Unanituhumu kwa kutoa mifano isiyo halisi, sasa wewe huu mfano wa ujenzi wa barabara sijui umekujaje hapa
Umekuja hapa kwa sababu ni mfano halisi.
Chanjo ni tofauti na huo mfano wako wa barabara
Hiyo ni mifano hai kwa sababu
Kwanza barabara zipo halisi na ajali zipo halisi zinatokea,fuatilia takwimu za ajali za barabarani utaona kwamba hizo ajali zinahusisha watu ambao wapo na zinahusisha barabara ambazo zipo na zinajengwa na serikali.
Hivyo mifano yangu ni halisi kwa sababu vitu vyote vipo vinatokea.
Wewe mifano uliyotoaa sio halisi kwa sababu hakuna chanjo mabayo ilokuja watu wakachomwa wakafa kama unavyodai.
Na huko ndio kutoa mifano ambayo haijawahi kutokea(mifano feki a.k.a mifano ambayo sio halisi)
Kwa hiyo maana ya uhalisia hapa ni kwamba iww kweli kitu kipo na kimewahi kutokea.
sio wote wataitumia kwa matumizi sawa hiyo barabara lakini chanjo nyote mnaochanjwa ni sawa nadhani kwa kila kitu
Kila anayepata ajali barabarani lazima awe anatumia barabara kwa lengo moja tu la kutoka sehemu moja kwenda nyingine ama kwa lugha nyepesi kusafiri.
Sio rahisi wewe kutuambia kwamba wanaopata ajali wanatumia barabara kwa matumizi tofauti,sio kweli.
Wanaopata ajali wote wanatumia barabara kwa lengo moja tu la kutoka sehemu moja kwenda nyingine,labda utuambie kila mtu analifikia lengo hilo kwa njia tofauti.
Na kitu kuwa na njia tofauti haina maana na lengo tofauti,unaweza kuwa na njia ishirini lakini lengo ni moja tu.
Hivyo point hii pia naomba kuiwakilisha kwako kwamba watumiaji wa barabara wanaopata ajali wote hutumia kwa lengo moja tu la kutoka sehemu moja kwenda ingine(au kusafiri)
chanjo nyote mnaochanjwa ni sawa nadhani kwa kila kitu
Sio kweli.
Kuna watu miili yao wana allergic reaction(aleji) wakiitumia baadhi ya dawa,na wengine hawana.
Kwa mfano huo tu watumiaji wa chanjo hawako sawa kwa kila kitu.
Wasiwasi wa sisi wananchi hadi kutoiamini serikali kwenye hili suala ni hiyo misimamo yake inayotia mashaka
Tatizo sio serikali bali tatizo ni nyie wananchi mumetiwa mashaka.
Walikua hawazitaki izo chanjo kabisa na kashfa kibao tena mpaka viongozi wa kwenye kada ya afya,
Hii sio hoja ya kukataa chanjo kwa sababu mfano tu wakati wa magufuli watu walikuwa wanasifia sana serikali bila kukosoa.
Lakini watu wale wale baadhi yao sasa hivi wanakosoa serikali.
Kama kweli wanayokosoa ni ya kweli tunayachukua,hatuwezi kukataa wanayoyakosoa kwa kigezo cha kuwa eti mwanzo walisema tofauti.
Hivyo kipimo sio kigeugeu bali kipimo ni nini anasema huyo mtu.wewe mwache ageuke geuke awe na ndimi mbili lakini hoja ya msingi tuangalie anasema nini.
leo hii wanaleta chanjo na kusema usign kabisaa kua ukipata side effects wao hawahusiki
Nakuuliza tena ni matibabu gani katika afya ambayo serikali ilisema kwamba itahusika na side effects ambazo mgonjwa atazipata baada ya kutibiwa ?
Lete ushahidi wa hayo matibabu,pengine ukawa unakataa jina tu lakini maana ni ile ile.
Yote ni taratibu za kimatibabu.
We ushawahi kwenda hospitali ukatibiwa na kusain form kama ile??
Wanaoenda kufanyiwa upasuaji lazima wajaze fomu ya kuhifadhi kumbukumbu ya ridhaa zao kwamba wamekubali wenyewe.
Jambo hili ni maarufu sana hata kama sijawahi kufanya upasuaji lakini lipo wazi.
Au wale wanaofanyiwa amputation(kukatwa viungo) lazima watoe ridhaa wenyewe kwanza then ndo wafanyiwe.