ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 754
- 1,478
Kwenye hoja namba 1 ya wingi wa nchi zinazokubali uraia pacha haimaanishi kuwa ina reflect idadi ya watu kwenye mataifa hayo.Nimeshangazwa sana na hotuba ya profesa Kabudi bungeni kuhusu uraia pacha.
Alianza kwa kusema amefanya utafiti Lakini alichokiongea ni uongo mkubwa na bunge lingelikuwa na heshima ya ukweli ingebidi aitwe ili kusahihisha makosa kibao kwenye utafiti wake.
Nimeona ni bora kufanya fact check ya hotuba yake:
1. 51% ya dunia hawana uraia pacha - uongo
Kati ya nchi 193 chini ya UN, zaidi ya nchi 100 zinaruhusu uraia pacha Japo sheria zinatofautiana kati ya nchi na nchi.
2. Ujerumani hawaruhusu uraia pacha. Uraia wao ni wa damu, Hata mtoto wa wageni akizaliwa huko anakuwa sio raia - Uongo
Ujerumani inaruhusu uraia pacha wa aina mbalimbali. Ukiwa na uraia wa nchi ya EU Unaweza Pia kuchukua uraia wa Ujerumani. Mtoto ambaye mzazi mmoja sio Mjerumani anaruhusiwa kuwa na uraia pacha. Watoto waliozaliwa Ujerumani na wazazi wasio Wajerumani wanakuwa Wajerumani Kuanzia 2000 ili mradi mzazi mmoja awe na uhalali wa kuishi Ujerumani.
3. Denmark hawaruhusu uraia pacha- uongo
4. Katoa quote ya Nyerere ya mwaka 1960 kuhusu uraia pacha
Kaacha quotes zingine nyingi za Nyerere za miaka baada ya 1960. Kwanza Huu ni mwaja 2023, Kweli anataka kutumia mifano ya 1960?
Kwa mfano kama Tanzania ikiwa ina sera ya kukubali uraia pacha haimaanishi wananchi wote tayari wanakuwa na uraia pacha, unaweza kukuta katika idadi ya watu Milion 60 ni watu wasiozidi 50,000 ndiyo wana uraia pacha. Na hoja ya Prof. ndiyo imejikita hapo