Kila siku nasisitiza elimu ya uraia inahitajika sana kwa baadhi ya wenzetu kuendelea na ujinga wa kuhoji vitu vidogo vidogo!.
Tanzania ni nchi moja, na uraia mmoja tuu!. Watanzania ni Watanzania bara wote na Watanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar, wako sawa sawa na wana haki zote za uraia sawa sawa kama Watanzania.
Hivyo Wazanzibari wana haki zote za kiraia ikiwemo kumiliki mali, ajira, elimu etc.
Japo Tanzania ni nchi moja ya JMT, ina sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar.
Tanzania Zanzibar ina utawala wake wa ndani kwa mambo yote yasiyo ya muungano, lakini Tanzania hatuna utawala wake wa ndani.
Kwa mambo yote ya ndani ya Zanzibar yasiyo ya muungano, ikiwemo ardhi, ajira ya SMZ, uongozi, etc, ni haki ya Watanzania Wazanzibari only.
Kutokana na hilo, kuna Watanzania wajinga wanadhani, Tanzania Bara ni kwa Watanzania bara tuu, na sasa wanahoji kwanini Wazanzibari wanaruhusiwa kila kitu huku bara, lakini wa Bara, hawaruhusiwi Zanzibar, hawa ni wajinga tuu na huo pia ni ujinga.
Kila Mzanzibari pia ni Mtanzania, lakini sio kila Mtanzania ni Mzanzibari. Tanzania ni kwa Watanzania wote, Wazanzibari wakiwemo ila Zanzibar ni kwa Wazanzibari pekee!.
P.