Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Mpango mzima ni kuungana, kwanini Tanzania tufikirie kuungana na Sudan Kusini walio kilomita zaidi ya 3000 halafu tufikirie wakati huo huo kutengana na Zanzibar?. Ni somo lenye kuhitaji hekima nyingi sana kuliko jazba na visasi.
Nani anasema kuna kuvunja Muungano? Wanaosema ni Wazanzibar
Tueleze ni kwa namna gani Zanzibar inaweza kuwa na mamlaka kamili bila kuvunja Muungano

Hata elimu ya mtaani tu inatuambia kwamba unapokuwa na ushirika na mtu au watu wengine lazima utoe sehemu.

Tanganyika imebeba Muungano na kuibeba Zanzibar kwa miaka zaidi ya 60. Kinachoonekana ni Zanzibar kudhani ni sehemu ''special' ya Muungano na wana umuhimu sana. Well, kila kitu wanataka kiwe na ' Uzanzibar'
Kwa sehemu kubwa inatuathiri ndio maana tunasema turudi katika makubaliano ya Muungano kwa kuanza na Tanganyika. Hili litawasaidia Wazanzibar kupata mamlaka (sehemu) na itawapunguzia gharama Watanganyika.

Kwa mfano, Wazanzibar wanalalamika kuongezwa mambo ya Muungano na kwamba ni kuwaonea.
Hoja yao ni nzuri sana, solution ni moja kuondoa mambo yote yaliyoongezwa kutoka 11 hadi 22 wanayodhani Tanganyika inanufaika nayo

Mfano
Tuondoe Elimu ya Juu
Tuondoe hali ya hewa
Leseni za viwanda
Taasisi kama mawasiliano

Kwa mifano hiyo mitatu, nieleze Tanganyika inanufaika na nini kwa hali ya hewa kuwa jambo la muungano! unaweza kuona ni kelele tu kwa kukosa elimu. By the way wote wanaolalamika elimu ya juu kuwa muungano wamesoma Tanganyika katika vyuo vya Tanganyika tena BURE.

Kuondoa mambo ya muungano hakuna athari yoyote kwa Tanganyika kwasababu hakuna kitu pale!
Tunachohitaji mambo hayo yaondolewe kwa staha na heshima na si ujanja na ulaghai

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais OMO, Uhamiaji wameondoa katika Muungano! guess what Wafanyakazi wa Uhamiaji na majengo yaliyojengwa miaka 2 tu yanatoka Hazina Dar es Salaam.

Lakini si hayo tu, tunahitaji kuona Wazanzibar wanachangia Muungano kama ilivyo Mikoa michanga ya Geita, Simiyu, Njombe. Hatuwezi kuwa na ushirika wakati Zanzibar wanadai tuu hatuwaoni katika huduma za Muungano!
 
Mkuu Nguruvi3, nimeshindwa kabisa kuelewa jinsi akili za baadhi ya Watanganyika wenzetu zinavyofanya kazi.
Mkuu inasikitisha! Mpuuzi anasimama na kusema '' waje kwa passport'' Watanganyika pale mjengoni wametoa macho tu. Mpuuzi yule yule anasimama na kusema '' yeye si Mtanzania'' watu wamekaa kimya!
Karibia nusu ya wanaojitambulisha kama Wazanzibari makazi yao ni Tanganyika na walezi wao ni Watanganyika.
Kwa mujibu wa Prof Makame wa SUZA akitoa mhadhara wa Muungano alisema '' Wazanzibar takribani 1.2M wanaishi Tanganyika, muungano ukivunjika watarudi Zanzibar! utawapa nini , wataishi wapi''
Kama vile watoto wadogo, kwa kauli ya Baba wa Taifa, ingawa tumewapakata wanatunyea na tukiwaacha wanalia.
Tumewapakata mgongoni bado wanacheza ngoma juu ya migongo yetu! wanaweza kutembea nadhani
Inavyonekana sasa baada ya kupata ufadhili upya kutoka wa wajomba zao hawatuhitaji tena Watanganyika.
Hicho ndicho kinawatia kiburi , nadhani wapewe fursa ya kuhanagaika na wajomba! hatuna cha kupoteza
Ila wakikumbuka maziwa na asali ya mama Tanganyika bado wanasita kwa hadaa za mama wa kambo.
Mkuu umri utakukumbusha zama zile wakitaka kitu wanasema '' msipotupa abcd tutavunja muungano'' siku hizi kauli hiyo hutaisikia maana wapi pengine wanaweza kupata maziwa na asali kama Tanganyika
Kwa msaada wa wajomba na kina Pascal Mayalla watakomba kila wanaloweza na kuiacha Tanganyika hoi.
Hakika uvumilivu una mwisho…
Na hilo linaendelea kwa nguvu sana! ipo siku hawa Watanganyika wasiojitambua watabaki na Tanganyika tupu, na tutaelekea ujombani kuomba
 
Pascal Mayalla

Raia wa nchi moja kama unavyosema wana mamlaka 2 tofauti za Uhamiaji, tutajadili

Rejea bandiko 196 , Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ Bw. Othman Masoud Othman (OMO) ametaja mambo yaliyoondolewa katika Muungano kwa ubabe na jeuri tu ya Wazanzibar kwama ifuatavyo;
Ushuru wa Forodha
Bandari
Gesi na Mafuta
Uhamiaji

Tuanze na Uhamiaji. Ni kwa utaratibu gani Uhamiaji iliondolewa katika Muungano?
Ilikuwaje mwaka wa fedha uliopita Uhamiaji JMT ilijenga majengo Zanzibar wakati si jambo la Muungano?
Tena katika kuficha matumizi ya fedha za Tanganyika, alialikwa kiongozi mkubwa kutoka Tanganyika

Inakuwaje Uhamiaji makao makuu wapeleke fedha za mishahara na malipo mengine Uhamiaji Zanzibar ikiwa iliondolewa ''kinyemela' na hatujui ni awamu gani ilifanya hivyo.

Tunawazaje ku control Passport tukiwa na mamlaka 2 tofauti?
Kwanini Watanganyika hawataarifiwi mabadiliko makubwa yanayofanywa na Wazanzibar peke yao!

Bandari: Ni lango la ''nchi'' kutoka eneo lolote. Bandari ni jambo la Muungano. Ni utaratibu gani uliondoa bandari katika Muungano? Nani alishirikishwa kutoka Tanganyika?

Kwanini mapato ya bandari Tanganyika yanahudumia Muungano na ni sehemu ya 4.5% (sasa ni 9 kwa mujibu mwenezi CCM Zanzibar'). Kwanini mapato ya bandari za Tanganyika yawe ya Muungano! ya Zanzibar yako wapi!

Gesi na mafuta
Kwanini gesi ya Mtwara itoe mapato yanayohudumia Muuungano na Zanz,ibar lakini SMZ imeondoa ya Zanzibar !

Ushuru wa forodha
kama nchi moja tunapaswa kuwa na ushuru wa forodha mmoja. Ikiwa kuna haja ya kutoa asilimia kwa SMZ ingeanishwa. Hili lingezesha bidhaa na huduma kutoka eneo moja la Tanzania kwenda jingine ziwe sawa.

Kwasasa ushuru wa forodha wa Zanzibar ni mdogo na ni uchochoro wa bidhaa kutoka nje.

Wazanzibar wasiotaka ushuru wa forodha wa pamoja wanataka waingize bidhaa Tanganyika kama nchi moja ( Ni kwa kutumia upuuzi wa kila mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar)

Jambo hili lina athari kwa uchumi wa Tanganyika kwasababu Zanzibar inatumiwa na wafanyabishara kama uchochoro mchafu wa kukwepa kodi. Lakini pia linaua biashara za Tanganyika kwasababu ushuru una uwiano na mauzo. Mtanganyika anayeingiza bidhaa za nje analipa zaidi na bei zake zitakuwa juu ukilinganisha na wakwepa kodi kupitia Zanzibar na walipa ushuru kidogo wa Zanzibar.

Bw Mayalla unatakiwa kupata elimu ya haya mauza uza. Haitoshi tu kusema '' Raia wa nchi moja, nyuma ya pazia Uhamijaji imeondolewa kinyemela hatujui ni awamu gani''

Mag3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…