HOJA YANGU: Mfumo ulio tumika kwa matokeo mwaka huu CSEE ni mfumo BORA KABISA{BEST EVER}

HOJA YANGU: Mfumo ulio tumika kwa matokeo mwaka huu CSEE ni mfumo BORA KABISA{BEST EVER}

si kweli.

ukweli kabla sijaweka maelezo.

serikali haijawahi kutumia continuous assessment toka nchi ipate uhuru pamoja na kuwa sera ya continous assessment ipo muda mrefu sana,hata mwaka huu haijatumika kabisa
Too generalised!
CA zimewah tumika miaka ya nyuma,though 10%.
kumbuka mabadiliko ya madaraja na grades yalifanyika wiki mbili ama tatu kabla ya mtihani. na kuna shule hazikuwa na hizo marks kabisa,kuna shule watoto hawakuwahi kufundishwa wala kufanya mtihani wa somo moja ama mawili toka form one mpaka form four,marks za continous assessment zilitoka wapi?ama za kutengeneza?
Kama umesoma vema,nimeelezea jinsi CA ilivyo patikana:
15% Form Two National,
15% Mock form 4,
10% Mtihan wa shule form 3.
2.unaposema mtu mwenye E kafaulu,je amefaulu kweli ama hajafaulu,mtu anapata marks chini ya 30 alafu ili akasome nini baadae.
Hakuna mahali nimesema mwenye E kafaulu!
Ili upate cheti[walau div 1V] ni lazma uwe na angalau C moja,au D mbili
5.ubovu wa kutumia continuous assessment ambazo zinatolewa mashuleni ndio utaharibu kabisa elimu,nani asiyejua kuwa kila shule itapika marks ili zionekane nzuri hata kama hawakufundisha na kutoa mitihani,


labda kama wangetumia mtihani wa necta form two kama continous assessment hapo sawa kwa kuwa wanafunzi wote nchi nzima watapimwa kwa mtihani uleule na kutakuwa na kigezo sawa cha kuwapima wanafunzi
Soma post yangu tena,kati ya 40% ya CA,ni 10% ndio hutoka shuleni.
 
Kama serikali haijawah tumia ca walikua wanapeleka wapi? ca hzo mana zilikua zikikazaniwa sana ,Lakina kwa ufupi tuache kutetea makosa kwan matokeo ni mabaya sana kama tunafuata academic ifanye kaz yake,ila kama ushabiki wa kiasisa fresh 15% imeongezeka,Leo mnasema 15% imeongezeka ila taifa ndilo linalopata hasala.
 
Heshima mbele wakuu!
Matokeo ya O level 2013 yametangazwa na kumezuka taharuki juu ya ongezeko la ufaulu kwa over 15% na madaraja mapya ya div 1V ya 46 na div 0 ya 41!!
Karibu tufuatane kwenye hoja hii:

KWANINI NINADHANI MFUMO WA MWAKA HUU NI BORA ZAIDI

Kabla ya mwaka jana,NECTA walikuwa wakifanya yafuatayo:

1: Mwanafunzi alipimwa baada ya miaka minne,by a single paper,at one sitting,kuamua amemudu vipi masomo yake.
Jambo hili lilipelekea baadhi ya wanafunzi,walio fanya vizuri toka form 1 hadi form 4 kutofanya vema sana katika mtihani wa mwisho.
Mathalani,mtu anaweza kupata A somo toka form one hadi form four,lakini akateleza na kupata C NECTA,na inafahamika kwamba mtahiniwa ana uwezo wa C kwenye somo husika,kinyume cha uhalisia!

Hali ipoje sasa?
Kwa kuanzia mwaka jana,ni lazima marks 40% kwenye NECTA zitokane na Continuous Assessment kwa utaratibu ufuatao:
  • Mtihani wa National Form Two unachangia 15%.Mtihani wa MOCK form four unachangia 15%.Mtihani wa shule form Three marks 10%
Then,NECTA Form 4 inachangia 60%.

Utaratibu huu ni bora kuliko wa marks 100% kwa mtihani 1 kwa sababu zifuatazo:

i: Una akisi uwezo halisi wa mwanafunzi toka anaanza hadi kumaliza shule.

ii: Unapunguza udanganyifu,kwani mwanafunzi hapimwi kwa paper moja tu.

iii: Unahimiza juhudi endelevu kwa mwanafunzi,kwani kila kidato kinakuwa na uzito sawa.

2: MGAWANYO WA MADARAJA

Kabla,marks za ufaulu HASA ilikuwa ni C ambayo ilikuwa 41% yenye thamani ya 3 katika division,hivyo mtu akipata C 7 ni 7*3,na hvo ni Two ya 21 pts.

Sasa,Credit imebaki almost ile ile,40%[C],ila thamani yake imepunguzwa hadi 4,hvyo,mtu akipata C 7 ni 7*4,na ni div Three ya 28!!

Hivyo,hoja kuwa div za sasa ni rahisi kupata haina nguvu!!

Twende kwenye madaraja
Hapo awali,kulikuwa na madaraja matano: A,B,C,D na F yenye thamani 1,2,3,4 na 5 kwa mfuatano huo huo.
Interval toka daraja moja hadi jingine ilikuwa 20%,
yaani:
81-100 A,
61-80 B,
41-60 C,
21-40 D,
na
0-20 F.
Hapa kulikuwa na shida,gap ilikuwa kubwa mno,
kwa mfano,mtu akipata 21% na mwingne 40% ilihesabika wote wana D,lakini kimsingi,watu walio tofautiana 20% wamezidiana uwezo sana!!!
Kilichofanyika sasa ni KUPUNGUZA GAP KATI YA MADARAJA KUWA 10%,
Hvyo,sasa madaraja ni kama ifuatavyo:
0-20 F,
20-29 E,
30-39 D,
40-49 C
[credit],
50-59 B,
60-74 B+,
75-100 A.
Thamani za madaraja ni 1,2,3,4,5,6 na 7 kwa A,B+,B,C,D,E na F respectively.
[COLOR=#00ff00][/COLOR][B]Hii ni bora kuliko mwanzo,kwani,sasa utofauti wa madaraja una reflect uwezo wa mtu[/B].

[B]MGAWANYO WA DIVISION[/B]
1: Div 1 haijabadilika [pts 7-17],ambayo ni minimum B+ 4 na B 3.
2: Div Two ni pts 18-22[kama sijakosea] ambayo ni min B 6 na C moja.
3: Div 3 ni pts 23-31,ambayo ni min C 4 na D 3.

4: [B]DIVISION 1V[/B] ni min pts 47,ambapo [B]Lazima uwe na angalau D mbili au C moja[/B],Kinyume na hapo ni FAIL[DIV 0]

5: [B]DIVISION 0 ni pts zozote kati ya 41 hadi 47 ambapo mtu hana ANGALAU D MBILI AU C moja[/B], na pts 48-49[ambapo hapa mtu hawez kuwa na D2 au C1]

[B]CONCLUSION[/B]:
Kama umefuatana nami vema,hakuna mteremko ulio wekwa,bali thamani ya elimu yetu imeongezwa!
Haikuwa fair hata kidogo kuamua uwezo wa mwanafunzi at one sitting!
Nimeupenda mfumo mpya.
Haya ni mawazo yangu,
KARIBUNI KWA MJADALA.[/QUOTE]

Mimi nashauri wapange upya madaraja especially kutoka daraja C hadi daraja F na waliondoe daraja E sababu daraja E kuna wakati linapingana na sheria ya kufaulu kama ilivyosemwa kuwa ufaulu wa mwisho ni angalau upate C moja au D mbili kama ilivyojionyesha kwa watahiniwa hawa.


[TABLE]
[TR]
[TD="width: 6%"][FONT=Arial][SIZE=1]S1697/0068[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 4%"] [FONT=Arial][SIZE=1]F[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 6%"] [FONT=Arial][SIZE=1] 46[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 4%"] [FONT=Arial][SIZE=1]IV[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 58%"] [FONT=Arial][SIZE=1]CIV - 'F' HIST - 'F' GEO - 'F' KISW - 'C' ENGL - 'F' BIO - 'F' B/MATH - 'F' [/SIZE][/FONT]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE]
[TR]
[TD="width: 6%"][FONT=Arial][SIZE=1]S2063/0042[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 4%"] [FONT=Arial][SIZE=1]F[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 6%"] [FONT=Arial][SIZE=1] 42[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 4%"] [FONT=Arial][SIZE=1]0[/SIZE][/FONT]
[/TD]
[TD="width: 58%"] [FONT=Arial][SIZE=1]CIV - 'E' HIST - 'F' GEO - 'E' KISW - 'D' ENGL - 'E' PHY - 'E' CHEM - 'F' BIO - 'E' B/MATH - 'F' [/SIZE][/FONT]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Hii inamaanisha daraja E linakuwa na kazi pale tu mtahiniwa akipata angalau D mbili au C moja la sivyo daraja E linakuwa halina kazi ,sheria ndo inatumika! sasa daraja E la nini?
 
inamaana mtu akipata E,kwenye cheti chake anaandikiwa pass au fail?
 
Hamna kitu hapo,hizo zimekaa kisiasa tu!2015 hiyoooo
kufaulu sasa ni rahisi ukilinganisha na mwanzo,hicho ulichoandika hakileti maana,la msingi hapo points zimeshushwa ili kujaza mashule yao ya advance yaliyokuwa yanaelekea kuwa magofu!
Sasa hivi kupata B,A ni rahisi sana kuliko mwanzo A =81-100 na hii leo A=75-100 alafu unasema elimu imeboreshwa!
Labda unisaidie kunijuza unatumia nini kufikiri?isiwe ndo wale wale wabunge wa Dar
 
Zilikuwa hazitumik ndomana NECTA wakatangaza kuwa wanarudisha mtinda wa countnue assesmnt kama zaman maana ulisimamishwa wakidai kuwa xcl zingne walikuwa wakijaza matokeo ya huongo kwenje jarida
hata sasa watajaziwa tu . hilo wala haliweziisha
 
Swala lipo kwenye udanganyifu wa CA hiki ndio chanzo cha kulalamikiwa kwa matokeo hasa shule za private hawez kupeleka CA ambayo kwa mwanafunz ili hali wapo kikaz
 
Hamna kitu hapo,hizo zimekaa kisiasa tu!
Well,ni siasa,na kila kitu siasa inahusika.Si lazima uamuzi wa kisiasa uwe mbovu.

2015 hiyoooo
kufaulu sasa ni rahisi ukilinganisha na mwanzo
Ingekuwa rahisi hvyo,div 1V na 0 zisingekuwa 70%,ambapo kimsingi wote wamefeli,au unadhan div 4 ni kufaulu kimsingi?
hicho ulichoandika hakileti maana,la msingi hapo points zimeshushwa ili kujaza mashule yao ya advance yaliyokuwa yanaelekea kuwa magofu!
Sasa hivi kupata B,A ni rahisi sana kuliko mwanzo A =81-100 na hii leo A=75-100 alafu unasema elimu imeboreshwa!
A hazijaongezeka kivile,
ukiondoa A,hakuna mabadiliko yoyote ya msingi kwa madaraja ya chni,soma vizuri bandiko langu.
Labda unisaidie kunijuza unatumia nini kufikiri?isiwe ndo wale wale wabunge wa Dar
Natumia makalio kufikiri,umefurahi eeh?
 
Na je?,
Wale wa kwenda Grade A (Chuo cha Ualimu) ni kuanzia point ngapi hadi ngapi?...... AU

Watatumia vigezo gani ktk hili?.......

NAOMBA MSAADA JAMANI...............
 
Well,ni siasa,na kila kitu siasa inahusika.Si lazima uamuzi wa kisiasa uwe mbovu.


Ingekuwa rahisi hvyo,div 1V na 0 zisingekuwa 70%,ambapo kimsingi wote wamefeli,au unadhan div 4 ni kufaulu kimsingi?

A hazijaongezeka kivile,
ukiondoa A,hakuna mabadiliko yoyote ya msingi kwa madaraja ya chni,soma vizuri bandiko langu.

Natumia makalio kufikiri,umefurahi eeh?

B=50-74 wakati za mwanzo zilikuwa 61-80!
C=40-49 wakati mwanzo ilikuwa 41-60 bado huoni mporomoko wa elimu?
Hilo la wanafunzi kufeli we unashangaa?kama umepanda miwa unataka uvune mchele?tumeona darasa la saba wanaenda sekondari hawajui kusoma wala kuandika na ndio hawa waliomaliza leo ulitegemea nini?duh..labda nikuulize mwenzangu upo sayari gani?isiwe ukawa upo pluto na akili yako ishaganda tayari
 
B=50-74 wakati za mwanzo zilikuwa 61-80!
Bila shaka,hata ukipewa paper uibie,unaweza fail wewe!
Haya rudi kwenye thread usome,sitaki kukutafunia hapa.
C=40-49 wakati mwanzo ilikuwa 41-60
Rud kwenye thread ukasome thamani ya C na B plain katika divisions.
duh..labda nikuulize mwenzangu upo sayari gani?isiwe ukawa upo pluto na akili yako ishaganda tayari
Inawezekana eeh!
Ushauri wa bure:Raise hoja ambazo sijajadili,sio unajichanganya kwa mambo niliyo chambua tayari.
Halafu unapo taka kutukana,atleast hakikisha you are better-off kuliko huyo unaye dhani ni kilaza!
Goodmorning!
 
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:

  1. Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012. Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.

Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.

[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]Kundi
[/TD]
[TD]Gredi
[/TD]
[TD]Pointi
[/TD]
[TD]Idadi ya Pointi
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 1
[/TD]
[TD]A
[/TD]
[TD]75 - 100
[/TD]
[TD]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2[/TD]
[TD]B+
[/TD]
[TD]60 - 74
[/TD]
[TD]2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3[/TD]
[TD]B[/TD]
[TD]50 - 59
[/TD]
[TD]3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4[/TD]
[TD]C[/TD]
[TD]40 - 49
[/TD]
[TD]4[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5[/TD]
[TD]D[/TD]
[TD]30 - 39
[/TD]
[TD]5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6[/TD]
[TD]E[/TD]
[TD]20 - 29
[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7[/TD]
[TD]F[/TD]
[TD]0 -19
[/TD]
[TD]7[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika.Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili (12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.


  1. Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.


  1. Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katika Daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.

Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013

[TABLE="width: 735"]
[TR]
[TD]Daraja
[/TD]
[TD] Pointi
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]I[/TD]
[TD]7 – 17
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]II[/TD]
[TD]18 – 24
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]III[/TD]
[TD]25 – 31
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]IV[/TD]
[TD]Ufaulu katika somo moja kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C au Ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili katika Gredi D
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0[/TD]
[TD]Alama chini ya D mbili
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

1 Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli.

2 Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.


Imetolewa Na:


KAIMU KATIBU MTENDAJI
 
Hamna kitu hapo hiyo mikakati ya CCM kupumbaza watu ili waendelee kutawala mambumbu kwa kuyapa bora elimu na si elimu bora
 
Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na NECTA E ni Fail. Kwa maelezo zaidi soma thread inayoeleza ufafanuzi kwa wadau wa elimu kuhusu matokeo ya Kidato cha Nne 2013
inamaana mtu akipata E,kwenye cheti chake anaandikiwa pass au fail?
 
Bila shaka,hata ukipewa paper uibie,unaweza fail wewe!
Haya rudi kwenye thread usome,sitaki kukutafunia hapa.

Rud kwenye thread ukasome thamani ya C na B plain katika divisions.
Inawezekana eeh!
Ushauri wa bure:Raise hoja ambazo sijajadili,sio unajichanganya kwa mambo niliyo chambua tayari.
Halafu unapo taka kutukana,atleast hakikisha you are better-off kuliko huyo unaye dhani ni kilaza!
Goodmorning!

mimi nimezicombine pamoja hizo B...
Sasa kma alama E na F zote zina maana 1 yani ni fail,sasa E ina kazi gani hapo?acheni utumwa wa fikra nyinyi,kama wengine wana makundi 9 mpk 12 kwahyo na nyinyi ndo mnataka muyaongeze?ni upumbavu usiovumilika,nyinyi dawa yenu ni 2015 kupiga chini tu.
Kwanini mama Ndalichako alitoka hapo?sababu ni upumbavu wa kuchanganya suala nyeti la elimu na siasa zenu za majitaka
 
wewe unasema kuhusu CA je kwa Private candidate (PC) CA gani wametumia? mbona na wenyewe mfumo ni huu mimi sikubariani na mfumo huu mpya.
 
Hilo la CA sidhani kama ni la kweli maana kuna shule nyingi sana hasa za private hazikufanya joint mock examinations. Hata baadhi ya wanafunzi ktk shule za serikali hawakufanya mitihani ya mock
 
mimi nimezicombine pamoja hizo B...
Wewe ndio ulikuwa unamwita mtoa mada akili mgando na ma.sa.buri thinker?
Sasa uta combine vipi B+ yenye thamani ya 2 na B plain yenye thamani ya 3?
Kama hujui kitu,kubali kueleweshwa,kuliko kujivua nguo hadharani!
Sasa kma alama E na F zote zina maana 1 yani ni fail,sasa E ina kazi gani hapo?
UDSM,kwa mfano,chini ya C ni fail,lakini zipo mbili,D na E,kwa hyo mwenye D ana afadhali,na ni rahs kufikisha GPA ya 2.0 inayo mruhusu ku SUP au ku carry.
acheni utumwa wa fikra nyinyi,kama wengine wana makundi 9 mpk 12 kwahyo na nyinyi ndo mnataka muyaongeze?ni upumbavu usiovumilika,nyinyi dawa yenu ni 2015 kupiga chini tu.
Kwanini mama Ndalichako alitoka hapo?sababu ni upumbavu wa kuchanganya suala nyeti la elimu na siasa zenu za majitaka
Ujinga na utumwa wa fikra ni kukataa mabadiliko!
 
Wewe ndio ulikuwa unamwita mtoa mada akili mgando na ma.sa.buri thinker?
Sasa uta combine vipi B+ yenye thamani ya 2 na B plain yenye thamani ya 3?
Kama hujui kitu,kubali kueleweshwa,kuliko kujivua nguo hadharani!

UDSM,kwa mfano,chini ya C ni fail,lakini zipo mbili,D na E,kwa hyo mwenye D ana afadhali,na ni rahs kufikisha GPA ya 2.0 inayo mruhusu ku SUP au ku carry.

Ujinga na utumwa wa fikra ni kukataa mabadiliko!

acha kukurupuka wewe mbwe.ha,sasa UDSM na SEKONDARI sawa?
Kule vyuo vikuu wanatumia C.A na final na pia kuna SUPP,CARRY DISCO sasa na huku sekondary yapo hayo?
Sasa hizo B+ na B zote si B tu na zina hadhi ya credit hata kama point tofauti,aliyepata B3 na B+3 kwnye comb wote wanaenda advance!unaelewa hoja yangu au muwasho tu?
Huu mfumo una madhaifu mengi,ikiwemo kurahisisha ufaulu wa wanafunzi kwa kupunguza grade za ufaulu,
mdau hapo kaongezea kama wanatumia C.A za 40% na final 60% je,hawa waliofanya mitihani hii kama PC hizo continuing assesment wanazitolea wapi?na mfumo ni huo huo mmoja unaotumika!
BRN unajua maana yake wewe?,hebu tulia kama hujui kitu
 
Back
Top Bottom