Kwenye issue hii nakumbuka Chadema walisema hivi: 1) Chadema hawajamteua mbunge yeyote wa viti maalum kwenda bungeni 2) Wabunge 19 waliodai wameteuliwa "walijiteua wenyewe" 3) Kwa sababu hiyo, waliojiteua wamekiuka utaratibu wa chama na hivyo wamefukuzwa uanachama. Kwa upande wa 'walioteuliwa au waliojiteua', baada ya kuona kama wamefukuzwa chama, wakakata rufaa kwa ngazi ya juu ya chama. Kwa maoni yangu, kukata kwao rufaa ni ushahidi kwamba wanatambua kuwa wamefukuzwa uanachama na hiyo inawafanya pia wakose sifa ya kuwa wabunge wa chama cha siasa kama walivyokuwa wakidai kuwa wako bungeni kwa baraka za chama chao. Na rufaa hiyo ndiyo ingeweza kuwarudishia uanachama endapo kama ingetupilia mbali uamuzi wa chama. Alternatively, rufaa nyingine nje ya chama (mfano mahakamani), ingeweza pia kuwarudishia uanachama endapo ingetupilia mbali uamuzi wa chama. Kwa vile uamuzi wa A au B haujafanyika, bado uamuzi wa chama unabaki kama ulivyo.