Hoja ya Mpina kuhusu upasuaji wa kuongeza makalio yazua mjadala Bungeni

Hoja ya Mpina kuhusu upasuaji wa kuongeza makalio yazua mjadala Bungeni

MJADALA mkali umeibuka bungeni kuhusu upasuaji kurekebisha maumbile, ikiwamo kupunguza au kuongeza ukubwa wa makalio katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa (CCM), ndiye aliyeibua zogo bungeni jijini, alipotoa hoja kwamba MNH-Mloganzila imeanzisha huduma hiyo kinyume cha Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007.

"Hakuna mahali kwenye Sera ya Afya yetu ya Mwaka 2007 imeruhusu jambo hili. Operesheni ya matibabu, operesheni kwa ajili ya kuongeza makalio; ni operesheni ya kimapambo (cosmetic surgery), si ya mtu ambaye ana changamoto yoyote ile ya afya.

Baada ya Mpina kutoa kauli hiyo, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby, alisimama na kumpa taarifa Mpina, akisema hata kiuno kikikaa vibaya nayo ni changamoto ya kimatibabu.

"Kwahiyo, kukiweka kiuno vizuri, ni kusababisha binadamu atembee vizuri na aweze kuwa na umbo zuri," alisema Shabiby.

Hata hivyo, Mpina alikataa kupokea taarifa hiyo ya mbunge mwenzake, akisisitiza serikali imeanzisha huduma hiyo bila kibali cha Bunge wala hakuna sheria, kanuni na mwongozo wa utoaji huduma hiyo.
Vitu vingapi vinafanyika bila kibali cha bunge amewahi kuhoji?? Wanaacha kuhoji sensitive issues anahoji ujinga wa mtu mmoja mmoja.
 
Sidhani kama kuna nchi inayojielewa duniani inaweza ruhusu taasisi zake za kutoa huduma ya afya zifanye implants surgeries.

We ukiona waziri kama Molel ndio ana promote hiyo biashara inakueleza jinsi huyo mtu alivyo wa hovyo. Serikali aitakiwi ku promote mambo ya urembo hasa kwa kuwaasa watu wapasue miili yao ili kufikia hiyo azma.

Mara pekee nchi zinazojitambua wanafanya cosmetic surgery ni uso wa mtu umeharibika sana kwa sababu za kiafya au ajali, deformation ya matiti kwa sababu za biology au afya ndio wanaruhusu, huko kwenye wowowo ndio kabisa uwezi sikia.

Isitoshe huko kwao hao private surgeons wana experience ya miaka mingi sana kama surgeons, baadae wana specialise ndio wanapewa hivyo vibali, kuna elimu kubwa ya jamii inatolewa on associated risks zilizopo wakati wa kufanya na baada ya hizo surgery.

Ndio maana watu wanakimbilia nchi kama za India, Turkey na kwengineko kwa hovyo wanazofanya hizo operation. Bado kuna muda wa ku asses hizo operation kila baada ya miezi kadhaa si chini 3 au 4 kwa mwaka.

In short ni maamuzi ya hovyo sana ethically serikali ku promote huo upuuzi kwenye jamii. Uwezi wapangia watu miili yao waongeze au wapunguze nini, lakini si busara ku-promote hayo mambo.

Tells you nchi ilipo.
 
Hivi huyo mpina huko mbungeni ndo nani? Au yule aliyekuwa waziri wa uvuvi akipokea rushwa ya 5M kwa kila mvuvi kanda ya ziwa ili asimchomee nyavu zake wala kumpa kesi ya uhujumu uchumi?
 
Jimboni kwake kuna mambo mengi ya kufanyia kazi, kama hilo halimuhusu, apite kule. Nchi lazima isonge mbele katika masuala ya sayansi
Asifanye masihara kwenye suala lenu la kuongeza makalio yenu kabisa, ama vipi?
 
Ila Betina angeenda na yeye aongeze tunyama nyama kidogo ili joho limkae vizuri.

Ikimpendeza zaidi hata ile sura angeifanyia touch up kidogo itoke ubabani hasa lile tabasamu lake pana.
 
Hivi huyo mpina huko mbungeni ndo nani? Au yule aliyekuwa waziri wa uvuvi akipokea rushwa ya 5M kwa kila mvuvi kanda ya ziwa ili asimchomee nyavu zake wala kumpa kesi ya uhujumu uchumi?
Alienda na ruler canteen ya bunge kupima urefu wa samaki.
 
Kuna kitu kinaitwa cross subsidisation. Mapesa yanayolipwa na wale wa kutaka kuongeza makalio ndio itatumika kuwapunguzia wengine gharama za tiba.

Amandla...
 
Hata hoja yake hujaisikiliza na kuielewa wewe unakurupuka tu kujibu

Huyo aliyeungua si ni mgonjwa huyo, Mpina anaongelea mtu asiye na ugonjwa ila kaona hana tako anataka kuliongeza ana nyonyo ndogo anaenda kuongeza na anasema hii surgery haipo kwenye sera ya ya taifa kiasi kwamba mtu akipata madhara hawezi kusaidika maana kitu kisichotambulika kimechomekwa tu
Sera ya afya ya 2007 ndio iamue maamuzi ya 2024? Yaani gap ya miaka 17? We can't be serious. Hiyo sera tukiweka yote ambayo haijaongelea sidhani hata MRI scan zingenunuliwa au bima kwa wote ingepitishwa!!
 
Watu wanapenda mkndn mikbw ukiona hivyo

Ova
 
Kwahiyo shabiby alisimama na hiyo ndio taarifa iliyomsimamisha?
Kuna watu wapo bungeni najiulizaga hawa ndio watunga Sheria hawa.
 
Hata hoja yake hujaisikiliza na kuielewa wewe unakurupuka tu kujibu

Huyo aliyeungua si ni mgonjwa huyo, Mpina anaongelea mtu asiye na ugonjwa ila kaona hana tako anataka kuliongeza ana nyonyo ndogo anaenda kuongeza na anasema hii surgery haipo kwenye sera ya ya taifa kiasi kwamba mtu akipata madhara hawezi kusaidika maana kitu kisichotambulika kimechomekwa tu
Mpina akili kubwa
 
Huyo mpina ni takataka, kuna watu wanapata ajali za moto, wanahitaji juduma hizo kuweka sura zao sawa, yeye akili yake imekaa kuwaza makalio tu
Shida yako,ni uelewa mdogo,akili ndogo na chuki kwa mpina.ni vigumu kujua mpina ameongea nn.
 
Back
Top Bottom