Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Hoja unayo but unamumunya mambo. Ukweli utakuweka huru. Uadimu na uadhimu wa Muungano wetu opo wapi? Kwanini Zanzibar ibaki na utawala wake wa ndani na Tanganyika ipoteze utawala wake wa ndani? Na kwanini utambulisho wa Uzanzibar ubaki? watu wanataka mambo yaliyonyooka; Ni ama Serikali moja kama ilivyo makusudio ya vyama vilivyoungana (TANU na ASP)au Serikali tatu (Serikali ya Zanzibar na Tanganyika zikiwa na mamlaka za ndani tu na Serikali kuu ikisimamia masuala yote ya ulinzi, uraia, mambo ya nje n.k). Ni mambo madogo tu yanayokera ktk muundo huu wa Muungano.
 
Zanzibar imebaki na utawala wake wa ndani kwasababu ni the minority. Tanganyika haikufa, bali ni serikali ya Tanganyika ndio imeubeba muungano, hata kule UN, kimefutwa kiti cha Zanzibar tuu, Balozi wa Zanzibar UN akawa rendered jobless, Balozi wa Tanganyika UN, aliendelea, na serikali ya Tanganyika ikajigeuza serikali ya muungano, katiba ya Tanganyika, ikageuzwa katiba ya muungano, Rais wa Tanganyika, akawa rais wa muungano. Kilichotokea ni jina tuu la Tanganyika kugeuka Tanzania, everything else remains the same!, hivyo ni Tanganyika ndio imeendelea kuubeba huu muungano wetu adhimu hadi leo.

Na mwisho hilo la serikali moja, nakuunga mkono, mimi ni muumini wa serikali moja!.
P
 
Berlin conference surveyor aliyechora ramani ya africa ni nani? Tumeshindwa kabisa kubadili mipaka
 
Tunahitaji elimu ya Uraia sisi vitimbakwiri

'' Federation ya Tanzania na Zanzibar ipoje'' ?
 
Mwalimu alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, ni kama kula nyama ya mtu, ukiishakula huwezi kuacha!.
Mwalimu ni binadamu kama mwingine yeyote yeye siyo Mungu kusema kwamba kila anachosema au kukifikiria ndiyo sahihi,yeye anasema kitu kwa utashi wake na uelewa wake.
Huwezi kusema eti kwa vile Watanganyika au Wazanzibar wanaohoji baadhi ya mambo katika huu Muungano ni wabaguzi sijui ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu sijui nini! Sio kweli kwanza Watanganyika na Wazanzibar sio ndugu hivyo ikitokea mmoja kamkataa mwenzie huo sio ubaguzi,Watanganyika na Wazanzibar ni marafiki tu hivyo ikitokea wakashindwa kupatana na wakavunja urafiki wao hapo hakuna ubaguzi wowote.
Tuache tabia ya kumuona Nyerere ndiyo Mungu wetu huko ni kumkufuru muumba wa kweli kama Mungu angetaka Watanganyika na Wazanzibar tuwe ndugu Zanzibar ingekuwa ndani ya Tanganyika kama ilivyo Mafia,Ukerewe na visiwa vingine vilivyojaa ndani ya nchi yetu Tanganyika na tuache kuwa makondoo ya kuja kutawaliwa na Wazanzibar hadi vijijini huko,
Kama Tanganyika na Zanzibar ingekuwa nchi moja basi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania angekuwa na mamlaka hadi kule Zanzibar lakini kwa sasa hana mamlaka yoyote huko Zanzibar.
Muungano gani eti "Sio kila Mtanzania ni Mzanzibar"(Wazanzibar wanalisema sana hili) lakini kila Mtanzania ni Mtanganyika yaani Wazanzibar wao ni Watanzania, Wazanzibar na ni Watanganyika lakini Mtanganyika yeye ni Mtanganyika tu maana hata huo Utanzania wake ni kama haujulikani ndiyo maana leo hii kuna Wazanzibar wanakuja na hoja ya kuwataka Watanganyika waingie kwa pasipoti Zanzibar, sasa hapo kuna udugu?
 
Siku hizi imekuwa slogan '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''
Hapa wanataka kutumia Utanzania katika kupata rasilimali za Tanzania lakini wao si Watanzania kwa imani yao kama alivyokana Mbunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT

Tuta debunk hii hoja, na ukweli ni kwamba hiyo slogan inachochea sana hasira za Watanganyika.
Hakuna sababu ya kupigazana kelele , tunahitaji Tanganyika

Pascal Mayalla anasema tuna '' Federation ya Tanzania na Zanzibar'' bado najiuliza kwasababu hii elimu ya Uraia sinayo kabisa. Kwamba kuna nchi ya Tanzania tofauti na nchi ya Zanzibar zimefanya Federation sijui inaitwaje.
 
Huyo jamaa anajifanya mahiri sana kwa uchambuzi lakini ninachokiona anajitia aibu tu,yeye anamuona Nyerere yupo sahihi kwa kila kitu maana kila siku Nyerere kasema,Nyerere kasema!
 
Pascal Mayalla anasema tuna '' Federation ya Tanzania na Zanzibar'' bado najiuliza kwasababu hii elimu ya Uraia sinayo kabisa. Kwamba kuna nchi ya Tanzania tofauti na nchi ya Zanzibar zimefanya Federation sijui inaitwaje.
Karibu kwenye elimu ya uraia kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, Natumaini umeelimika
P
 
Huyo jamaa anajifanya mahiri sana kwa uchambuzi lakini ninachokiona anajitia aibu tu,yeye anamuona Nyerere yupo sahihi kwa kila kitu maana kila siku Nyerere kasema,Nyerere kasema!
Sijifanyi mahiri, mimi ni mwandishi wa habari kwa miaka zaidi ya 30, na pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, hivyo nina umahiri fulani kwenye baadhi ya maeneo.

Mwalimu Nyerere ni mtu sahihi sana, na kuna vitu vingi Nyerere kasema, nitaendelea kuwaletea Nyerere alichokisema.
P
 
Karibu kwenye elimu ya uraia kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu,
Natumaini umeelimika
P
Hapana sijaelimika kwasababu sijui federation inatoka wapi
Nimeangalia Federal gov zote kuanzia East hadi West hakuna mahali nchi inaungana na jimbo au state

Kwa mfano, hakuna Federation ya USA na California au state yoyote. Kuna Federal gov ya state 50 za Marekani kufanya USA.

Nimeangalia Australia ambayo ni Federal state, sikuona mahali Australia imetengeneza federation na state zake

Orodha inaendelea.

Hii Federation ya Tanzania na Zanzibar inawezekanaje? Hii ndiyo elimu ngumu ninayohitaji,
Hapa tufafanulie sisi wenye vichwa vyepesi, Tanzania ni ipi na inafanyaje federation na Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania. !!!
 
Mwalimu Nyerere ni mtu sahihi sana, na kuna vitu vingi Nyerere kasema, nitaendelea kuwaletea Nyerere alichokisema.
P
Baada ya muda wake wa Urais Nyerere aliulizwa kuna kosa gani anafikiri alitenda akiwa madarakani

Mwl alisema ' Kosa kubwa lilikuwa kuua vyama vya Ushirika'' sasa usahihi unaousema wewe yeye kasema haupo
Pili, Nyerere aliua mfumo wa vyama vingi 1965 na kisha ''kusimamia' kwa remote urejeshwaji wake mwaka 1990
Usahihi upo wapi?

Ni kwamba alikuwa na maono, lakini kama binadamu alikuwa na mapungufu! si kosa ni ubinadamu

Hata hili la mkanganyiko wa Federation ya Tanzania na Zanzibar unalozungumzo ni mapungufu.
Nyerere hakuwahi kukataa uwepo wa Tanganyika ! Watoa elimu ya Uraia wanamsingizia
 
Tunahitaji elimu ya Uraia sisi vitimbakwiri

'' Federation ya Tanzania na Zanzibar ipoje'' ?
Muungano wetu adimu na adhimu ni muungano wa kitaifa na kimataifa. Kimataifa ni muungano wa union ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuunda nchi moja ya JMT.

Lakini kitaifa ndani ya muungano, ni muungano wa federation ya nchi mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar.

Ni very unique duniani kote hakuna muungano kama huu, na kitu kikubwa kumhusu huu muungano wetu adhimu ni dhima ya muungano, ni muungano wa milele, hakuna any legal provisions za kuuvunja muungano!.

Kiukweli kabisa elimu hii ya uraia kuhusu muungano wetu ninayoitoa hapa, itasaidia sana kuwaelimisha wengi kuhusu muungano wetu adimu na adhimu, wakiwemo vitimbakwiri.
P
 
Waache na ujinga wao hao manyumbu.

Just imagine ikiwa Tanganyika Mimi ndio itaniongezea hela?
 
Muungano wetu adimu na adhimu ni muungano wa kitaifa na kimataifa. Kimataifa ni muungano wa union ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuunda nchi moja ya JMT.
Nakubaliana nawe 100%
Lakini kitaifa ndani ya muungano, ni muungano wa federation ya nchi mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar.
Hakuna nchi ya Tanzania Bara, kuna Tanganyika na Zanzibar.
Kama kuna Federation ya Tanganyika na Zanzibar ipo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Iko wapi Serikali ya Tanganyika?

Kumbuka unapokuwa na 'conflict' kati ya state au Province zinazounda Federal gov, msuluhishi ni Federal gov.
Lakini conflict hizo zitahusu mambo yaliyokubaliwa kuwa ni ya Federal gov.

Kukiwa na conflict zinazitwa kero za Wazanzibar (state) ikilalamikia Tanganyika (state) msuluhishi ni Tanzania (Federal gove). Swali kwa Pascal , katika meza ya majadiliano SMZ inawakilishi Zanzibar, iko wapi Serikali inayowakilisha Tanganyika! ili Zanzibar na Tanganyika zikae meza moja chini ya msuluhishi Tanzania?

Ni very unique duniani kote hakuna muungano kama huu, na kitu kikubwa kumhusu huu muungano wetu adhimu ni dhima ya muungano, ni muungano wa milele, hakuna any legal provisions za kuuvunja muungano!.
P

Kwani mkataba wa Muungano wa 1964 ulikuwa legally binding au la?
 
Nimesema nukibahatika kuwa rais Kaz ya Kwanza kufanya Ni kufunja huu muungano ndani ya siku tatu narejesha serekali ya tanganyika
 
Nakubaliana nawe 100%
Hakuna nchi ya Tanzania Bara, kuna Tanganyika na Zanzibar.
Kama kuna Federation ya Tanganyika na Zanzibar ipo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Iko wapi Serikali ya Tanganyika?
Ndio maana nimesema kunahitajika elimu ya uraia kuhusu huu muungano wetu. Muungano wetu ni wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar na kuunda serikali moja ya JMT. Ni kweli hakuna nchi inayoitwa Tanzania Bara, wala Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar, hizi sio nchi, ni sehemu ya JMT. Tanzania Bara ni ile sehemu iliyokuwa Tanganyika, jina la Tanganyika limefutwa na nafasi yake kuchukuliwa na Tanzania Bara.

Muungano wetu ni very unique, Zanzibar ndio yenye utawala wake wa ndani wa SMZ, lakini kwa Tanzania, serikali ya JMT, ni serikali ya muungano ambayo pia imevaa koti ya serikali ya Tanganyika kwa mambo ambayo sio ya muungano.
P.
 
Kwani mkataba wa Muungano wa 1964 ulikuwa legally binding au la?
Kulipaswa kuwe na mkataba wa kimataifa wa muungano ambao ni legally binding, but it's very unfortunately, kitu kilichopo ni zile Articles of Union, ambazo ni hati za muungano, japo zinaitwa mkataba, but in reality sio mkataba, ni just an agreement which is not legally binding kwasababu unapungukiwa na moja ya sifa muhimu za mikataba ya kisheria, inayoitwa "privity to contract" ni kila mkataba wa kisheria lazima uwe na kipengele cha privity kinacho onyesha jinsi ya kuuvunja huo mkataba. Kwenye articles of union, hakuna kipengele cha jinsi ya kuuvunja muungano, hiyo ndio dhima ya muungano ni for life!.

Karibu pande hizi Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano? na hizi Je, wajua kuwa kuna uwezekano Tanzania sio nchi halali Kisheria (De Jure) Bali ni De Factor?! na Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?!. (Ufuatiliaji Muungano Sehemu ya I)
P
 
Huu ndio umuhimu wa elimu hii, muungano wetu adhimu ni very unique kwasababu kwa kimataifa ni muungano wa union ya nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT.

Lakini kitaufa ni muungano wa federation ya nchi mbili, za JMT na Zanzibar. Federal state ni serikali ya JMT, local states ni SMZ na Serikali ya JMT kwa mambo yasiyo ya muungano. Serikali ya JMT imevaa koti la serikali ya Tanganyika kwa mambo yasiyo ya muungano at the same time ndio federal state ya serikali ya muungano kwa mambo ya muungano. Kimataifa muungano wetu ni union ya nchi moja tuu ya JMT na Zanzibar kimataifa sio nchi, ni sehemu ya JMT lakini Kitaifa ni muungano wa federation ya nchi mbili, JMT na Zanzibar. Huu ni muungano very unique duniani na hatuhitaji kufanana na muungano mwingine wowote, tungekuwa ni watu wazuri kwenye international promotion, marketing na branding, tunge i promoti Tanzania kwa kuifanyia branding ya union promotion watu dunia nzima wangemiminika Tanzania kuja kushuhudia muungano wa ajabu wa union on one side and federation on the other side, tunge make millions!.

Sasa jambo kubwa zuri kama hili hatuwezi kuliacha likabezwa na vitimbakwiri, lazima tutokee watu Wazalendo wa kuitetea, tena sasa chini ya rais Mtanzania kutoka upande wa pili, Zanzibar, this is the most opportune moment to solidify the union into one solid government. Tumemshauri Rais Samia kwanza kwa kuuliza Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja? kisha kwa kushauri Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…