Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

no gentleman,
usiwanyime publics mawazo na maoni ya yako ya maana na muhimu juu ya jambo hili, ambayo inaashiria kabisa dhahiri shahiri unayo. usiwe mchoyo au mbinafsi sana kwenye vitu vya maana, vizito na muhimu hivi bana.....

ni kwasabb ya uelewa na ufahamu usio wa kutosha, juu ya jambo hili la muungano, ndio maana, tupo hapa tulipofikia hususani kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

jambo hili linaelezwa na kujadiliwa nusu nusu, tena kwa ukali usio na sababu, bila kueleza au kujadili mpaka mwisho, ili kusudi waTanzania waelewe nyeusi na nyeupe bayana.....

sasa hii shule na darasa la kupanic na kusema sitaki tena majadiliaona wakati nafasi na jukwaa ndio hili, sio jambo lenye afya kwa academicians na visionary professionals who are aiming at transforming a certain agenda into other form or established formation 🐒

ni uchoyo na ni ubinafsi wa kuwanyima waTz uelewa na ufahamu zaidi kwenye suala hili la muungano.

Natoa wito wa majadiliano kuendelea licha ya setbacks, dhihaka na vitimbi miongoni mwetu na kwa baadhi ya wachangiaji. Hivyo vitu hochee kujadiliana zaidi.

Tusuonge kwa pamoja kwa upendo, mpaka mwisho kwenye hili safari hii, huku amani miongoni mwetu ndio ikawe hitimisho la majadiliano na hoja yenyewe 🐒
 
Unaongea ki layman namashaka sana na kula yako ya siku.. kuwa makini usije ukawa unaishi maisha ya kusindikiza watu kwenye mafanikio

Linapokuja suala la Uzanzibari na utanganyika ni suala pana ..

Kwanza unabidi ujue visababishi vya Zanzibar kuomba kuungana na Tanganyika kipindi kile ilikuwa ni sehemu ya kiusalama na hofu ya kutawaliwa na machafuko kwa sasa haipo tena hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuishikilia huu muungano unaogemea upande mmoja..

Wakati mwingine naweza nikawa naelezea mtu ambaye hajui historia yeyote zaidi ya kujifanya anajua
Mtu yeyote haijalishi ni msomi au Lah lazima ataona kasoro zilizopo katika hichi kinachoitwa Muungano Uchwara
 
mihemko ya nini sasa angali inaonekana una hoja za maana kabisa, ingawa bado unaghadhabu, ubinafsi na kujisifu ambako hakuna maana yoyote kwa jamii, hivyo baki navyo kama vinakusaidia 🐒

usinielekeze mimi binafsi hiyo elimu muhimu sana unatoa, elekeza kwa ujumla wana JF fraternity wanaofatilia kwa makini mijadala huu wa maana sana, ili tuchote kwa pamoja elimu, uelewa na ufahamu wa jambo hili la muungano 🐒

achana na habari ya kuhitimisha kwamba iwe hivi au vile, yafaa kufahamu kinagaubaga mambo muhimu kabla ya hatua hiyo muhimu 🐒

nachelea kusema, ukielekeza mambo haya muhimu sana kwangu huchelewi kuanza kuyaporomosha zaidi kama ambavyo umeanza kupasha pasha moto kwenye ufunguzi wa haya maelezo yako dhidi yangu yangu kwenye aya ya kwanza na kwenye aya ya hitimisho.

si muhimu na wala hayana maana . Cha kuzingatia ni Muungano kiungwana 🐒
 
Funny
Bush lawyer Paskali Njaa eti anajua sheria ya katiba kuliko Warioba na Lissu....
 
Muungano ni kama ndoa, mwanamke kama kachoka moe talaka, usiwazikilize mashemeji ambao wanatumia mali zako, hao watakuongopea tu.

Kwenye huu muungano tanganyika ndio mwanaume, kama kweli wa uoande wa pili hawataki basi waachieni taifa lao, sio kusikiliza wanasiasa uchwara na wachache wenye kufaidika huku tanganyika.

Kwani faida ya huu muungano haswaa ni upi!?
 
Funny
Bush lawyer Paskali Njaa eti anajua sheria ya katiba kuliko Warioba na Lissu....
kwan warioba na Lisu wanajua sheria zipi au gani zaidi ya zilizopo tena wazi kabisa hapa Tanzania, ndugu muungwana ?🐒

ama kuna sheria za ziada tofauti na zilizopo kwenye katiba na zinazotumika kwenye sekta na mihimili ya nchi ambazo ni wew, Lisu na warioba pekee ndio mnazijua?🐒

by the way,
who is warioba or lisu? si ni waTanzania kama wengine tu....

what is so special to them, kupigwa risasa au kua waziri Mkuu? 🐒
 
Wewe kijana kichwani hauna kitu, ungejua usingekuwa unaandika andika hizi insha zako.. haujui chochote na wewe unaandika uonekane unacha kuandika kumbe kichwani hauna kitu sidhani kama unachoandika unakisoma au wewe ni Mzanzibari maana unatabia za kizanzibari uwezo mdogo kichwani naignore posts zako unaandika utumbo tu
 
Hoja za uzanzibari zipo miaka yote, na zinachekewa, zinaonekana ni ushujaa, Ila zikiguswa hoja za utanganyika ndio watu matumbo ya kuhara yanawabana, ni heshima kuitwa mzanzibari Ila ni ujinga na ubaguzi kuitwa mtanganyika!!!!
 

Leo nimejitahidi kusoma makala yako hadi mwisho na kwa msingi huu, nina neno la kusema..

Ndugu Pascal Mayalla mimi sijaona mtu ambaye ana shida na muungano huu..

Tatizo la sisi watu unaotuita "vitimbakwiri" ni muundo wa muungano. Ni hilo tu

Na huwezi kuanza kuhoji na kukosoa muundo wa muungano huu pasipo kuzitaja nchi mbili zinazounda muunga huu i .e Tanganyika na Zanzibar..

Aidha, huwezi kuhoji na kukosoa muundo wa muungano huu bila kuwataja Watanganyika na Wazanzibar ambao ni wakazi wa nchi zinazounda muungano huu..

Tunachohitaji ni kurekebisha muundo wa muungano ili kuondoa hizi kelele..

Kama na hili nalo unaliona ni tatizo na ndani ya matatizo haya mko tayari kuulinda muungano huu kwa gharama zozote, basi upande wa pili nasi tunasema, kwa gharama yoyote tutahakikisha muungano huu unarekebishwa au unapotolea mbali huko..
 
Mkuu nataka kukupabacho ni toafuti elimu hapa , maana mnatumia elimu kweny uhalisia kitu ambacho ni tofauti
 
ndugu muungwana, mwerevu,
mbona unaleta mihemko na panic kama zote yaani, nini shida?, malalamiko, gubu na ubinafsi wako si muhimu sana , tafuta namna binafsi kutatua hiyo shida yako 🐒

imotional stability control yako ni zero sio,

wew ukiignore au ukiblock, achilia mbali mimi hata mwingine yeyote, inanisaidia nini mimi? hiyo ni useless kabisa kwangu, do it hardly ikiwa inakusaidia 🐒

lakini sio kubwekabweka hapa na huna content, mie nababaika na hiyo kitu unadhani ambayo ni haki na uhuru wako 🐒
 
Ndugu Pascal kuna kitu hujaelewa kuhusu malalamiko ya wananchi wa pande zote mbili. Kero za muungano ndiyo shida hivyo kuwafanya wahoji muungano wenyewe.

Zanzibar inaonekana ilihali Tanganyika imepotea.

Zanzibar wana serikali yao na mambo mengine yote wanayo. Hata ikitokea leo Muungano unavunjwa Zanzibar wao wako kwenye safe side.

Ikitokea watu wakadai kuvunjwa au kurekebisha Muungano, Zanzibar wao maamuzi yatakuwa approved na Rais wao. Tanganyika nyie wenzetu ndiyo kwanza mtaanza kujikusanya mjue itakuaje.

Siku hizi sikuelewi elewi hivi pascal
 
Hakika siku hazigandi, Pascal kwisha habari yake! Mzee tunafahamu sabasaba iko karibu, ni lazima ujikombe ili upate matangazo ya nssf, CRDB na mengine.

Hongera sana kwa kulenga
Kumbe mnamjua? Mimi ndiyo namfahamu kwa hizi makala za sasa. Huyu jamaa anapotosha kwa maandishi yanayoelekea kuwa kweli kwa kujisahaulisha kuwa muungano una kero zake ambazo lazima zitatuliwe ili wananchi waufurahie
 
 
Mleta Uzi unajitoa ufahamu sana , ni kwamba una njaa au , ukusikia yule aliyesema tuwe tunaenda na passport Zanzibar,
Mleta uzi anatafuta cheo kwa nguvu njaa inamsumbua.
Ukweli unajulikana kwamba serikali ya tanganyika iliuliwa kuhuni sana na Nyerere baadae kabisa baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kama Zanzibar wanaserikali yao, wana katiba yao, wanavitambulisho vyao kama wanzanzibar.
Maana yake wanautambulisho wao kama taifa la zanzibar.
Nilitembelea nchi flani nikakuta kuna chama cha wanzanzibar wanaoishi katika nchi hiyo.
Serikali ya Tanganyika inabidi irudishwe ili kusawazisha mambo
 
Jamaa ana njaa kali sana halafu ni Babu kabisa
Taifa letu limekuwa nawatu wajinga sana, yani mtu mzima kabisa na akili zake anaamua kujitoa ufahamu kwasababu ya vipande vya halua na tende🚮 takataka kabisa. Hoja ziko wazi kabisa halafu mtu anakuja na vioja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…