Hoja yangu kuhusu Lengai Ole Sabaya aliyekuwa DC wa Hai

What?? Umekosea sana kujenga hoja yako, labda wewe ndiyo Sabaya mwenyewe, au mfuasi wake! Ukiteuliwa ndo ufanye ujinga kisa mfumo? Huo mfumo kina RC wake Sabaya walikuwa kwenye mfumo tofauti? Yaani wewe mtu mzima ukiambiwa kunya hadharani utakunya? eti kisa umeambiwa hivyo na mkubwa wako? Kuna DCs na RCs wengi tu wako kwenye Majimbo ambayo yalikuwa ngome za upinzani, lakini wamejitahidi kutumia busara na akili za ziada ili kuendana na mfumo, huku wakiishi kwa akili na wananchi na maisha yanaenda mpaka leo. Next time Sabaya na watu wa aina yako mjifunze utu, ukiteuliwa fanya kazi yako kwa ufasaha, tenda haki, chapa kazi za kimaendeleo zaidi, ili hata Mteuzi wako akikuondoa basi unakuwa na amani na nafsi yako, na wananchi, na Mungu wako pia. Tukumbuke huwa lazima mtu huondoka tu hakuna anayedumu milele kwenye ofisi ya umma, hasa kwa hizi nafasi za uteuzi.
 
Tusijifiche nyuma ya makosa ya kiufundi,Sabaya anatakiwa kuwa jera,yawe makosa ya kimfumo au la,hakuna shaka kwamba huyu jamaa alitumia madaraka vibaya,
Ma DC waliokuwa wanachapa watu viboko,haiitaji kuwa na shahada ya sheria kugundua kwamba walivunja sheria,Sabaya,Makonda,Ali API,lile fala na kubwa jinga la Mbeya,yote yanastahili kuwa jera.
 
Siku hizi hamna mwenye hofu ya Mungu, mtu yuko radhi kafanya Jambo analojua lipo kinyume kabisa na haki hata mbele ya mwenyezi Mungu ili tu amfurahishe Fulani. Bila kujua yuko Mkuu zaidi ya huyo anayempa jeuri ambaye akiamua chochote kufumba na kufumbua mambo yanabadilika.
Tujitahidi kusimamia haki, Dunia hii tunapita tu & tuache dhulma.
 
Pole mkuu. Kubalini kwamba Sabaya sio DC tena na msiache kusindikiza atakapopelekwa mahakamani
 
Mbona kuna wakuu wa wilaya kibao na walikua hawafanyi upumbavu kama wa huyo taahira
Taja upumbavu mmoja tu, uliouona ktk utendaji wa Sabaya. Usiniambie yeye siyo mchaga, hapo sitakuelewa maana nalo najua ni tatizo.
 
Sabaya= Saa mbaya, ndiyo maana saa zote hakuwa mtu mwema.

Saa mbaya Wamasai hutamka Sabaya.
 
Good analysis. Thank you
 
Hata mama pia alikuwa kwenye mfumo huo huo. Alimuonea nani? Kuna mtu leo hii anaweza kusimama na kusema....makamo wa Rais JPM alinifanyia ubaya fulani? Well unaweza kusema hakuwa mtendaji kwa cheo chake....lakini ni suala la hulka ya mtu tu. Angekuwa muonezi ungemsikia tu, akikanyaga watu ili kupata sifa kwa bosi wake!

Tizama mkuu wa mkoa kama Mh Mtaka.....alifanya kazi na bado anaendelea kufanya kwa weledi na mafanikio sana. Huwezi kusikia "amekanyaga" wananchi hovyo....but then tizama Makonda!
 
Kwahiyo tukisema Sebaya alikuwa "Punda" hakuna kosa???!!😲
Yeremia 17.5 Bwana asema hivi, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu , amfanyaye mwanadamu kinga yake na moyo wake umemwacha Bwana, maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema, bali atakaa jagwani palipo ukame. Alimwacha Bwana akamtegemeaMagufuli sasa amekufa hana wa kumlinda kwa madhambi na maovu aliyowatendea watu.
 
You are right. The entire system was abnormal.
 


Lakini huyo ni Punda, punda anayo excuse.🤣 the Biblical verse has nothing to do with an animal.
 
Wakuu wa mikoa na wilaya wana faida gsni nchi hii ?
Rubbish
 
Ndio, hata damu ya Ben Saa8, italipwa kwa waliomuua na hata walio shangilia watavuna!
 

Kosa la kimfumo.!!? Hata kuua na kuharibu mali za watu? Kutumia Magari yenye namba bandia za UN kwenda kufanya uhalifu??

Basi atakuwa hana akili kama alikuwa anafanya kila analoambiwa na hayati Rais Magufuli akisindikizwa na kauli ya "...you have my full support.."

Sasa huyu "you have my support" is NO MORE, IS DEAD. Nani atamlinda na kum - support tena kwenye uhalifu wake? MUNGU wake kafa, hayupo...!!

Wahenga wanasema hivi, "..za kuambiwa changanya na zako..."

Sasa huyu Sabaya hata kutumia akili kidogo tu kujua anayemwambia "you have my full support" yeye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kosa lolote, akawa hata hajui...

Mwambie hivi alipaswa kuelewa kuwa "za kuambiwa" ilikuwa ni lazima "achanganye na za kwake"..

Sasa huyo nduguyo atafungwa jela. Ni swala la wakati tu hilo na ndipo atakapojua kumbe wakati mwingine tutumie akili kuishi na kutenda tukiwa ndani ya mfumo...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…