HOJA YANGU: Mfumo ulio tumika kwa matokeo mwaka huu CSEE ni mfumo BORA KABISA{BEST EVER}

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,903
Reaction score
1,979
Heshima mbele wakuu!
Matokeo ya O level 2013 yametangazwa na kumezuka taharuki juu ya ongezeko la ufaulu kwa over 15% na madaraja mapya ya div 1V ya 46 na div 0 ya 41!!
Karibu tufuatane kwenye hoja hii:

KWANINI NINADHANI MFUMO WA MWAKA HUU NI BORA ZAIDI

Kabla ya mwaka jana,NECTA walikuwa wakifanya yafuatayo:

1: Mwanafunzi alipimwa baada ya miaka minne,by a single paper,at one sitting,kuamua amemudu vipi masomo yake.
Jambo hili lilipelekea baadhi ya wanafunzi,walio fanya vizuri toka form 1 hadi form 4 kutofanya vema sana katika mtihani wa mwisho.
Mathalani,mtu anaweza kupata A somo toka form one hadi form four,lakini akateleza na kupata C NECTA,na inafahamika kwamba mtahiniwa ana uwezo wa C kwenye somo husika,kinyume cha uhalisia!

Hali ipoje sasa?
Kwa kuanzia mwaka jana,ni lazima marks 40% kwenye NECTA zitokane na Continuous Assessment kwa utaratibu ufuatao:
  • Mtihani wa National Form Two unachangia 15%.Mtihani wa MOCK form four unachangia 15%.Mtihani wa shule form Three marks 10%
Then,NECTA Form 4 inachangia 60%.

Utaratibu huu ni bora kuliko wa marks 100% kwa mtihani 1 kwa sababu zifuatazo:

i: Una akisi uwezo halisi wa mwanafunzi toka anaanza hadi kumaliza shule.

ii: Unapunguza udanganyifu,kwani mwanafunzi hapimwi kwa paper moja tu.

iii: Unahimiza juhudi endelevu kwa mwanafunzi,kwani kila kidato kinakuwa na uzito sawa.

2: MGAWANYO WA MADARAJA

Kabla,marks za ufaulu HASA ilikuwa ni C ambayo ilikuwa 41% yenye thamani ya 3 katika division,hivyo mtu akipata C 7 ni 7*3,na hvo ni Two ya 21 pts.

Sasa,Credit imebaki almost ile ile,40%[C],ila thamani yake imepunguzwa hadi 4,hvyo,mtu akipata C 7 ni 7*4,na ni div Three ya 28!!

Hivyo,hoja kuwa div za sasa ni rahisi kupata haina nguvu!!

Twende kwenye madaraja
Hapo awali,kulikuwa na madaraja matano: A,B,C,D na F yenye thamani 1,2,3,4 na 5 kwa mfuatano huo huo.
Interval toka daraja moja hadi jingine ilikuwa 20%,
yaani:
81-100 A,
61-80 B,
41-60 C,
21-40 D,
na
0-20 F.
Hapa kulikuwa na shida,gap ilikuwa kubwa mno,
kwa mfano,mtu akipata 21% na mwingne 40% ilihesabika wote wana D,lakini kimsingi,watu walio tofautiana 20% wamezidiana uwezo sana!!!
Kilichofanyika sasa ni KUPUNGUZA GAP KATI YA MADARAJA KUWA 10%,
Hvyo,sasa madaraja ni kama ifuatavyo:
0-20 F,
20-29 E,
30-39 D,
40-49 C[credit],
50-59 B,
60-74 B+,
75-100 A.
Thamani za madaraja ni 1,2,3,4,5,6 na 7 kwa A,B+,B,C,D,E na F respectively.
[B]Hii ni bora kuliko mwanzo,kwani,sasa utofauti wa madaraja una reflect uwezo wa mtu[/B].

[B]MGAWANYO WA DIVISION[/B]
1: Div 1 haijabadilika [pts 7-17],ambayo ni minimum B+ 4 na B 3.
2: Div Two ni pts 18-22[kama sijakosea] ambayo ni min B 6 na C moja.
3: Div 3 ni pts 23-31,ambayo ni min C 4 na D 3.

4: [B]DIVISION 1V[/B] ni min pts 47,ambapo [B]Lazima uwe na angalau D mbili au C moja[/B],Kinyume na hapo ni FAIL[DIV 0]

5: [B]DIVISION 0 ni pts zozote kati ya 41 hadi 47 ambapo mtu hana ANGALAU D MBILI AU C moja[/B], na pts 48-49[ambapo hapa mtu hawez kuwa na D2 au C1]

[B]CONCLUSION[/B]:
Kama umefuatana nami vema,hakuna mteremko ulio wekwa,bali thamani ya elimu yetu imeongezwa!
Haikuwa fair hata kidogo kuamua uwezo wa mwanafunzi at one sitting!
Nimeupenda mfumo mpya.
Haya ni mawazo yangu,
KARIBUNI KWA MJADALA.
 
Myakubanga



Vzur umetoa mchango mkubwa sana cz nahc nw wataelewa ingawa hapo kwe three nikwamba sasa inaanzia 25 bigup
 
Last edited by a moderator:
So unamaanisha Hapo zamani walikuwa hawafuati continuous assessment? Zile project zilikuwa za nini?,na ile mitihani mingine mbona ilikuwepo? Ama?
 
So unamaanisha Hapo zamani walikuwa hawafuati continuous assessment? Zile project zilikuwa za nini?,na ile mitihani mingine mbona ilikuwepo? Ama?

Zile zilikuwa geresha tu,marks 100 zote zilikuwa zinachukuliwa final.
Kwanza,shule nyingi zilikuwa zinapeleka project moja tu nzuri NECTA,nyingine wanabaki nazo.
Mitihani mingine ilikuwepo,ila ili contribute nothing kwenye final exam.
 
Zilikuwa hazitumik ndomana NECTA wakatangaza kuwa wanarudisha mtinda wa countnue assesmnt kama zaman maana ulisimamishwa wakidai kuwa xcl zingne walikuwa wakijaza matokeo ya huongo kwenje jarida
 
alama zilizokuwa
zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la
Taifa (Necta) katika kupanga matokeo
hayo, kwa kidato cha nne ni A=80-100,
B=65-79, C=50-64, D=35-49, F= 0-34 kwa
upande wa kidato cha sita A=80-100,
B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54,
S=40-44 na F= 0-39.
Alisema mfumo mpya, umehusisha alama
za kidato cha nne na cha sita na kuwa
kuanzia sasa A=75-100, B+=60-74,
B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na
F=0-19.
 

Karibu uchangie Molembe
 
Last edited by a moderator:
Zile zilikuwa geresha tu,marks 100 zote zilikuwa zinachukuliwa final.
Kwanza,shule nyingi zilikuwa zinapeleka project moja tu nzuri NECTA,nyingine wanabaki nazo.
Mitihani mingine ilikuwepo,ila ili contribute nothing kwenye final exam.

Usiongee vitu kama huna uhakika navyo. Toka mwanzoni wa miaka tisini, final exam zilikuwa zinachukua 60% na C.A 45%.
 
Mfumo unaotumika sasa ni mzuri an bora pia.
Muhimu ni utekelezaja ulio adilifu na makini.
Ukishaelewa vizuri mfumo huu hutapiga kelele juu ya madaraja, labda masuala mengine.
 
Usiongee vitu kama huna uhakika navyo. Toka mwanzoni wa miaka tisini, final exam zilikuwa zinachukua 60% na C.A 45%.

Kwa hyo mtihani ulikuwa na marks 105%?
Sina hakika na miaka ya 90,ila nina hakika toka miaka ya mwanzo mwa 2000,CA ilitakiwa ikontributi 10%,na hata hvyo hlo halifanyiki.
 
Kitu kingine ni kwamba, kuwepo na madaraja yanayo fanana kuanzia kindagate mpaka chuo kikuu kunasaidia kutathimini mwenendo wa elimu kwa ujumla. Hivyo inakuwa rahisi kugundua weakness and strength of our education.

Ombi jamani msi quote threaad maana ni ndefu.
 

politics hayo madaraja yaliyosemekana yalitumiwa 2012 hayakuwa yanafahamika kwa yeyote yule hata wakuu wa shule hawakuujua utaratibu huo.

hapa ndo yakuambiwa unachanganya na yako
 
Kwa hyo mtihani ulikuwa na marks 105%?
Sina hakika na miaka ya 90,ila nina hakika toka miaka ya mwanzo mwa 2000,CA ilitakiwa ikontributi 10%,na hata hvyo hlo halifanyiki.

Ha ha I mean 40%. Nikuhakikishia ndugu yangu haikuwa hyo 10 % ilikuwa 40 na imetumika mda wote huo.
 
Nimekupotezeq muda kivp kama uwelewa wako ni mdgo na mfinyu ndipo tatzo lako lilipo acha kuongea things bila vivid evidenc
 
Myakubanga

si kweli.

ukweli kabla sijaweka maelezo.

serikali haijawahi kutumia continuous assessment toka nchi ipate uhuru pamoja na kuwa sera ya continous assessment ipo muda mrefu sana,hata mwaka huu haijatumika kabisa,kumbuka mabadiliko ya madaraja na grades yalifanyika wiki mbili ama tatu kabla ya mtihani. na kuna shule hazikuwa na hizo marks kabisa,kuna shule watoto hawakuwahi kufundishwa wala kufanya mtihani wa somo moja ama mawili toka form one mpaka form four,marks za continous assessment zilitoka wapi?ama za kutengeneza?


narudi kwenye hoja zangu.

1.huu mfumo bado si bora na umetoa upendeleo zaidi kwa kundi moja na kunyonya jingine,hivi mtu mwenye A ya 75 analingana uwezo na mwenye A ya 98? kama akili ziko sawa jibu ni hapana.

hapa kuna shida,tunaposema mfumo huu umewabeba wengi tunamaanisha kweli,jiulize leo kuna A ngapi zimepatikana kati ya 75 mpaka 80 ?ambazo kwa zamani zilikuwa ni B? na bado hakuna one za 7 pamoja na A kushushwa sana na kutoa wigo mpana sana kwa wengi kujizolea A kirahisi.


2.unaposema mtu mwenye E kafaulu,je amefaulu kweli ama hajafaulu,mtu anapata marks chini ya 30 alafu ili akasome nini baadae.


3.fair ya mfumo haitokani tu na grades,kuna usahishaji na uchakataji matokeo,zamani wanafunzi wakifeli sana ama kwa sababu ya ugumu wa mtihani wana standardize matoke na hapa ndo fair ya zamani ilipokuwa. unasikia paper ilikuwa balaa lakini matokeo yanawashangaza baada ya kuona si mabaya sana.


4.PIA unapoongelea C kuwa ina credit 4 kwa sasa lakini ilikuwa na credit 3 kwa zamani.
piga hivi.

sawa zamani C saba ni two ya 21,

lakini usipotoshe kabisa kusema mwenye C za zamani akipangiwa kwa mfumo wa sasa atapata three ya 28,kumbuka kulikuwa na C za kati ya 50 mpaka 60 mabazo kwa sasa ni B NA POINT ZAKE NI TATU hivyo ingebaki division two ya 21 kama kawaida kati ya marks hizi,

unapopiga mahesabu lazima uangalie pande zote na usijilimit kuwa lazima kila mtu alipate C ya 41 na 50,kuna wengine walipata C za 55 ama 60 ambazo kwa sasa ni B,HAPO UTAKUWA UMENIELEWA. na kwa maana hiyo aliyekuwa na flat C huwezi kusema kirahisi kuwa alistahili three kwa sasa kwa kuwa haijulikani alipata marks kiasi gani.

5.ubovu wa kutumia continuous assessment ambazo zinatolewa mashuleni ndio utaharibu kabisa elimu,nani asiyejua kuwa kila shule itapika marks ili zionekane nzuri hata kama hawakufundisha na kutoa mitihani,


labda kama wangetumia mtihani wa necta form two kama continous assessment hapo sawa kwa kuwa wanafunzi wote nchi nzima watapimwa kwa mtihani uleule na kutakuwa na kigezo sawa cha kuwapima wanafunzi wote kisichokuwa na double standard

,alafu utampimaje wanafunzi kwa vigezo tofauti,mtihani wa mzumbe hauwezi kulingana ugumu na mtihani wa marian,alafu unataka watoto wale watumie marks za mashuleni,

pia mtihani wa mzumbe unaweza kuwa ni wa topiki mbili lakini wa kibaha ukawa ni wa topiki 6,hapa akili za mtu anaye support hili haziko sawa,mimi niliwahi kufanya mitihani migumu ya kiingereza form one marks kubwa niliyopata ni 33 na wakati mwingine wa kwanza darasa zima anapata 10 lakini hawa wanafunzi ukiwaambia wafanye necta wanafumua A za kutosha,sasa hapa wakipewa hizi assessment si umewaua,na form two waliingia wanafunzi watatu top ten kikanda na mimi nikiwemo ambapo hata form two sikuwahi kupata A tofauti na mtihani wa NECTA
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…