Rais SSH aliyesema wakati akiwa VP, muda hauongopi rangi zipo wazi hata maua ya Zambarau anapewa. Ukipendwa na Zambarau kuna jambo unafanya dhidi ya Tanganyika kwasababu wana chuki nayo. Niishie hapo
Pili, alichosema kuhusu manufaa kwa upande wa Zanzibar ni kweli.
Hoja ni kwamba Tanganyika inapoteza nini ikiwa Wazanzibar hawataki muungano!
Tatu kuhusu Wizara ya mambo ya nje, ni kweli Jakaya Kikwete aliwapa ruhusu ya kukopa.
Kelele unazosikia wanataka kukopa kupitia jina la JMT halafu hawalipideni linalipwa na Hazina Tanganyika inayoitwa Hazina Tanzania. Ikiwa wanakopa na wanalipa wenyewe sioni kama ni tatizo! sivyo! wao wanataka kupitia JMT !
Kuhusu misaada, nimewasikia Wazanzibar wengine na ma-digrii wakiishi nje ya nchi wakilizungumzia hili.
Misaada inayokuja ni fadhila wala haina 'guarantee' hivyo kuiongelea ni ukosefu tu wa elimu.
Bajeti ya ulinzi ni 3.3T ambayo Zanzibar haichangii hata senti!
Bajeti ya Mambo ya ndani na Taasisi za Muungano ni zaidi ya 2.5 Trilioni, Zanzibar haichangii hata senti tano.
Gharama za Wabunge wanaochaguliwa na watu 3,000 na mfuko wa jimbo la watu 3,000 zinatoka Tanganyika
Mishahara , marupu rupu na pensheni za Watumishi wa Muungano zinatoka Hazina Tanganyika
Kuna 4.5% sasa (9%) kwa mujibu wa mwenezi CCM Zanzibar, msaada wa kibajeti kutoka 49T za Bajeti ya Tanganyika
Mwaka 2023/2024 Bajeti ya Zanzibar isiyo na ulinzi , usalama , mambo ya nje na Muungano ilikuwa 2.8T.
Makusanyo ya Zanzibar kwa miezi 5 ni takribani 270 Bilioni ikiwa ni takribani 50 Bilioni kwa mwezi
Pia, Tanganyika imebeba Wazanzibar wengi kuliko wanaoishi Zanzibar , wanatumia resources za Tanganyika bila kubaguliwa iwe shuleni , Hospitali n.k. kwa jina la Tanzania kwasababu ile ile wao ni Watanzania na Wazanzibar
Hoja hapa ni kwamba gharama za Muungano na SMZ zinabebwa na kodi za Watanganyika , wanaposema misaada ni upuuzi tu maana wanapewa kuliko wanachoweza kukusanya au kutengeneza. Ni ukosefu wa matumizi ya elimu.
Tatu, kuhusu deni la umeme kutotozwa VAT na Tanesco si sawa. Ikiwa Tanesco ni shirika la Tanzania kwanini kuna ZESCO. Kukiwa na mashirika mawili tayari Tanesco inakuwa ya Tanganyika.
Kutotoza VAT ni kuwabebesha mzigo Watanganyika kwasababu gharama za uendeshaji Tanesco zinabebewa na Watanganyika, si Wazanzibar!
Hoja kwamba eti ni nchi moja ni ya kipuuzi kwasababu huwezi kuwa na ZESCO inayoongeza gharama za uendeshaji wakati Tanesco ingefanya peke yake. Lakini pia nchi moja ipi ikiwa Wabunge wa Zanzibar wanasema si Watanzania?
Kufuta deni la umeme ni kuwaumiza Watanganyika kwasababu Tanesco ikipata hasara anayefidia ni Mtanganyika.
Swali linabaki pale pale, Kwa kubebeshwa zigo la Bilioni 60 za umeme, Tanganyika inafadika nini na Muungano na ingepoteza nini kama isingepeleka umeme Zanzibar !
Nne, suala la kero ni la ajabu maana Zanzibar inalalamika dhidi ya nani?
Tanganyika haina structure ya gov. Zanzibar haiwezi kulalamika dhidi ya Tanzania kwasababu kanuni za asili zinasema '' huwezi kuwa mlalamikaji, halafu ukawa mwedesha mashtaka na kisha Hakimu''.
Leo SMZ inakuja na Kero dhidi ya Tanganyika. Mwendesha mashtaka ni VP wa JMT ambayo Wazanzibar wamo. Hakimu ni Rais wa JMT ambayo Wazanzibar wamo. Tanganyika inayolalamikiwa haina mwakilishi mahakamani, wala mahakama haitambui uwepo wake ingawa hukumu ni dhidi ya Tanganyika! all nonesense
Ndicho kilichopo sasa hivi na mwisho wa siku losers ni Watanganyika.
Kuna tatizo la waandishi wa habari wa Tanzania. Hakuna anayehoji maswali magumu na muhimu nadhani ni mapungufu ya kutojua au kujisomea . Mfano, sijasiki mtu akiuliza viongozi wa Zanzibar mambo haya
1. Mchango wa Zanzibar ni upi katika kuendesha Muungano
2. Kero za Tanganyika ni zipi zinazojadiliwa kwa upande wa Tanganyika
3. Formula la kugawana rasilimali za Tanganyika kwa jina la Tanzania zinazingatia nini
4. Ni wapi Bajeti ya SMZ inaonyesha wanalipa mikopo kupitia JMT na kwanini wasiruhusiwe kukop na kulipa wenyewe
5. Nani anasimamia masilahi ya Tanganyika ndani ya Muungano
6. Wazanzibar wanataka Muungano au la, na kama hawataki nini kinawazuia wakiwa na nyenzo na taasisi zote
7. Kwanini wasitumie taasisi zao, BLW au Wabunge kudai kura ya maoni kama Eritrea, Scotland, Timor, Quebec n.k
8. Wazanzibar wanadhani wapi wanadhulumiwa na Tanganyika, na Tanganyika inanufaika na nini katika muungano
Waandishi lazima wawe na uwezo wa kuuliza maswali si kukaa na kusikiliza hadithi kama wale wa ITV na ipad !