#COVID19 Hoja za baadhi ya Watanzania kuhusu kukataa chanjo bado ni dhaifu sana

oja za wezio unaita dhaifu ila atuchanji
 
Mwaka 1987 nilichanjwa chanjo ya typhoid nilipata homa kali mno.Bro umeongea point ahsante
 
Mkuu umeeleza mengi sana lakini 90% umetoa majibu tofauti kabisaa.

Umesema mfano wako wa barabara ni halisi, kuna mahali ulishaona watu wanaikataa barabara kwa namna yoyote ile?? Maana ya yangu ya mfano halisi imejikita hapo.
Na kusema hujawahi kusikia watu wamechoma chanjo wakapata madhara ilhali kuna baadhi ya chanjo zimetumika huko nchi za ulimwengu wa kwanza na zimeleta madhara, hapo inaonekana si mfuatiliaji wa habari tena ni hii hii johnson & johnson inayotuhumiwa.
(Sina uhakika juu ya madhara yake ila imetuhumiwa sana).

Kitu kingine hapo labda hukuelewa ila tu umetoa majibu ni kuhusu mtu kwenda hospitali na kupewa tahadhari juu ya dawa anazo/atakazotumia mgonjwa. Kama hukuelewa vizuri ni kua, ukienda hospitali sio serikali inayokutibu pale, sio inayokulipia gharama, sio iliyokuhamasisha ukatibiwe ni wewe na magonjwa yako wala sio serikali inayoidhinisha upewe dawa gani bali ni daktari uliyemkuta hapo.
Maana yangu ni kwamba serikali ndio inaleta hiyo chanjo, hatulipii chochote, na tunahamasishwa tuchanje huoni hapo kua ili sisi kua na imani na hiyo chanjo ni vizuri kuhakikishiwa usalama wetu. Teknolojia imekua mkuu kureason ni muhimu saivi sio kama zamani kwamba kila kitu unaamini chap tu, wacha wenye wasiwasi tuendelee kusubiri.

NB: Sijakujibu mengine kama hilo la operation kwasababu liko wazi operation na chanjo havifanani ila ni vile tu mnakaza ubongo.
 
umetema nondo I salute you
 
Dawa za ukimwi mnalipishwa shingapi?

Chanjo ya johnson and jonhson hadi CDC na FDA wametoa recommendation kua itumike rasmi marekani kuliko chanjo zingine.

Nini maoni yako?
 
Chanjo gani hiyo ukiweka Taa inawaka [emoji81][emoji81]
Propaganda.

Hakuna ushahidi wowote unaoonesha kwamba ile video inahusiana na chanjo ya corona.


Watanzania tunapenda sana kuletewa picha alafu habari tukamalizia wenyewe kwa mujibu wa tunavyoona inafaa.
 
Dawa za ukimwi mnalipishwa shingapi?

Chanjo ya johnson and jonhson hadi CDC na FDA wametoa recommendation kua itumike rasmi marekani kuliko chanjo zingine.

Nini maoni yako?
Mkuu naomba unitag akikupa maoni yake.
 
We ushawahi kwenda hospitali ukatibiwa na kusain form kama ile??
Jambo hili ni maarufu sana hata kama sijawahi kufanya upasuaji lakini lipo wazi kwamba unapewa fomu kabla ya tiba


Au wale wanaofanyiwa amputation(kukatwa viungo) lazima watoe ridhaa wenyewe kwanza then ndo wafanyiwe
 
Dawa za ukimwi mnalipishwa shingapi?

Chanjo ya johnson and jonhson hadi CDC na FDA wametoa recommendation kua itumike rasmi marekani kuliko chanjo zingine.

Nini maoni yako?
Dawa ya za ukimwi-chanjo ya corona
Mkuu hivyo vitu waona vina ufanano??
Hiyo dawa ya ukimwi atapata mwenye ukimwi hii ya corona haijalishi unayo au huna inashauriwa uipate. Hivi ni kwanini mnafananisha dawa na chanjo, upasuaji na chanjo. Mnasema wanaopinga chanjo hawana hoja wakati nyie hoja yenu kuu ni hiyo ya ufananisho tu, sijui kwani hiki ni hiki, kile ni hiki aisee nyie watu .

Sijui kama mnaelewa ninachomaanisha. Ni hivi serikali imesema chanjo ni hiari kwasababu wanajua fika kuna watu wasioafiki, sio wajinga kuweka hivo. Kuna chanjo ambazo ni za lazima utake usitake utachanjwa tu. Swali ni jee kwanini hii, kwanini serikali haitaki ihusike na side effects na fomu unajaza kabisaa kuthibitisha hilo. ??

Je marekani huko unakosema imeidhinishwa nako kuna kusign na kujicommit kama huku??
Ni chanjo ipi iliyokuja kwa mfumo huu ilhali hili ni gonjwa zito.??

Toeni majibu ya kueleweka sio ufananisho. Tuelewesheni kama hujui sema sijui sio ajabu kutojua.
 
Jambo hili ni maarufu sana hata kama sijawahi kufanya upasuaji lakini lipo wazi kwamba unapewa fomu kabla ya tiba


Au wale wanaofanyiwa amputation(kukatwa viungo) lazima watoe ridhaa wenyewe kwanza then ndo wafanyiwe
Upasuaji upasuaji upasuaji
Mkuu kwani Samia ile tar 28/7/2021, uliona kuna upasuaji unafanyika pale??
Hivi kwanini mnafananisha chanjo na upasuaji?? Upasuaji mara nyingi unakua huna option ww kama mgonjwa, utaacha kufanya upasuaji ilhali unafia kitandani??

Em leteni hoja za maana basi, toa hoja sio ufananisho hiki ni kile, kile ni hiki.
Ukitoa ufafanuzi wa kidaktari itapendeza zaidi lakini bra bra sio hoja. Sio wewe tu wengi hapa wamekazana kutajataja upasuaji.
Jamani chanjo na upasuaji ni tofauti labda useme tulipopata chanjo flani flani tulisainishwa na serikali ikasema hivi na vile, tulipopata chanjo hii ikawa hivi na vile.
Sasa nyie mnafananisha upasuaji wa mgonjwa mmoja na chanjo ya nchi nzima namna gani nyie.
 
Wanaokataa chanjo hawana hoja ni mbummbu flani hivi, nnasikitika kusea kuwa kanda ya ziwa mitikio wa kuchoma chanjo nidogo sana
 
Jambo hili ni maarufu sana hata kama sijawahi kufanya upasuaji lakini lipo wazi kwamba unapewa fomu kabla ya tiba


Au wale wanaofanyiwa amputation(kukatwa viungo) lazima watoe ridhaa wenyewe kwanza then ndo wafanyiwe
Na kwenye hicho ulichokijibu sijaongelea kuhusu upasuaji ila umelazimisha kujibia kupitia upasuaji. Nimeuliza tiba nyingine na sio upasuaji mfano malaria, labda kupata zile neti za bure, ama typhoid nk nk, swali langu lilijikita huko.
 
Chanjo ya johnson and jonhson hadi CDC na FDA wametoa recommendation kua itumike rasmi marekani kuliko chanjo zingine.
Kuthibitishwa kwake hakufanyo watu wasiwe na mashaka mkuu.

Halafu unajua nyie watu wa chanjo mmekaa kukejeli na sio kutoa hizo hoja zenu.
Bado nafatilia kupitia vipindi mbali mbali wanaelekeza vizuri na kwa weledi ila humu naona wote sawa tu , hakuna hoja mnazodai mnazo zaidi ya mifananisho.
 
Kawaida hiyo jambo lolote linalofanywa kwa hiyari ya mtu mwenyewe lazima kuwepo na notes of responsibility mfano mara kibao tunakkutana na parking ipo mahali fulani lakini tunakutana na warning note ya parking fo
Ni sawa na mtu akupe kitu usichojua uhatari wake na ajitoe endapo litakupata baya lolote basi usimhusishe.

Ujinga wa watu upo hapo kutokujua kwakwe haimaaishi hiyo chanjo haifai, serekali wanajua kabisa hawa wasiojua ndiyo watakaoleta usumbufu kwasababu ya umbumbu wao wakipatwa na complication zozote hata ambazo hazihusiani na chanjo watataka kufidiwa.

Ndiyo maana kuna maeneo ya parking ya magari unakuta wameandika park on your own risk
 
Bila shaka wewe ulikimbia shule darasa la nne.
 
Ujinga wa watu upo hapo kutokujua kwakwe haimaaishi hiyo chanjo haifai,
Una hoja nzuri ila huku mwisho naona umetindinganya mambo. Eti kutokujua kwangu hakumaanishi hiyo chanjo haifai namna gani wewe, sasa hizo ngonjera za kuhamasisha watu wakachanje kwa kuwaambia ni salama zinatoka wapi kama sio muhimu kujua uhatari wake.

Kitu kingine kinachoonesha baadhi yenu watu wa chanjo (ukiwemo wewe) ni weupe kichwani ni kuamini kua mtu asietaka chanjo ni mjinga😂😂.

Yani dunia hii unategemea watu wawe upande wa unachokiamini au upande wa wengi kwa 100%. Mkuu em acheni tabia za kuita wenzenu wenzenu wajinga ilhali hata nyie hamna hoja zaidi ya blah blah tena sio za kidaktari ni zile za wanasiasa wa tz kina ndugai 😂.
 
Imani ina nguvu kuliko science, na ndio inatangulia before science. Hakuna mwanasayans anayefanya kitu bila kukiamini kwanza. Sisemi msichanje au mkachanje hio ni hiari ya mtu kulingana na vile aonavyo moyoni mwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…