Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Ndio kielelezo cha utaifa wa Tanzania kinapotambulika kimataifa. Kwani Tanganyika na Zanzibar zipo mbinguni?.
Umesema hayo mambo mengine ni ufahari wa kidunia tu ila kwako muhimu ni Tanzania kuwa na kiti umoja wa mataifa ndiyo nimekuuliza huko umoja wa mataifa ni mbinguni siyo duniani? Hata hivyo nisikutwishe mzigo usiyohumudu maana inawezekana tunajadili vitu viwili tofauti.
 
Neno!
Tunautaka muungano. Tunataka ushirikiano na watu au nchi zingine. Lakini muungano huo ni lazima uwe wenye usawa na kuheshimiana kwa pande zote zilizokubali kuunga/kushirikiana..
Na pia muungano huo uwe na faida kwa pande zote. Mfano, Tanzania inapokuwa na MoU na mataifa kama Marekani, UK, Ufaransa , China n.k. utajiuliza ni kwa vipi? Uchumi wa Miji ya Beijing, New York , California n.k. ni mkubwa kuliko wa Tanzania! swali ni kwanini wanatuhitaji? Jibu ni rahisi kuna kitu kinaitwa ''mutual benefit'.

Swali, Muungano wetu na Zanzibar, Watanganyika wana kitu gani cha kufaidika?
Hii haina maana hatuhitaji Muungano, lakini Muungano uliopo una investment isiyo na return au dividend.

Lakini pia tunajiuliza pamoja na kubeba muungano kwanini tutumie muda mwingi na gharama kubwa kuwabembeleza Zanzibar na si ku invest katika maeneo yatakayokuwa na tija kwa ustawi wa Tanganyika
KWA HIYO: Sio UJINGA wala u - TIMBAKWIRI watu kuzisema kasoro hizi kwa malengo ya kurekebisha. Ujinga na u - timbakwiri ni kule kung'ang'ania kuishi ktk makosa au kasoro. Na huyo mtu ni wewe na wenzako wote huko CCM...
Makosa ni kudhani kwamba wataweza kuendelea na ulaghai huo daima milele.
Kwasasa hali ya muungano ni mbaya kwasababu walioubeba wamechoka! Nani atazuia wimbi linalovuma
Swali ni moja tu: Mataweza kuwafanya Watanganyika kuishi ktk ujinga wenu hadi lini?
Hilo halikubaliki na ni LAZIMA TUCHUKUE HATUA KUREKEBISHA..
' The train has just left the train'' fursa ilikuwa kupitia Tume ya Warioba, wakaihujumu.
Tanganyika itarudi ni suala la muda na haiuziliki. Marekebisho yatakuwa na gharama kubwa sana

Walifanya makosa kutowahi marekebisho wakati Watanganyika wakiwa kimya! hatari kubwa wasiyo iona viongozi ni ' Tanganyika ina upper hand'' ndiyo iliyobeba Muungano, haina cha kupoteza.
Viongozi wanapuuza Watanganyika bila kujua kwamba wanaohitaji Muungano ni Zanzibar!
Tanganyika inatoa haipati kitu! ina nini cha kupoteza !

Hawa viongozi wasipofanya jambo ipo siku Watanganyika wataamka na kusema ''NO' na huo utakuwa mwisho. Hizi projo za ' tutalinda kwa gharama yoyote hazina maana , Nyerere alionja joto la G55''
Je, yupo Nyerere mwingine?
 
Mkuu nakuelewa sana
Hatari ninayo iona ni watu kuachwa wafanye '' exploitation' ya jamii yetu iliyojaa wengi wasio na maarifa ya kutafuta ukweli. Kwa mfano kuna kijana kaniambia eti natakiwa nijibu 'uadhimu na uadimu wa Muungano''
Tena anasisitiza kwamba Pascal kaeleze vizuri sana kuhusu Muugano wa 'Union na Federation'

Huyo kijana anaamini kwamba kuna federation ya '' Tanzania na Zanzibar' kutoka kwa Pascal, na si yeye, unapokuwa na vijana kama hawa kwa wingi iwe kwa ignorance au uchawa bado kama Taifa tuna tatizo

Nilipomuuliza huyo kijana Federation ya Tanzania na Zanzibar inatokeaje, hakuwa na jibu.

Upotoshaji unapewa nafasi katika media na media kuacha wajibu wao .
Hivi media house ikiwa na editorial board inashindwa vipi ku 'fact check' kuhusu contents wanazochapisha!

Watu wenye ushawishi katik jamii wanapoongozwa na tamaa na ulafi kuna madhara makubwa.
Si kwamba wanafanya exploitation lakini pia wanafanya intellectual abuse na wana najisi akili za watu. Tunakuwa na vicious circle ya chawa na wapuuzi.
 
Zanzibar ni ndogo sana kiasi cha kuzisumbua akili za watu wengi wa bara wakaacha kutafuta mkate wao wa kila siku na kuanza kuiwazia. Ni sawa na wilaya mbili tu za mkoa wa Morogoro au Tabora.
Lakini inapewa mapato kuliko Morogoro au Tabora! mapato yanayotoka Morogoro na Tabora.
Hulioni tatizo hapo?

Lini Wananchi wa Morogoro na Tabora waliwahi kulipiwa umeme na JMT? Zanzibar wanalipiwa. Huoni tatizo?

Nafasi za ajira za Morogoro na Tabora zipo wapi? Zanzibar wanazo!
Nafasi za elimu ya juu na mikopo za Tabora na Morogoro ziko wapi? Zanzibar wanazo! huoni tatizo?


Unaweza ku ignore ukatafute mkate lakini bei ya mkate huo ni pamoja na bill ya umeme ya watu waliopunzika ufkweni Zanzibar! Ni pamoja na mishahara ya Wazanzibar wanaolala pale Mjengoni wakisema si Watanzania. Kwahiyo katafute mkate na maji ili ujaze ndoo inayovuja
 
Inapewa mapato? haina vyanzo vyake vya mapato unataka kusema?. Tunajaribu kushusha thamani Zanzibar kwa maarifa yetu ambayo upatikanaji wake una walakini.

Muungano una faida zake za pande mbili tatizo unapofikiria kuhusu hasara ukitumia nguvu nyingi unapoteza uwezo wa kuuona upande wa faida.
 
Kupewa mapato ni makubaliano ya kikatiba yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita. Nafasi za ajira za bara zipo nenda kwenye raasisi za kiserikali zinazotoa ajira watakupa mgawanyo wa kila eneo la Tanzania.

Nafasi za elimu pia zipo tena nyingi tu, hakuna kinachowagusa watu wa huku bara kisiwaguse wazenji pia.

Ni hulka zile zile za uchoyo, ubaguzi na umaskini pia. Tuna mamia kwa mamia ya fursa za kujiendeleza sisi wenyewe wa huku bara bila hata kugusa hicho wanachokipata ndugu wa visiwani.

Tembea tu na gari lako kutoka nje ya Dar kabla hujafika Morogoro utaona kushoto na kulia ardhi nzuri ambayo haijaguswa bado, bado haijatumika kuweza kuchangia pato kwa taifa. Tembea mikoani uone ardhi nzuri tu ambayo bado haijaguswa na hivyo haijaweza moja kwa moja kuweka mchango kwenye pato kuu la Taifa.

Ni aibu sana kwetu sisi wa huku bara kulia na hicho kidogo kinachokwenda huko viswani wakati tunao utajiri usioguswa leo hii miaka 63 baada ya uhuru.
 
Inapewa mapato? haina vyanzo vyake vya mapato unataka kusema?. Tunajaribu kushusha thamani Zanzibar kwa maarifa yetu ambayo upatikanaji wake una walakini.
Yes! tuonyeshe bajeti ya ulinzi, mambo ya ndani, nje katika bajeti ya SMZ.
Onyesha mikopo wanayopewa kama sehemu yao wapi wanarudisha wenyewe kama si JMT
Makusanyo ya kodi ya SMZ ni bilioni 60 kwa mwezi sawa na chini ya bilioni , bajeti ya 2023/2024 ni 2.4T!
Unajua ni kiasi gani 4.5% sasa ni 9% ya Bajeti ya JMT inakwenda Zanzibar! Morogoro na Tabora wanapata kiasi gani
Tuonyeshe wapi mapato ya TRA yamevuka kutoka SMZ kuja hazina Dar
Tuonyeshe wale Wabunge 80% wanalipiwa na bajeti ipi ya SMZ?
Kwanini mfuko wa Mbunge wa uende Zanzibar wakati hawana mchango wowote katika katika JMT
Kwanini Mbunge anayechaguliwa na watu 3,000 awe na haki sawa na Mbunge anayechaguliwa na watu 400,000
Kwanini wao wawe na kipaumbele zaidi ya raia mlipa kodi wa Tanganyika.
Muungano una faida zake za pande mbili tatizo unapofikiria kuhusu hasara ukitumia nguvu nyingi unapoteza uwezo wa kuuona upande wa faida.
Tuonyeshe na utushawishi kwamba Tanganyika inahitaji Muungano! hebu tushawishi ni kwa lipi au faida gani.
 
Kupewa mapato ni makubaliano ya kikatiba yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita.
Tuonyeshe wapi katika katiba imeelezwa hiyo!
Kumbuka wao ndio wanataka formaula ya kugawana rasilimali za Tanganyika! kama ipo kikatiba ni wapi?
Ni hulka zile zile za uchoyo, ubaguzi na umaskini pia.
Hkusikia wanataka passport kuingia Zanzibar! huo si ubaguzi
Hukuwasikia Wazanzibar hawataki Utanzania kwasababu ni Wazanzibar, huo si ubaguzi

Unashindwa kuelewa kwamba Ubaguzi wa Wazanzibar ndio chanzo cha matatizo na sasa ubaguzi huo itakula kwao. Watu wanaitaka Tanganyika yao ili Zanzibar ipate mamlaka kamili

Tunahitaji Tanganyika tusimamie mambo yetu, hatuna muda wa kubembelezana kila siku!

Ikiwa wanataka Muungano watasema wao , Tanganyika haina cha kupoteza wala kunufaika!

Narudia tena tuonyeshe au tueleze, kwanini Tanganyika inahitaji Muungano! ni kwasababu au faida gani
 
Narudia tena tuonyeshe au tueleze, kwanini Tanganyika inahitaji Muungano! ni kwasababu au faida gani
Karibu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Natumaini umeelimika
P
 

Rais SSH aliyesema wakati akiwa VP, muda hauongopi rangi zipo wazi hata maua ya Zambarau anapewa. Ukipendwa na Zambarau kuna jambo unafanya dhidi ya Tanganyika kwasababu wana chuki nayo. Niishie hapo

Pili, alichosema kuhusu manufaa kwa upande wa Zanzibar ni kweli.
Hoja ni kwamba Tanganyika inapoteza nini ikiwa Wazanzibar hawataki muungano!

Tatu kuhusu Wizara ya mambo ya nje, ni kweli Jakaya Kikwete aliwapa ruhusu ya kukopa.
Kelele unazosikia wanataka kukopa kupitia jina la JMT halafu hawalipideni linalipwa na Hazina Tanganyika inayoitwa Hazina Tanzania. Ikiwa wanakopa na wanalipa wenyewe sioni kama ni tatizo! sivyo! wao wanataka kupitia JMT !

Kuhusu misaada, nimewasikia Wazanzibar wengine na ma-digrii wakiishi nje ya nchi wakilizungumzia hili.
Misaada inayokuja ni fadhila wala haina 'guarantee' hivyo kuiongelea ni ukosefu tu wa elimu.

Bajeti ya ulinzi ni 3.3T ambayo Zanzibar haichangii hata senti!
Bajeti ya Mambo ya ndani na Taasisi za Muungano ni zaidi ya 2.5 Trilioni, Zanzibar haichangii hata senti tano.

Gharama za Wabunge wanaochaguliwa na watu 3,000 na mfuko wa jimbo la watu 3,000 zinatoka Tanganyika
Mishahara , marupu rupu na pensheni za Watumishi wa Muungano zinatoka Hazina Tanganyika

Kuna 4.5% sasa (9%) kwa mujibu wa mwenezi CCM Zanzibar, msaada wa kibajeti kutoka 49T za Bajeti ya Tanganyika

Mwaka 2023/2024 Bajeti ya Zanzibar isiyo na ulinzi , usalama , mambo ya nje na Muungano ilikuwa 2.8T.
Makusanyo ya Zanzibar kwa miezi 5 ni takribani 270 Bilioni ikiwa ni takribani 50 Bilioni kwa mwezi

Pia, Tanganyika imebeba Wazanzibar wengi kuliko wanaoishi Zanzibar , wanatumia resources za Tanganyika bila kubaguliwa iwe shuleni , Hospitali n.k. kwa jina la Tanzania kwasababu ile ile wao ni Watanzania na Wazanzibar

Hoja hapa ni kwamba gharama za Muungano na SMZ zinabebwa na kodi za Watanganyika , wanaposema misaada ni upuuzi tu maana wanapewa kuliko wanachoweza kukusanya au kutengeneza. Ni ukosefu wa matumizi ya elimu.

Tatu, kuhusu deni la umeme kutotozwa VAT na Tanesco si sawa. Ikiwa Tanesco ni shirika la Tanzania kwanini kuna ZESCO. Kukiwa na mashirika mawili tayari Tanesco inakuwa ya Tanganyika.

Kutotoza VAT ni kuwabebesha mzigo Watanganyika kwasababu gharama za uendeshaji Tanesco zinabebewa na Watanganyika, si Wazanzibar!

Hoja kwamba eti ni nchi moja ni ya kipuuzi kwasababu huwezi kuwa na ZESCO inayoongeza gharama za uendeshaji wakati Tanesco ingefanya peke yake. Lakini pia nchi moja ipi ikiwa Wabunge wa Zanzibar wanasema si Watanzania?

Kufuta deni la umeme ni kuwaumiza Watanganyika kwasababu Tanesco ikipata hasara anayefidia ni Mtanganyika.

Swali linabaki pale pale, Kwa kubebeshwa zigo la Bilioni 60 za umeme, Tanganyika inafadika nini na Muungano na ingepoteza nini kama isingepeleka umeme Zanzibar !

Nne, suala la kero ni la ajabu maana Zanzibar inalalamika dhidi ya nani?

Tanganyika haina structure ya gov. Zanzibar haiwezi kulalamika dhidi ya Tanzania kwasababu kanuni za asili zinasema '' huwezi kuwa mlalamikaji, halafu ukawa mwedesha mashtaka na kisha Hakimu''.

Leo SMZ inakuja na Kero dhidi ya Tanganyika. Mwendesha mashtaka ni VP wa JMT ambayo Wazanzibar wamo. Hakimu ni Rais wa JMT ambayo Wazanzibar wamo. Tanganyika inayolalamikiwa haina mwakilishi mahakamani, wala mahakama haitambui uwepo wake ingawa hukumu ni dhidi ya Tanganyika! all nonesense

Ndicho kilichopo sasa hivi na mwisho wa siku losers ni Watanganyika.

Kuna tatizo la waandishi wa habari wa Tanzania. Hakuna anayehoji maswali magumu na muhimu nadhani ni mapungufu ya kutojua au kujisomea . Mfano, sijasiki mtu akiuliza viongozi wa Zanzibar mambo haya
1. Mchango wa Zanzibar ni upi katika kuendesha Muungano
2. Kero za Tanganyika ni zipi zinazojadiliwa kwa upande wa Tanganyika
3. Formula la kugawana rasilimali za Tanganyika kwa jina la Tanzania zinazingatia nini
4. Ni wapi Bajeti ya SMZ inaonyesha wanalipa mikopo kupitia JMT na kwanini wasiruhusiwe kukop na kulipa wenyewe
5. Nani anasimamia masilahi ya Tanganyika ndani ya Muungano
6. Wazanzibar wanataka Muungano au la, na kama hawataki nini kinawazuia wakiwa na nyenzo na taasisi zote
7. Kwanini wasitumie taasisi zao, BLW au Wabunge kudai kura ya maoni kama Eritrea, Scotland, Timor, Quebec n.k
8. Wazanzibar wanadhani wapi wanadhulumiwa na Tanganyika, na Tanganyika inanufaika na nini katika muungano

Waandishi lazima wawe na uwezo wa kuuliza maswali si kukaa na kusikiliza hadithi kama wale wa ITV na ipad !
 
Punguza chuki na roho mbaya. Zanzibar ni sehemu ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa Bara.
 
Tanganyika kwa sababu ya hasira ya uzanzibari haitadumu huo ni wosia wa Mwalimu Nyerere. Tusijione eti tupo salama sana kuweza kuwa peke yetu.

Umoja ndio kila kitu kwa nchi hizi za kiafrika, huu usalama wa Tanganyika ni kwa sababu tupo ndani ya muungano nje yake kuna ubaguzi mwingine unaokwenda kuzaliwa baina yetu sisi kwa sisi.

Tupunguze hasira na akili za kukomoana, hata Baba na Mama wanaoishi miaka 70 pamoja haina maana siku zote kwao ni sherehe tu, tupunguze hizi jazba zina madhara kwetu sis wenyewe tunaojiona tuna kila haki.
 
Chuki dhidi ya urais wa Samia inasumbua baadhi yetu hakuna jema atakalolifanya likaonekana ni la maana kwa ustawi wa Tanzania. Hizi hoja za utanganyika zinakuzwa kwa sababu ya uzanzibari wa Samia sio zaidi ya hapo.

JPM hata angefanya makosa makubwa kiasi gani hakuna ambaye angesema chochote. Nyerere pia hakuna ambaye aliweza kusema chochote, SSH akifanya chochote japo ni kidogo kulinganisha na walivyofanya watangulizi wake zinaanza nongwa za kila aina!.

Walijaribu kupiga kelele kisa mkataba wa kibiashara na DP World na ukichunguza kwa umakini wahusika wanaohoji masuala ya muungano ndio wale wale waliopinga bandari zetu kuwa na uwekezaji utakaopanua wigo wa ufanisi.

Lakini misukosuko ndio sifa ya uhusiano wenye maisha yanayodumu.
 
Hapana! Ubaguzi wameanza wao! kwani si miaka yote wanasema Tanganyika imevaa koti la Muungano?
Husikii wakisema wao siyo Watanzania! Huwasikii wakidai Watanganyika waende kwao na passport

Akisema Mtanganyika ni tatizo, akisema Duni, Jussa na OMO ni halali! huu upuuzi umefika mwisho.
Tunawaambia wazi bila kumung'unya maneno, wao ndio wanauhitaji Muungano! shut up or put up

Hatuhitaji malumbano yasiyo na mwisho, Zanzibar inachukua rasilimali nyingi sana kuliko mkoa wowote na haichangi chochote. Tunahitaji kusonga mbele, hatuwezi kuishi kwa ku please watu milioni.
Tunachukua resources Simiyu, Geita na Njombe mikoa michanga kabisa kupeleka kwa nchi ya karne tano!


Umesahau ni wamoja kwasbabu ya adui Tanganyika. In fact wanataka mamlaka kamili hawataki muungano.

Hatuwezi kuishi kwa fikra tu kama unavyosema! jibu hoja moja baada ya nyingine
Nimekuuliza Tanganyika ina nini cha kupoteza ikiwa watapewa mamlaka kamili!
Nimekuuliza mchango wa Zanzibar kwa Tanganyika ni upi
Kwanini wanapewa hadhi ya raia daraja la kwanza wakati wakichangia sifuri katika Muungano
 
walidai wanaeneo lao mkuranga TANGANYIKA
Uliziba maskio hukuona hatari bandari kupewa mwarabu kwa mkataba wa kimangungo
Inakuwa vipi mwanaume kuwa chawa wa mwanamke tena si waAsili yake mwenye kujitapa waarabu ni wajomba zake
wanaume kama mabinti malaya
 
chuki zipo wapi? Jibu hoja
Huna hoja mkuu Zanzibar ina ukubwa wa wilaya mbili za huku bara, hicho kinachopelekwa huko kimeanza kwenda jana au juzi?.

Unapalilia chuki na madhara yake yanaweza kabisa kuja kuwa sumu kama sio leo basi hata muongo mmoja ujao.
 
Hekima, umoja na amani na hizi ni ngao zetu Afrika na watu wake - maneno ya wimbo wa Taifa walioyatunga wana akili na waliona watu wenye fikra kama za kwako.

Huwezi kila kitu ukakipima kwa mali au kwa mchango wa kiuchumi, mara nyingi data hizo ni taarifa tu za kujengea hoja kwenye vikao au mikutano kiuhalisia hazina nguvu kuliko utashi wa wanaoungana,

Hizi chuki dhidi ya Muungano na wazenji zinazaliwa siku zote wakati Rais akiwa ni wa huko kizimkazi akiwa wa huku Chato na mkatoliki mwenzetu hayupo hata mmoja mwenye kuidai Tanganyika. Msingi wa kuzaliwa kwa Tanganyika ni roho ya kisasi dhidi ya Uzenji, huo utanganyika pia hauwezi kuwa na maisha marefu.
 
Naelewa nguvu inayokuwa nyuma za hoja ya utanganyika kwamba ni kutaka kulipa kisasi kwa yanayosemwa na hao wa upande wa pili. Sioni uhai wa Tanganyika ikisimama yenyewe na ikadumu.
Hakiuna kulipa kisasi, Tanganyika ni dude kubwa sana haliwezi kulingana na Zanzibat. Kinachotokea sasa hivi ni kuchoshwa na kelele na madai ya kipuuzi ya Wazanzibar. Mfano, wameondoa Uhamiaji katika mambo ya Muungano, unaelewa hilo? Zanzibar wanapokuwa juu ya katiba ya JMT na kuwa raia wa daraja la I kwa upendeleo wakati hawana mchango wowote kwa maendeleo ya Tanganyika inakera! Tunahitaji muda wa kufikiri mambo muhimu si kaeneo ka watu laki 5 milioni 1 wakiishi Tanganyika.
Yes tulimpinga kwasababu alifanya hayo na mfano mmoja ni Uwanja wa Chato ambao ni hasara.
Tulimpinga kwa kauli zake za kipuuzi kuhusu watu wa kanda fulani ''watusubiri'
Watu wote waliompinga ni wale wanaotaka umoja. Na hata Kikwete Tulimpinga kwa kuendekeza ufisadi.
Mkapa tulimpinga kwa kupallilia ufisadi. Mwinyi tulimpinga kwa sera zake hasa za uchumi.
Nyerere tunamsema kila siku na mimi ni mmoja wao hasa kuua vyama ya ushirika na ujamaa
Samia atapingwa without exception!
Kwahiyo unadhani kama hayo yapo Wanaozuia ni Wazanzibar!
Mstaarabu huvumilia na hutafuta namna za kumaliza kero zinazosumbua uhusiano wake na jirani yake wa karibu. Hakuna kisichoweza kutatulika kwa maongezi.
Hapana tumewavumilia na sasa ni kero kwetu, tunahitaji muda wa kufikiri namna ya kushirikiana na nchi zinazotuzunguka zenye population ya 100M. Kila siku wao wanataka hawana cha kuwajibika! hapana

Nimekuuliza, tushawishi hapa jamvini kwanini Tanganyika inahitaji Muungano kiasi cha kutoa rasilimali nyingi kiasi hicho. OMO kasema 54% ya bajeti ya Zanzibar inategemea pesa za Tanganyika, na bado wanataka kupewa zaidi.
 
Huwezi kila kitu ukakipima kwa mali au kwa mchango wa kiuchumi, mara nyingi data hizo ni taarifa tu za kujengea hoja kwenye vikao au mikutano kiuhalisia hazina nguvu kuliko utashi wa wanaoungana,
Yes tunaungana kwasababu za Uchumi1 matatizo mengi duniani yanatokea kwasababu za uchumi.
Ni uchumi tu! Tunahitaji mshiriki wa Muungano. Zanzibar wanadai hadi inakera! Sasa hivi wanataka eti kuwe na formula ya kugawana rasilima za Tanganyika. Wao kila siku ni kugawana hutawasikia wakishiriki kuchangia au kujenga.
Hakuna chuki ni hisia zako. Maalim Seif alidai mamlaka kamili miaka zaidi ya 20, mbona hujasema ni chuki
Jussa , OMO na Duni kila siku wanatukana Muungano mbona hujaona ni chuki
Sasa hivi wanataka twende Zanzibar kwa passpor, hujaona ni chuki
Wanasema wao si Watanzania huoni kama ni chuki
Wazanzibar wanamtukana Mwl Nyerere wakisema ''Laanatullah' kila siku huoni ni chuki
Hawataki hata ndizi ivuke bahari lakini mkono wa tembo kutoka Mombasa ni sawa, huoni ni chuki
Wana vitambulisho vya kuwabagua Watanganyika, huoni kama ni chuki

Kwa taarifa yako waliorudisha neno Tanganyika wakisema '' Watanganyika wamelala' ni Wakoloni weusi , wanaiba rasilimali (wanaiba zero) ni Wazanzibar!

Kwanini Mtanganyika akisema yaishe mnasema ni chuki! Yaani yote hapo juu hukuwahi kuyasikia.
Hapana, wapewe mamlaka kamili sisi tunahitaji Tanganyika. Ikiwa watataka muungano ni wao waje waombe, Tanganyika haina cha kupoteza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…