Wanaokubali chanjo wote sio kwasababu ya uhalali na usahihi wa chanjo bali kwa kupingana na mwenda zake(hawakubali lakn ndo ukweli). Wanaokataa ni vile tu mindset zao ni kuwa mzungu sio mtu wakutoa vitu kiholela nimjanja sana anamingo yake nyuma ya chanjo.Una hoja nzuri ila huku mwisho naona umetindinganya mambo. Eti kutokujua kwangu hakumaanishi hiyo chanjo haifai namna gani wewe, sasa hizo ngonjera za kuhamasisha watu wakachanje kwa kuwaambia ni salama zinatoka wapi kama sio muhimu kujua uhatari wake.
Kitu kingine kinachoonesha baadhi yenu watu wa chanjo (ukiwemo wewe) ni weupe kichwani ni kuamini kua mtu asietaka chanjo ni mjinga😂😂.
Yani dunia hii unategemea watu wawe upande wa unachokiamini au upande wa wengi kwa 100%. Mkuu em acheni tabia za kuita wenzenu wenzenu wajinga ilhali hata nyie hamna hoja zaidi ya blah blah tena sio za kidaktari ni zile za wanasiasa wa tz kina ndugai 😂.
kifupi hi hivi! Chanjo ni HIARI, wanaotaka kuchanja wakachanje na vilevile ni sahihi kuwahimiza wengine wakachanje.Wasiotaka kuchanjwa sio sahihi kutumia hoja tata kuwaogopesha wenzao ambao wametumia hiari yao kwenda kuchanjwa.
😆😆😆Gwajima si aliwaaminisha waumini wake kua corona imetokana na waves za 5G technology
Kama alikua muongo kwa hoja hiyo kwanini waumini wasimuone muongo kwa hoja hii ya chanjo?
Afu anatuondolea focus ana tusahaulisha kimakusudi tusahau ile video yake
Hapo ndo tatizo lilipo anza baada ya serikali kuonyesha undumilakuwili wa hali ya juu sana.Kwa nini watie hofu uhuru wa watu wengine katika jambo ambo serikali imesema ni salama ?
Hoja dhaifu umezipinga vizuri sana naomba nisaidie na hoja imara na zenye nguvu za kupinga chanjoNimekuja hapa kuvunja hoja dhaifu zinazotumiwa kupinga chanjo.
Na wala sikuja hapa kutetea kila kinachohusu chanjo...
Hahaha wale wanaendeshwa na vivuli vya dini mwache rashid aendelee kukusanya sadakaGwajima si aliwaaminisha waumini wake kua corona imetokana na waves za 5G technology
Kama alikua muongo kwa hoja hiyo kwanini waumini wasimuone muongo kwa hoja hii ya chanjo?
Afu anatuondolea focus ana tusahaulisha kimakusudi tusahau ile video yake
Hamjiamini au ...Sasa si ukachanje kwani shida iko wapi mtoa mada,mbona hv vibandiko vimekuwa vingi sana wiki hii? Ww ukijiskia kuchanja nenda hujakatazwa.....hamjiamini au!!
Mimi sijakataa kuchanjwa nataka sana! Ila naogopa tu ile sindano halaf sina uhakika kama hiyo chanjo ina uhakika wa kukinga hayo maradhi au tunachoma tu halaf baada ya muda inaisha nguvu tatu naona hata nikichanjwa bado natakiwa kuchukua tahadhari vilevile sasa yanini?Watanzania hawaishiwi hoja kwa kweli.
ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ambayo serikali imejitoa kabisa kwamba litakalokupata wao hawawajibiki kwa lolote ?
Watanzania wamesahau kwamba hata ukienda hospitali una haki ya kukataa kutibiwa,una haki ya kukataa sawa,una haki ya kumkataa daktari usiyemtaka asikutibu.
Endapo ukikubali kutibiwa kwa ridhaa yako na katika tiba hiyo ukapata madhara basi hakuna daktari atakayewajibika eti ahukumiwe kwa jambo hilo.
Hata ukienda kufanya upasuaji lazima ukubali kusaini,usaini ukaenda ukafa kwenye upasuaji ujue hakuna utakayemlaumu kwa sababu ulikubali mwemyewe.
Hivyo sio kwenye korona tu hata kwenye tiba zingine wanaohusika na jambo hilo wanajivua endapo ukikubali kufanyiwa jambo hilo litakalo kupata lakwako wewe.
Hivyo serikali ipo sahihi kujitoa lwenye lawama kwa sababu mtu atachoma chanjo akiumwa kichwa tu atataka aiwajibishe serikali kwamba chanjo inamdhuru,katika hili serikali imefanya vyema.
ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ukishachanja unaambiwa uendelee kuchukua tahadhari ?
Watanzania hakuna chanjo utakayochukua alafu ukaambiwa ukae katika mazingira hatarishi ati kwa kuwa umepata chanjo,hakuna chanjo hiyo.
Angalia tu ukidungwa sindano ya kujikinga na tetenasi haina maana kwamba ujiachie tu wewe ujikate ovyo na kujiachia kwenye mazingira hatarishi.
Ukidungwa chanjo ya yellow fever haina maana eti ndio utaambiwa ukae tu kwenye mbu na mazingira hatarishi,lazima iwe ni muhimu kujiepusha na mazingira hayo hatarishi.
Hivyo hata chanjo ya korona ukidungwa haina maana ujiachie tu,lazima uendelee kujikinga.
Maana ya chanjo sio kutafuta matatizo yalipo,maana ya chanjo ni kukukinga endapo kwa bahati mbaya umepata ugonjwa,sasa wewe utafute kwa makusudi.
Ukicheza karate unatakiwa uepuke ugomvi,haina maana kwamba unajua kupigana ndo uchokoze watu.
ETI Baadhi husema sijui ukichanjwa utapata madhara kadha wa kadhaa,ni kweli unaweza kupata madhara kdha wa kadha lakini swali la msingi ni je chanjo hiii pekee tu ya corona ?
Jawabu ni kuwa chanjo zote zina madhara fulani yanaweza kutokea kwa mtu.
Mfano.
Kuna chanjo watoto wachanga wakichomwa wanapata homa sana lakini baadae wanatulia maisha yanaendelea chanjo hizi hazipigiwi kelele.
Unaweza kuchoma chanjo ukapata aleji kinga za mwili zikaanza kushambulia seli mwenzake za mwili ukaanza kupata machovu na matatizo mengine ambayo yanaweza kupotea baada ya muda fulani.
Zipo kinga au chanjo mfano kinga ya homa ya manjano tafuta side effects zake utaona miongoni mwa matatizo ambayo unaweza kupitia ni kama vilee.
Maumivu ya joints,maumivu ya misuli,kupata homa,mapele,kichwa kuuma n.k
Kwa hiyo kama chanjo ya corona itakuwa inaambatana na matatizo basi tukubaliane hakuna chanjo iliyosalimika.
Lakini pia naomba kuwauliza wanaosema hii chanjo baada ya muda ina madhara.
Je wamejuaje kama ina madhara wakati hapo hapo wanasema haijafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu usalama na madhara yake ?
Na je hayo madhara yataonekana baada ya muda gani ukishachoma chanjo ?
Swali la mwisho ambalo naomba niliulize ni kwamba tokea tuanze kudungwa hizi chanjo utoto wetu ambazo tisema tunajaribiwa mpaka hivi leo hii tumepata madhara gani kwa watu wote ambayo tutasema kisayansi yametokana na chanjo hizo za utotoni ?
NB : siko hapa kutetea chanjo,bali niko hapa kuvunja hoja dhaifu zinazotumika na baadhi ya watu kuwatisha wengine.
Nakubaliana na mambo ambayo kisayansi yana hoja zenye nguvu zinazoingia akilini na sio kuokota kila hoja tu na kuisema ili tuendee kulaumu.
Point ya kusema watu wasiwe na mashaka bado haibadilishi uhalisia, watu wamekua na mashaka kwenye vitu vingi sana ambavyo sayansi imekua ikifanya. Hata ishu ya moon landing watu kibao wana mashaka kua sio kweliKuthibitishwa kwake hakufanyo watu wasiwe na mashaka mkuu.
Halafu unajua nyie watu wa chanjo mmekaa kukejeli na sio kutoa hizo hoja zenu.
Bado nafatilia kupitia vipindi mbali mbali wanaelekeza vizuri na kwa weledi ila humu naona wote sawa tu , hakuna hoja mnazodai mnazo zaidi ya mifananisho.
Sikupingi kwa hilo, kumbe tuko pamoja kua sio ajabu watu kua na mashaka na hiyo chanjo. Kwahivyo sioni haja ya kushambulia wasioiamini kama alivyofanya mleta uzi.Point ya kusema watu wasiwe na mashaka bado haibadilishi uhalisia, watu wamekua na mashaka kwenye vitu vingi sana ambavyo sayansi imekua ikifanya. Hata ishu ya moon landing watu kibao wana mashaka kua sio kweli
Sayansi haipo kwa ajili ya kuwafurahisha wadau, kusema kitu fulani ni uongo eti kwasababu wewe haikikuridhishi sio sawa.
Mkuu kwenye hiyo ya kwanza uko sawa kabisa, wengi wao ndio wako hivyo.Wanaokubali chanjo wote sio kwasababu ya uhalali na usahihi wa chanjo bali kwa kupingana na mwenda zake(hawakubali lakn ndo ukweli). Wanaokataa ni vile tu mindset zao ni kuwa mzungu sio mtu wakutoa vitu kiholela nimjanja sana anamingo yake nyuma ya chanjo.
Niambie kitu gani ambacho watu wote 100% hawana mashaka nachoSikupingi kwa hilo, kumbe tuko pamoja kua sio ajabu watu kua na mashaka na hiyo chanjo. Kwahivyo sioni haja ya kushambulia wasioiamini kama alivyofanya mleta uzi.
Na nikusahihishe hapo, hakuna aliesema ni uongo, kua na mashaka na kitu haimaanishi ni cha uongo mkuu, kinaweza kua kweli na mashaka yangu yakatoweka kabisa ama kikawa uongo.
Mpaka hapa sijaelewa tunachobishana hasa ni nini ilhali unajua kua ni kawaida kwa kitu kutoaminiwa 100%.Niambie kitu gani ambacho watu wote 100% hawana mashaka nacho
Wengi walio na mashaka na chanjo sio ya kua wameingia lab kufanya testing na izo ishu ka izo, ni kupembua taarifa hii na ile kama ulivyofanya wewe na kuangukia upande huo wao nao kulingana na taarifa wanzaopata/pewa wameangukia upande mwingine.Unakua na mashaka kulingana na observation uliyofanya juu ya hicho kitu kua majibu yake haya relate na namna ambavyo wao wanavyosema au ni yale mashaka yasiyo hitaji uchunguzi bali mhemko?
For me, side effect ya chanjo ni kubwa kuliko kuishi bila chanjo.Mkuu kwenye hiyo ya kwanza uko sawa kabisa, wengi wao ndio wako hivyo.
Kwa upande wangu siipingi hiyo chanjo na mi nilikua napenda walete chanjo ila tu jinsi ilivoletwa ndio imenitia mashaka kidogo na najaribu kufatilia zaidi. Lakini humu ndugu zetu hawa ukiwaambia mashaka yako wanakushukia jumla jumla kama mwewe na kifaranga.
Hizi mindset za kua watu fulani wako sahihiwakati wote zaidi ya mwingine tuzipunguze jama
Sijashambulia mkuu,kushambulia ni kufanya kitu bila hoja.Sikupingi kwa hilo, kumbe tuko pamoja kua sio ajabu watu kua na mashaka na hiyo chanjo. Kwahivyo sioni haja ya kushambulia wasioiamini kama alivyofanya mleta uzi.
Na nikusahihishe hapo, hakuna aliesema ni uongo, kua na mashaka na kitu haimaanishi ni cha uongo mkuu, kinaweza kua kweli na mashaka yangu yakatoweka kabisa ama kikawa uongo.