Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 141
- 183
Deogratias Mutungi
Bwana Tundu Lissu mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA anajenga hoja na ana hoja pindi anapokuwa jukwaani akinadi ilani ya chama chake, lakini hulka binafsi ya Bwana Lissu kupitia hoja zake zinaonyesha ni kiongozi anayestahili kuwa “Nyampara” na hivyo kupoteza radha ya hoja zake anazozijenga majukwaani.
Binafsi namjua sana Bwana Lissu kuwa ni msomi na mjenga hoja aidha ni mdhaifu kwenye dhana ya ustahimilivu na maamuzi sahihi, kisiasa unapokosa “Ustahimilivu na maamuzi sahii” ni dhambi na unaweza kuingiza nchi kwenye matatizo makubwa yenye athari kwa wananchi na mali zao.
Kwa dhana hiyo Urais kwa Bwana Lissu ni nafasi inayompwaya sana sawa na kiatu cha oversize, Bwana Lissu ni kiongozi anayefaa kupewa nafasi ya “Unyampara” ili awaongoze wenzake, Unyampara sio tusi bali ni kiongozi anayestahili kutoa maelekezo kwa wenzake lakini asiye na mamlaka makubwa zaidi ya uamuzi, Kwa hulka za bwana Lissu anafaa kupewa nafasi ya “Unyampara” lakini si ukuu wa nchi kwa sasa..
Uongozi wa nchi hauitaji “Unyampara” Bali unahitaji kiongozi mwenye hoja za utatuzi wa matatizo ya watu, sera na falsafa zenye mrengo wa kiukombozi, Uongozi ni kipaji na karama, uongozi ni kujenga hoja chanya, uongozi ni dira na hekima ya kuyaishi matatizo ya watu, Uongozi si vitisho wala lawama, uongozi si fujo, uongozi ni muundo uliojaa matumaini ya kutatua kero za Wananchi hasa katika eneo la kiuchumi.
Kwa mantiki ilivyo kwa sasa ni kweli kuwa Bwana Lissu anahoja mbadala, lakini kwa hulka yake kisiasa ni kiongozi anayestahili kupewa nafasi ya “Unyampara” na si URAIS wa nchi yetu.
Watanzania tuwe makini Oktoba 28, tusipige kura kwa mihemko bali tuzingatie uwezo wa mtu kwa kiongozi atakaye tuvusha kwenda tutakako “KIUCHUMI” Aidha nashauri ni vema kura nyingi za ndio tukampa John Pombe Magufuli Kwa Tanzania bara na Zanzibar mpeni Dkt. Hussein Mwinyi hawa ni viongozi wenye uchungu na Watanzania, na wana sifa za uongozi wa kuongoza watu.