#COVID19 Hoja za baadhi ya Watanzania kuhusu kukataa chanjo bado ni dhaifu sana

#COVID19 Hoja za baadhi ya Watanzania kuhusu kukataa chanjo bado ni dhaifu sana

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Watanzania hawaishiwi hoja kwa kweli.

ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ambayo serikali imejitoa kabisa kwamba litakalokupata wao hawawajibiki kwa lolote?

Watanzania wamesahau kwamba hata ukienda hospitali una haki ya kukataa kutibiwa, una haki ya kukataa sawa, una haki ya kumkataa daktari usiyemtaka asikutibu.

Endapo ukikubali kutibiwa kwa ridhaa yako na katika tiba hiyo ukapata madhara basi hakuna daktari atakayewajibika eti ahukumiwe kwa jambo hilo.

Hata ukienda kufanya upasuaji lazima ukubali kusaini,usaini ukaenda ukafa kwenye upasuaji ujue hakuna utakayemlaumu kwa sababu ulikubali mwemyewe.

Hivyo sio kwenye korona tu hata kwenye tiba zingine wanaohusika na jambo hilo wanajivua endapo ukikubali kufanyiwa jambo hilo litakalo kupata lakwako wewe.

Hivyo serikali ipo sahihi kujitoa lwenye lawama kwa sababu mtu atachoma chanjo akiumwa kichwa tu atataka aiwajibishe serikali kwamba chanjo inamdhuru,katika hili serikali imefanya vyema.

ETI katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ukishachanja unaambiwa uendelee kuchukua tahadhari?

Watanzania hakuna chanjo utakayochukua alafu ukaambiwa ukae katika mazingira hatarishi ati kwa kuwa umepata chanjo, hakuna chanjo hiyo.

Angalia tu ukidungwa sindano ya kujikinga na tetenasi haina maana kwamba ujiachie tu wewe ujikate ovyo na kujiachia kwenye mazingira hatarishi.

Ukidungwa chanjo ya yellow fever haina maana eti ndio utaambiwa ukae tu kwenye mbu na mazingira hatarishi,lazima iwe ni muhimu kujiepusha na mazingira hayo hatarishi.

Hivyo hata chanjo ya korona ukidungwa haina maana ujiachie tu,lazima uendelee kujikinga.

Maana ya chanjo sio kutafuta matatizo yalipo,maana ya chanjo ni kukukinga endapo kwa bahati mbaya umepata ugonjwa,sasa wewe utafute kwa makusudi.

Ukicheza karate unatakiwa uepuke ugomvi,haina maana kwamba unajua kupigana ndo uchokoze watu.

Eti baadhi husema sijui ukichanjwa utapata madhara kadha wa kadhaa,ni kweli unaweza kupata madhara kdha wa kadha lakini swali la msingi ni je chanjo hiii pekee tu ya corona?

Jawabu ni kuwa chanjo zote zina madhara fulani yanaweza kutokea kwa mtu.

Mfano:
Kuna chanjo watoto wachanga wakichomwa wanapata homa sana lakini baadae wanatulia maisha yanaendelea chanjo hizi hazipigiwi kelele.

Unaweza kuchoma chanjo ukapata aleji kinga za mwili zikaanza kushambulia seli mwenzake za mwili ukaanza kupata machovu na matatizo mengine ambayo yanaweza kupotea baada ya muda fulani.

Zipo kinga au chanjo mfano kinga ya homa ya manjano tafuta side effects zake utaona miongoni mwa matatizo ambayo unaweza kupitia ni kama vilee.

Maumivu ya joints,maumivu ya misuli, kupata homa, mapele, kichwa kuuma n.k

Kwa hiyo kama chanjo ya corona itakuwa inaambatana na matatizo basi tukubaliane hakuna chanjo iliyosalimika.

Lakini pia naomba kuwauliza wanaosema hii chanjo baada ya muda ina madhara.

Je, wamejuaje kama ina madhara wakati hapo hapo wanasema haijafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu usalama na madhara yake?

Na je hayo madhara yataonekana baada ya muda gani ukishachoma chanjo?

Swali la mwisho ambalo naomba niliulize ni kwamba tokea tuanze kudungwa hizi chanjo utoto wetu ambazo tisema tunajaribiwa mpaka hivi leo hii tumepata madhara gani kwa watu wote ambayo tutasema kisayansi yametokana na chanjo hizo za utotoni?

NB: Siko hapa kutetea chanjo, bali niko hapa kuvunja hoja dhaifu zinazotumika na baadhi ya watu kuwatisha wengine.

Nakubaliana na mambo ambayo kisayansi yana hoja zenye nguvu zinazoingia akilini na sio kuokota kila hoja tu na kuisema ili tuendee kulaumu.
 
Wanaotaka kuchanja nao wawashawishi hao watu kwa hoja zao..
Uzuri wa wanaotaka kuchanjwa wanatoa hoja za kisayansi lakini, ambao hawataki, ukimuuliza hilo unalosema una uhakika nalo anakwambia "nimesikia watu wanasema" kuna nini hapo?mala chanjo hizi kwanini zimetumia muda mfupi kupatikana!!hiyo nayo kwa dunia ya sasa ni hoja?
 
Nasikia chanjo iliua kakakuona wakati wa majaribio, sasa unajua tena sisi na kakakuona...akitokea huwa tunamletea hadi maji🤣🤸🐒
 
👏👏👏 Hongera sana kwa hoja zako. AstraZeneca isharekebishwa kugandisha damu?
Nimekuja hapa kuvunja hoja dhaifu zinazotumiwa kupinga chanjo.

Na wala sikuja hapa kutetea kila kinachohusu chanjo...
 
Wengine wameenda mbali wakasema takwimu zinaonesha watu waliopata chanjo katika nchi za magharibi bado wanakufa kwa corona

Jamii hii ya watu ni ya kuionea tu huruma kazi ya chanjo ni kudibiti ugonjwa ambao bado haujaingia mwilini. Ugonjwa ukiishaingia mwilini halafu ikafata chanjo hapo utakua kwenye zone ya hatari
 
Uzuri wa wanaotaka kuchanjwa wanatoa hoja za kisayansi lakini, ambao hawataki, ukimuuliza hilo unalosema una uhakika nalo anakwambia "nimesikia watu wanasema" kuna nini hapo?mala chanjo hizi kwanini zimetumia muda mfupi kupatikana!!hiyo nayo kwa dunia ya sasa ni hoja?
Gwajima si aliwaaminisha waumini wake kua corona imetokana na waves za 5G technology

Kama alikua muongo kwa hoja hiyo kwanini waumini wasimuone muongo kwa hoja hii ya chanjo?

Afu anatuondolea focus ana tusahaulisha kimakusudi tusahau ile video yake
 
Kabisa mkuu
 
Mtu anayemsikiliza na kumwamini Gwajima ujue lazima atakuwa msukule wa kanisa lake au muumini wa imani ya yote yaliyosemwa na mwendazake.
 
Sasa si ukachanje kwani shida iko wapi mtoa mada,mbona hv vibandiko vimekuwa vingi sana wiki hii? Ww ukijiskia kuchanja nenda hujakatazwa.....hamjiamini au!!
 
mala chanjo hizi kwanini zimetumia muda mfupi kupatikana
Muda mfupi huu huu wao wanasema kuna madhara yanapatikana.

Sasa wamewezaje kujua madhara hayo kwa muda mfupi huo huo ?

Wamefanya tafiti gani wakajiridhisha kwamba kwa muda mfupi huu haya ndio madhara yake badala yake wasikae kimya wasubiri upite muda mrefu waje na mdhara ambayo yishafanyiwa utafiti wa muda mrefu.
 
Sasa si ukachanje kwani shida iko wapi mtoa mada,mbona hv vibandiko vimekuwa vingi sana wiki hii? Ww ukijiskia kuchanja nenda hujakatazwa.....hamjiamini au!!
Hampendi kusikia tunajibu hoja dhaifu ambazo hazina msingi.

Acheni hoja zisizo na maaana kama hizi tuzijibu ili kama kupotosha basi watu wapotoshe kwa hoja za msingi sio hoja za kitaani kitaani
 
Uzuri wa wanaotaka kuchanjwa wanatoa hoja za kisayansi lakini, ambao hawataki, ukimuuliza hilo unalosema una uhakika nalo anakwambia "nimesikia watu wanasema" kuna nini hapo?mala chanjo hizi kwanini zimetumia muda mfupi kupatikana!!hiyo nayo kwa dunia ya sasa ni hoja?
Wanaijua sayansi au ndo porojo za kitaa tu.
 
Kuhusu hili swala la chanjo kila mtu asimamie anachokiamini isiwe ajenda sana,maana kumeibuka na kundi la watu kujidai wao ni wataalamu wa kuelimisha watu kuhusu swala la chanjo wakati kwa namna moja au nyingine hawana utalaamu wowote wanaishi kwa kuzani,kama ina madhara yataonekana kama haina it's fine tusileteane ngonjera nyingi!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom