Hoja za Profesa Kabudi kuhusu uraia pacha si za kweli

Kwenye hoja namba 1 ya wingi wa nchi zinazokubali uraia pacha haimaanishi kuwa ina reflect idadi ya watu kwenye mataifa hayo.
Kwa mfano kama Tanzania ikiwa ina sera ya kukubali uraia pacha haimaanishi wananchi wote tayari wanakuwa na uraia pacha, unaweza kukuta katika idadi ya watu Milion 60 ni watu wasiozidi 50,000 ndiyo wana uraia pacha. Na hoja ya Prof. ndiyo imejikita hapo
 
kama 49% ya nchi za dunia kwa hoja yake haitoshi TZ kufuata sasa Kwanini tufuate hati maalum ambayo ni nchi mbili tu kati ya nchi 193 za dunia zinafuata?

Prof Kabudi anataka kuhusu Yeye kukaa Ujerumani miaka 9 ili tuamini anayajua ya Ujerumani, Kumbe hajui chochote sawa tu na mtu wa Manzese ambaye hajawahi kufika Hata AirPort.

Nawahofia wanafunzi wake Chuo kikuu UDSM.
 
Hivi Unajua Hata kinachojadiliwq hapa?

Wakati mwingine Kama Hujui Bora kukaa kimya.
EU Sera ya uraia kila nchi ina sera yake Wala hawana sera moja.

Hapa tunaongelea uraia pacha na sio Uhamiaji.
 
Kwenda zako huko wewe. Mbona wewe ulipotosha kuwa bwawa la mwl Nyerere lilivuja na kuleta mafuriko mpaka Morogoro.
 
Kwa lazima tuwe na uraia pacha?
 
Huyo mzee ni muongo wa muda mrefu, na anatumia udhaifu wa viongozi wengi kutokuwa na tabia ya kusoma kuwapotosha. Mzee huyu ametumika kutengeneza sheria nyingi mbaya za kulinda viongozi dhidi ya watawaliwa.
Unajua taratibu za kutunga sheria?
 
Kabudi ni janja janja hana lolote akitoa jicho basi watu wanajua kaongea point kinachombeba ni huo u profesa wa mchongo ila ni kenge tu ndio maana samia akaamua kumuweka kando na mambo ya mikataba akijua kabisa jamaa linatoa tu macho halina kitu kichwani.
 
Mbona unarukaruka....!!! Jibu hoja kwa hoja Tena na ushahidi.
Suala la ujerumani huo stringent issues zilizobebwa na hiyo hiyo uraia pacha wao uliosema?
 
Uraia pacha haukubaliki Tanzania.

Majaribio yote ya kubadili yatafail.
 
Hata mimi nilimskiliza, nikamdharau hasa pale aliposihiwa muda ikabidi aongezewe dakika. Profesa ni ,mtu anayetakiwa ajue kupangilia facts zake na kuzitoa ndani ya muda alio nao, siyo anaingia darasani lkwenyemkipindi cha dakika hamsini halafu anataka aongee kwa saa moja. Kabudi alisahahu ubongo nyumbani alipokuwa anakwenda bungeni akaishia kutoa pumba nyingi sana bungeni. Ni vizuri atunze ubongo wake kwenye pochi asijeusahahu siku nyingine.

Rafiki yangu mmoja alikuwa mwanajeshi wa kimarekani huko ujerumani akaoa mwanamke wa kijerumani. Jamaa huyo alikuwa ana dual citizenship ya Marekani na Trinidad & Tobago. Watoto wao wote wawili waliozaliwa waka retain citzenships za wazazi wao za Ujerumani, Marekani na Trinidad & Tobago. Sijui yeye alikuwa anazungumza Ujerumani ya wapi.

Kinachomata sana ni jinsi nchi inatunga sheria zake za dual citzenship. Kuna nyingine zinazoruhusu mtoto aliyezaliwa katika ardhi yake kuwa raia hata kama wazazi walikuwa wanasafiri wakiwa on tnasit. Na kuna nchi nyingine uraia unaruhusuiwa kwa vigezo vikali vya kutaka kuwepo na trail ya damu, wya wazazi na wababu. Dual citzenship conditions zinatofautiana kati ya nchi na nchi.
 
Nimeishi ulaya maprofesa wanachukuliwa kawaida sana ni kawaida kukuta manager ana diplôma kisha assistant ni profesa .elimu ni yako sisi tutakuweka kulingana na unaitumiaje na ww una attitude gani .Ulaya si lazima tuwaige yote maana wanamakasoro kibao ila hili nalo mkalitazame
 
Nchi za kiafrika ambazo zinaruhusu uraia pacha zimepata faida gani kutoka kwa raia wake wenye uraia pacha?
 
Kazi uliyoifanya ni ya upinzani na umeifanya vizuri mno 100% excellent.
Kazi ya upinzani ni ni rahisi kuliko kazi zote zinazojulikana, kazi hiyo ni kubisha na kupinga tu kila kitu tena bila hoja, whether Jambo lenyewe wanalijua au hawalijui, ni la maana au sio la maana, na hiyo ndio kazi namba 1 ya mpinzani na ndio chimbuko la upinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…