Hoja yangu kuhusu Lengai Ole Sabaya aliyekuwa DC wa Hai

Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Sabaya kupisha Uchaguzi juu ya tuhuma zinazomkabili.
Kama umelijua hilo basi ujue mfumo wa sabaya haukua wa haki ni wa uonevu sasa umekuja mfumo wa haki tulieni haki itendeke
 

AKipelekwa kwa Pilato huyo aliyesema ana full support aje kumsaidia.
 
Alikuwa katili kama hitler
 
Umejitahidi sana kumtetea , kiukweli Majambazi mnajua kulindana.
Lakini kwakuwa lakuvunda halina ubani mkamdanganya aende clouds akaongee kumbe ndio mmeharibu.
Sabaya ni mshenzi sana, watu tunakunywa Riverbills hapa Ngarenaro tulikuwa tunashuhudia uchafu wake.


Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Atakuwa ni sabaya mwenyewe anavinjari humu
 
Kitendo cha kustopishwa kupisha uchunguzi ni tayari kuna chochote kitu na majibu yapo.subiri majibu yake sasa
 
Usishangae 2025 Sabaya akawa anasafishwa hadharani na Chadema kama walivyofanya kwa Lowasa

Na hapo ndio utajua fisadi mchafu ni nani kati ya huyo sabaya na chadema🤣🤣🤣🤣
Huu lzm utakuwa ujinga wa hali ya juu sana
 
Sabaya alikuwa na haki ya kukataa shinikizo lolote la huo unaoita mfumo

MaDC wote huwa wanakula kiapo kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao sehemu walizopangiwa; na katika kiapo hicho wanaapa kuwa WATAILINDA na KUITETETA katiba ya nchi ambayo ndio sheria mama!! Sasa kama Sabaya alishindwa kuheshimu na kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizotokana na katika hiyo aliyoapa kuilinda basi hana sababu ya kusingizia eti alikuwa anatimiza matakwa ya JIWE!! Huko ni kujitetea tu kwasbabu Jiwe katutoka!! He should pay the price!!!
 
Marehemu kichaa alichagua vichaa wengi wamsaidie
 
Sawa na akimaliza hapo aende moja kwa moja kwa Dar es salaam ya zamani!
 
Umekosoa kilichofanywa na wenginna baada tu ya kuwakosoa na wewe ukafanya kile kile. Labda kosa lao wao ni kuonesha baadhi ya hizo tuhuma halafu wewe kuka na kumtetea na kusema kuwa kwako wewe yote aliyoyafanya wala sio tatizo na hivyo si hatia. Nadhan pia umeingilia hiyo tume kama ulivyokataza wengine. Nafhani ungesema sentensi moja tu kuwa

"Tuipe tume nafasi ifanye kazi yake na itoke na maamuzi baada ya uchunguzi huru".

Ila, ukipitia post ya Malisa, G. Kuna mengi ya kujifunza na tume wanaweza pata pa kuanzia.
 
Walishaambiwa mwenzao(mwanakwendazake!) ana kinga, kwamba huyo anaye walinda kuna siku hatakuwa madarakani, wakabisha!
 
Umeshachukua bahasha ya khaki tayari! Unawananga wengine kuwa wanapotosha uchunguzi huku nawe ukifanya yaleyale ya kuwapa majibu ya task yao kuwa mfumo ubebe lawama na makosa! Ni mfumo upi uliokuwa unampa baraka za kubaka, kupita, kuumiza na hata kuua? Ni mfumo upi uliokuwa unampa mamlaka ya kuvamia wilaya nyingine zenye wakuu wa wilaya Kama yeye na walioteuliwa na mfumo unaofanana kwenda kufanya uhalifu huko?
Mfumo gani uliokuwa unampa baraka za kumdharau mkuu wake wa mkoa?
Mwandishi nawe umeshiriki kula haramu ujue! Unayemsadisha hasafishiki hata kwa kumbabua na maji Moto Kama kuku! Atakutwa na hatia tu hata umtetee vipi!
Hongera kwa kumchuna Sabaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…