zililipwa kwa watumishi wasio walimu.

4. Ongezeko la mishahara kwa kiwango kisichotozwa kodi.

Pamoja na kupandisha vyeo watumishi wa Umma, kulipa malimbikizo yaliyorithiwa kutoka awamu ya nne, kutoa nyongeza ya mishahara na ajira vilevile Serikali ya awamu ya 5 imepandisha kiwango cha mshahara usiotozwa kodi.

Hatua hiyo imeongeza imeongeza pato halisi la mshahara (take home) kwa wastani wa Tsh. 100,000/= kwa kila mfanyakazi wa umma na sekta binafsi. Kwa kipindi cha mwezi July, 2020 hadi June, 2021 Serikali itatumia Tsh. billioni 517 kama ongezeko la pato halisi kwa watumishi wa umma. Hatua hii imeanza kutekelezwa kuanzia mwezi July, 2020. Halafu mtu aseme tofauti kwa maslahi ya watumishi wa umma.

5. Ajira mpya.

Serikali zote duniani haziwezi kuajiri watu wake wote peke yake isipokuwa ni lazima iwezesha na kuweka mazingira mazuri ya watu kuajiriwa na kujiajiri pia. Serikali ya awamu ya 5 imezalisha ajira nyingi kwa kuwezesha sekta binafsi kuajiri lakini pia Serikali yenyewe kuajiri jumla ya vijana 66,178. Jumla ya Tsh. billioni 54.9 zimeongezeka kila mwezi katika sekta ya ajira. Hapo unazungumza watumishi zaidi ya elfu 14 kwenye sekta ya afya, sekta ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ambayo nayo imezalisha ajira nyingi sana. Kulipa madai yasiyo ya mishahara na kutoa mikopo isiyo na riba kwa watumishi wa umma.

Hadi kufikia Agost 2020, Serikali ya awamu ya tano imelipa madai ya watumishi yasiyo ya mishahara kiasi cha Tsh. billioni 358.1. Malipo hayo yamefanyika baada ya kuhakikiwa na kuondolewa malipo bandia yaliyokuwa yameghushiwa tu na wajanja.

Aidha, Serikali ya awamu ya 5 imefanikiwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa watumishi wa umma. Jumla ya Tsh. billioni 54.8 zimetumika kwa ajili hiyo hadi sasa. Mambo yote haya yamefanyika na serikali kwa kutambua wajibu wake kwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi.

7. Kulipa mishahara ya watumishi wa umma mapema na kwa wakati.

Leo kutoka kwenye kero ya watumishi kucheleweshewa mishaharo yao sasa watumishi wanateleza tu. Yani kabla ya mwezi haujaisha tarehe za mapema kabisa kuanzia Oktoba 23-27 mshahara unakua umeingia. Nani huyo anananga kazi kubwa ya kuboresha maslahi ya watumishi umma iliyofanyika?

8. Kudhibiti mfumuko wa bei na utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania ili mshahara wa Mtumishi uendelee kuwa na nguvu.

Hili ni eneo ambalo Serikali ya awamu ya 5 imejitahidi sana kwa kuhakikisha hapawi na mfumuko wa bei ya bidhaa na huduma kwa kuendelea kubaki kuwa ndani ya wigo wa tarakimu 1 kwa wastani wa asilimia 4.4 toka mwaka 2016 hadi sasa na nguvu ya hela yenyewe hata ikiwa mia 1. Hii ni katika kuhakikisha hela anayopata mtumishi kwenye mshahara wake inaendelea kuwa na nguvu na imara zaidi. Sasa hawa wanaopotosha haya akina nani? Shubash!

#MITANO TENA.
Hakika wapinzani hawana hoja hao wanabwabwaja tu
 
Hivi wapinzani wanaweza kupaisha na wapiga kura wasiozidi milioni 1? Wapiga kura walio wengi hawajui hata maana ya daraja( wanadhani ni lile la mkapa/Dar), annual increament n.k
 
Keep kubwa ya Wafanyakazi Ni mafao

Watu hawalipwi, wanazungushwa miezi na miezi. Mifuko haina Pesa

Nasikia wamechukua Pesa na kupeleka kwenye Kampeni.

Wafanyakazi wanajua hujuma za CCM
Njoo na hoja zlizo waz, huko kuckia ckia kla mtu anasema lake.
Mm mwenyewe nmeskia eti lissu mtoto cio rizki 😄😄
 
Hii article ina rudiwa rudiwa sana kupostiwa humu na watu tofauti tofauti...

Inavyoelekea hii imewaingia sana Team Magufuli Campaign na inawaumiza sana na sasa wanajaribu ku - minimize damage yake...

Huyu ni mtu wa nne kuleta kitu hikihiki kwa hoja zile zile na takwimu zilezile...

Jibu ni moja tu, wanajitetea tu. Wanajaribu kuendelea kutudanganya watumishi. Wanadhani sisi ni wajinga kama wao...

Sisi ndiyo watumishi wenyewe. We know every thing kuwa kwa miaka mitano;

1. Hakuna nyongeza yoyote ya mshahara kwa watumishi wote wa umma..!

2. Maelfu ya wafanyakazi bado wanadai malimbikizo ya mishahara yao, madeni ya likizo, matibabu, masomo nk

3. Maelfu ya watumishi wa umma hawajapandishwa vyeo (promotion) huku wakiwa tayari wanastahili...

4. Maelfu ya wazee wetu wastaafu waliostaafu ktk vipindi tofauti tofauti wengine miaka 2, mwaka 1, miezi 6 au 3 hawajalipwa viinua mgongo vyao na hakuna sababu yoyote sensitive...!!

Hili la maslahi ya watumishi ni eneo jingune ambalo Bw. John Pombe Magufuli amefeli sana ktk miaka yake mitano ya Urais kinyume kabisa na ahadi zake mwenyewe kwa mdomo wake...!!

Huyu ni sharti AHUKUMIWE tu hapo Oktoba 28, 2020....
Ukiona hvo ujue watu wameona mnavofanganywa na wapinzani nanyi mnakubali
 
Hivi wewe uliepost hii article ambayo kila siku naiyona una akili zako nzuri kweli? Sisi watumishi tunajua alichotufanyia Huyo shetani wenu mwenye roho mbaya utafikiri anauza sum.Umeandika uharo kuja kuaminisha watu huo uoumbavu ,watumishi tushakubaliana na ndugu zetu kura zetu hapati.
Jidanganye tu
 
Del
Na Bwanku M Bwanku

Hekaheka na pilika za kampeni zinaendelea kutimua vumbi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi kwa wagombea wa Urais, wabunge na madiwani kunadi Sera na Ilani zao wanazoenda kuzitekeleza kwa miaka mitano ijayo kama wananchi wakiwapa ridhaa yao.

Kwa bahati nzuri sana nimeendelea kufuatilia kwa kila jambo linaloendelea kwenye kampeni hizi na leo kwa uchache kidogo nitazungumzia kwa uchache tabia ya upotoshaji inayotumiwa na kuota mabawa kwa baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali.

Ukiachana na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kuwakashfu kwa kutweza utu na heshima ya watumishi wetu wa umma wote wanaofanya kazi kubwa usiku na mchana kwa kuwaita watu waliokotwa majalalani lakini zaidi nimesikia mara kadhaa wagombea haohao wa vyama vya upinzani wakipotosha kuhusu maslahi ya watumishi wa umma na mambo mbalimbali yanayowahusu watumishi wetu.

Nimewasikia wakipotosha waziwazi kuhusu hoja ya maslahi kwa watumishi wa umma bila hata ya kuogopa kama maneno yao yanaweza kuichonganisha Serikali, jamii na watumishi wetu wanaofanya kazi kubwa sana. Sasa njia ya muongo ni fupi na wala hakawii kuumbuka.

Kimsingi Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt. John Pombe Magufuli imeshughulikia maslahi ya watumishi wa umma kwa kiasi kikubwa sana tangu iingie madarakani Novemba 2015 hadi sasa.

Zifuatazo ni hatua mbalimbali na chache tu kati ya nyingi zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya 5 kushughulikia changamoto na maslahi ya watumishi wa umma wote nchini. Nayasema haya ili kuondoa huu upotoshaji wa wachache wasiolitakia mema Taifa letu. Twende pamoja.

1. Malipo ya malimbikizo ya mishahara.

Mpaka Novemba, 2020 Serikali imelipa Tsh. Billioni 137 kwa watumishi 76,332. Kati ya watumishi hao walimu ni 41,385 waliolipwa Tsh. Bil. 45.5 na watumishi wasio walimu ni 34, 947 waliolipwa Tsh. 91.6. Haya ni malimbikizo yaliyokuwa kero kwa watumishi kwa miaka na miaka. Halafu mtu anakuja kupotosha kuhusu maslahi ya watumishi hapa. Hapana! tutaongea ukweli.

Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha malipo ya malimbikizo kufanyika kwa kipindi cha miaka mitano katika historia ya nchi yetu.

2. Watumishi kupandishwa vyeo na madaraja.

Serikali ya awamu ya tano hadi August, 2020 imewapandisha madaraja na vyeo watumishi wapatao 246,637. Kati ya watumishi hao, walimu 161,655 walipandishwa vyeo na kulipwa Tsh. Billioni 33.28, watumishi wasio walimu ni 91,982 waliolipwa Tsh. 27.47.

Serikali yoyote duniani ni lazima itambue watumishi wake, na kuwathamini kwani ndio nyenzo na kichocheo cha maendeleo katika nchi. Serikali imekusudia kuendelea kupandisha vyeo watumishi wake watakaokidhi vigezo kama inavyohitajika zaidi.

3. Nyongeza ya mwaka ya mshahara (Annual Increment).

Baada ya zoezi la uhakiki wa watumishi kukamilika Serikali ilitoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wa umma 505,985 kwa mujibu wa utaratibu. Jumla ya Tsh. bilioni 72.8 ziliongezeka, kati ya kiasi hicho Tsh. 37.2 zililipwa kwa walimu 270,878 na Tsh. bilioni 35.7 zililipwa kwa watumishi wasio walimu.

4. Ongezeko la mishahara kwa kiwango kisichotozwa kodi.

Pamoja na kupandisha vyeo watumishi wa Umma, kulipa malimbikizo yaliyorithiwa kutoka awamu ya nne, kutoa nyongeza ya mishahara na ajira vilevile Serikali ya awamu ya 5 imepandisha kiwango cha mshahara usiotozwa kodi.

Hatua hiyo imeongeza imeongeza pato halisi la mshahara (take home) kwa wastani wa Tsh. 100,000/= kwa kila mfanyakazi wa umma na sekta binafsi. Kwa kipindi cha mwezi July, 2020 hadi June, 2021 Serikali itatumia Tsh. billioni 517 kama ongezeko la pato halisi kwa watumishi wa umma. Hatua hii imeanza kutekelezwa kuanzia mwezi July, 2020. Halafu mtu aseme tofauti kwa maslahi ya watumishi wa umma.

5. Ajira mpya.

Serikali zote duniani haziwezi kuajiri watu wake wote peke yake isipokuwa ni lazima iwezesha na kuweka mazingira mazuri ya watu kuajiriwa na kujiajiri pia. Serikali ya awamu ya 5 imezalisha ajira nyingi kwa kuwezesha sekta binafsi kuajiri lakini pia Serikali yenyewe kuajiri jumla ya vijana 66,178. Jumla ya Tsh. billioni 54.9 zimeongezeka kila mwezi katika sekta ya ajira. Hapo unazungumza watumishi zaidi ya elfu 14 kwenye sekta ya afya, sekta ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ambayo nayo imezalisha ajira nyingi sana. Kulipa madai yasiyo ya mishahara na kutoa mikopo isiyo na riba kwa watumishi wa umma.

Hadi kufikia Agost 2020, Serikali ya awamu ya tano imelipa madai ya watumishi yasiyo ya mishahara kiasi cha Tsh. billioni 358.1. Malipo hayo yamefanyika baada ya kuhakikiwa na kuondolewa malipo bandia yaliyokuwa yameghushiwa tu na wajanja.

Aidha, Serikali ya awamu ya 5 imefanikiwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa watumishi wa umma. Jumla ya Tsh. billioni 54.8 zimetumika kwa ajili hiyo hadi sasa. Mambo yote haya yamefanyika na serikali kwa kutambua wajibu wake kwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi.

7. Kulipa mishahara ya watumishi wa umma mapema na kwa wakati.

Leo kutoka kwenye kero ya watumishi kucheleweshewa mishaharo yao sasa watumishi wanateleza tu. Yani kabla ya mwezi haujaisha tarehe za mapema kabisa kuanzia Oktoba 23-27 mshahara unakua umeingia. Nani huyo anananga kazi kubwa ya kuboresha maslahi ya watumishi umma iliyofanyika?

8. Kudhibiti mfumuko wa bei na utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania ili mshahara wa Mtumishi uendelee kuwa na nguvu.

Hili ni eneo ambalo Serikali ya awamu ya 5 imejitahidi sana kwa kuhakikisha hapawi na mfumuko wa bei ya bidhaa na huduma kwa kuendelea kubaki kuwa ndani ya wigo wa tarakimu 1 kwa wastani wa asilimia 4.4 toka mwaka 2016 hadi sasa na nguvu ya hela yenyewe hata ikiwa mia 1. Hii ni katika kuhakikisha hela anayopata mtumishi kwenye mshahara wake inaendelea kuwa na nguvu na imara zaidi. Sasa hawa wanaopotosha haya akina nani? Shubash!

#MITANO TENA.
D
Delete ccm Oct 28
 
1. Malipo ya malimbikizo ya mishahara.

Mpaka Novemba, 2020 Serikali imelipa Tsh. Billioni 137 kwa watumishi 76,332. Kati ya watumishi hao walimu ni 41,385 waliolipwa Tsh. Bil. 45.5 na watumishi wasio walimu ni 34, 947 waliolipwa Tsh. 91.6.
Mkuu November 2020 imeshafika?
 
Mwenyewe JPM kasema hasinge obgeza mshshara akaacha kujenga reli sas hizo ngonjera unazogani unamsemeaje alambayo mwenyew kaa admit kutoongeza. Rubish
 
Yajayo yanafurahisha CCM oyee
1600096841036.png
 
Wewe sio mtumishi wa serikali hii dhalimu....unachofanya ni kujitoa tu ufahamu!
Haya weka na namba yako ya simu kenge wenzio wakupe teuzi!
UMENIKERA...
Uwe unaongea kwa fact kama huna data ni Bora ukae kimya sio kupinga makala ya mtu aliyefanya utafiti.
 
Siamini kama umeandika ukiwa na akili zako timamu mkuu kuna mambo machache aidha umepiga Kitwanga zako za kutosha ama upo hospitali malaria ipo juu sana. Ni hayo mkuu
Ni vyema ukatoa kilichopo kwenye ubongo wako bila kukashifu makala ya mwenzako.
 
Back
Top Bottom