Hoja ya maslahi ya watumishi wa Umma inavyopotosha na Wapinzani

 
Nilidhani unajibu hoja kumbe unatukana?
 
Acha kushabikia sababu ya ukabila hilo jina lako linatosha kabisa kueleza kilichopo kichwani mwako
Ndiyo hiyo ninayosema kwamba unapinga kwa sababu ya kupinga tu. Nimekuambia mimi mwenyewe nilikuwa mtumishi serikalini kwa miaka 11. Dada zangu wawili walikuwa waalimu huko mikoani. Mmoja alistaafu miaka mitatu iliyopita na mwingine kastaafu miezi michache iliyopita. Walikuwa wanakaa hata miezi mitatu bila mshahara. Wanafanya kudunduliza hapa na pale kwa kuwa walikuwa vijijini na sisi ndugu zao tunasaidia kidogo kidogo mpaka mwezi ufuatao. Naeleza mambo yaliyonisibu mimi mwenyewe. Wewe unaleta mambo ya ukabila; kwamba nisemayo ni kwa sababu tu ya kabila langu. Kwanza kabila langu siyo unalodhania, pamoja na kutumia jina la kabila unalodhania. Labda wewe ndiye unapinga kwa sababu tu ya utofauti wa kabila lako tu.
 
Acha kuongea upuuzi wako hapa, 2015 unadhani wote tulikuwa wajinga tulikuwa hatuoni?
 
Unaongea utadhani nchi imepata uhuru 2015, watu wa kusifiwa ni akina Mkapa na JK wamefanya mambo mengi lakini siyo wapenda sifa.
 
Wewe ni mgonjwa,kwa nini umeandika mtiririko wa mambo ya uongo mtupu tena bila aibu?Hizi taarifa chanzo chake ni hapo hapo Lumumba?Polepole na Magufuli wanafahamu kuwa umewaadhiri kwa kiasi hicho?
 
Bwanku M Bwanku
Watumishi waliopanda mara ya mwisho 2015 kabla ya october hawajapandishwa hadi naandika hapa.Wanaowapa taarifa wanawadanganya.
Kachungulie upya.
 
Huihitaji utafiti,watumishi waseme wenywe.
Nikupongeze sana Mwandishi wa Makala hii iliyojaa hoja za nguvu na tafiti zenye data,Hii inaonesha jinsi serikali inavojitahidi kuhakikisha wafanyakazi wanapata maslahi yao na kuongeza utendaji kazi katika sekta zao.
 
Mijitu kama nyinyi mnakuwaga michawi, watumishi tunakandamizwa wewe unajipendekeza kwa serikali kandamizi kuwahi kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ki ufup umedanganya sana, serikali ya hawamu ya 5/hajawasaidia chochote watumishi wa umma, kuna watu wameajiriwa tangu 2013 , 2014, 2015,....na hadi sekunde ya leo hawajawahi panda daraja hata siku moja. Pia mwaka/ hapa nakupa mfano Mh Kikwete hadi anaondoka madarakani mwalimu mwenye Digrii aliye muajiri mara ya mwisho ni 2015 alimuacha kwemye msharaha wa shilingi TGTD D1, 716,000/= baadae Magufuli aliongeza na kwa huyo mwalimu hadi shiling el 733,000/= Hadi sekunde hii yaani hakuna kitu kimebadilika kwenye mshahara, juzi kwa mwalimu huyohuyo Magufuli kampunguzia kodi ya takribani shiling elf 32,000/= tu, leo unabwatuka. Lakini ki msingi huyu mwalimu wa 2013,2014 na 2015 alipaswa awe amepanda daraja ila hamna kitu leo unaleta uongo laana itakutafuna wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…