Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Hakuna hata mtu ana muda wa kusoma hilo gazeti lako. Ni hivi, hakuna uwezekano wa kutetea muungano huu kwa hoja. Hapa unapoteza muda wako bure. Tumechoka na muungano wenye kero zisizotatulika.
Jambo la kushangaza ni gazeti na Wahariri kutokuwa na muda wa 'fact check''
Hivi unakuwaje na Federation ya Tanzania na Zanzibar?

Yaani ni kama kusema kuna federation ya USA na California! na wamechapa kwenye gazeti!

Halafu anasema baada ya Muungano majina yalibadilishwa. Hana ushahidi ni lini au kwa sheria gani iliyobadili majina hayo.

For the sake of disussion tukubaki tu kwamba kulikuwa na Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Halafu anaendelea kusema Zanzibar ikaendelea kuwepo kwasababu za ''uadhimu na uadimu wa mUUngano''

Ukishasikia maneno hayo ujue hapo ni hoja muflisi, yaani hana namna ya ku defend

Alichokusudia ni kusema Zanzibar ipo, Tanganyika ilikufa lakini hawezi kusema hivyo kwsababu atajifunga.

Alichokifanya ni ku 'insinuate' Bara na Viswiani halafu akairudisha Zanzibar ili mbele ya safari atengeneze Federation yake ya Tanzania na Zanzibar. Hii ndio elimu ya Uraia tunayoambiwa itolewe! nope hakuna elimu hapa watu wanatafuta vipindi tu maisha yaendelee

Lakini mhariri wa gazeti anasikitisha, anawezaje kuacha ubabaishaji! utamalaki
 
Kwa vile Tanganyika ilifutwa na jina la Tanganyika kufutwa, utanganyika nao ukafutika, Watanganyika tunajisabisha kwa Utanzania wetu, lakini kwa vile kwa vile jina la Zanzibar, halikufutwa, na kuna Uzanzibari ukaazi, hivyo baadhi ya Wanzanzibari, wanajinasibisha kwa Uzanzibari wao kama uraia wa Zanzibar, badala ya kujinasibisha na Utanzania wao
Hapa ulisahau kwamba kuna aya uliyosema ''siku za karibuni kumekuwa na ubaguzi''
Ubaguzi wa Wazanzibar ni wa siku nyingi sana kinachotokea sasa hivi ni Watanganyika wamechoshwa

Watanganyika wamechoka kukaa kimyaa wakiwa na zigo la Muungano na kamzigo ka SMZ mgongoni na mkononi.
Swali wanalojiuliza ni kwamba ni kwa 'return gani' . Wanajua hawana cha kupoteza na wala hawana sababu za kuwazuia Wazanzibar kuvunja muungano! Akunyimae kunde kakupunguzia mashuzi
 
Baada ya Muungano, majina ya nchi hizi zote mbili, nchi ya Tanganyika, na nchi ya Zanzibar, yalibadilika na kuwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, hivyo jina la Tanganyika likafutwa, ila jina la Zanzibar, liliendelea kuwepo, kutokana na uadimu na uadhimu wa huu muungano wetu.
Hadi hapa sioni sababu ya kuendelea kusoma Hii hekaya yako. Inawezakana vipi mkubaliane "kufuta" majina ya zamani LAKINI mwingine aendelee na jina lake kwasababu eti kwa sababu ya "uadimu" na "uadhimu" wake? Hauko serious kabisa Ndugu. Kuna hoja za msingi kabisa, zinapaswa kuwa addressed na Sio hili andiko lako.
 
Hakuna hata mtu ana muda wa kusoma hilo gazeti lako. Ni hivi, hakuna uwezekano wa kutetea muungano huu kwa hoja. Hapa unapoteza muda wako bure. Tumechoka na muungano wenye kero zisizotatulika.
Aliandika akiwa amelewa
 
1. Tanganyika haipo nafasi yake imechukuliwa na Tanzania Bara, na Zanzibar japo ipo, ila sio nchi ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye utawala wake wa ndani, lakini hakuna uraia wa Zanzibar, uraia ni mmoja tuu wa Tanzania.
Hiki ndicho nilikieleza, kwamba, Pascal alisema majina yalikufa na kuwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Hakuishia hapo kwa njia za ubabaishaji akarudisha Zanzibar na siyo tena Tanzania Visiwani.

Hapo juu anasema Tanganyika nafasi yake imechukuliwa na '' Nchi mpya ya Tanzania Bara''
Hata katika ububusa tukubaliane kwamba kuna nchi ya Tanzania Bara.
Asichoeleza pascal ni kwamba serikali ya hiyo nchi ya Tanzania Bara ipo wapi?

Kama Tanzania Visiwani iimebaki kuwa Zanzibar, Tanganyika imebadilika kuwa Tanzania Bara, wapi ilipo serikali ya Tanzania Bara? Tunasema hivi kwasababu kukiwa na serikali ya Tanzania Bara na kisha Zanzibar lazima uwe na Serikali ya pamoja ya Tanzania. Na tukikubaliana na pascal kwa kujifanya hatuna akili, Federation itakuwa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar siyo Tanzania na Zanzibar

Ukiangalia mkanganyiko huo halafu ukaambiwa ndio elimu ya Uraia, naomba nisihudhurie au kusoma hata kipande cha elimu hiyo. Hiyo siyo elimu ni ubabaishaji na upotoshaji wa kutumia ''mass' kupata vipindi vya TV.

Hapana! stop exploitation , watu wetu wanahitaji tuwasiaidie si kuwapotosha.
 
Nafikiri mada yako ingejikita kwanini wanasiasa wanatumia hoja ya utanganyika na Zanzibar.
Kasome bandiko #6, ameandika si kwa minajili ya kuamsha fikra au majadiliano. Ni wazi kuna 'kazi' anafanya hasa pale anaposema '' tunawamudu na tutawanyoorosha'' Ni kwasababu hiyo article yake yote imejaa 'fallacy and misleading information'' ili kutimiza azma ya kunyooorosha, si kwa mtazamo wa uwakili au uandishi!
Hoja kuu aliyotumia mwalimu Nyerere kuzima hoja ya G55 mwaka 95 ni kwa sababu wale walikuwa wabunge wa ccm, na sera ya CCM ilikuwa serikali mbili hivyo hoja yao ilikuwa batili kwani ilitakiwa ianzie ndani ya chama.
Nyerere hakukataa Serikali 3, alikataa utaratibu uliotumika bila kupitia chama kwa wakati ule
Kwanini watanganyika wanadai serikali yao?
Sababu kuu ni uvunjanji wa katiba unaofanywa na viongozi wakati CCM ambayo inaunda serikali imejaa kimya.
Hili lilianza na OIC ya Marehemu Mwinyi, kukawa na mambo ya ajabu ajabu kama yanayoendelea kuhusu kuchota rasilimali za Tanganyika, kukiuka katiba n.k. G55 wakasema tunahitaji Tanganyika
Hivi rais wa Zanzibar anapata wapi mamlaka ya kugawa uraia.
Halafu Pascal anasema hii ni nchi moja na Uraia ni wa nchi moja. Ni wapi kikatiba Rais wa SMZ ana uwezo wa kugawa Uraia. Lakini si hilo tu, Rais wa Zanzibar kuna wakati anakuwa '' Deputy Amir Jeshi Mkuu'' wakati huo huo anapigiwa mizinga 21 kama Amir Jeshi Mkuu. Wapi kwenye Federation hilo linatokea
Rais Samia alitumia vigezo vipi kuongeza kiwango cha asilimia ya misaada kwenda Zanzibar .
Siyo ,misaada ni pesa zilizoitwa za kibajeti
Kwanini serikali ya Zanzibar haichangii gharama za kuendesha muungano lakini wakati huo huo wanapata asilimia 2 ya mapato ya muungano, wanapata mapato ya payee ambayo hawachangii hata senti tano.
Kwa mujibu wa Katiba wa CCM wa Zanzibar bw Mbeto kiwango kimeongezwa kutoka 4.5% hadi 9% na Rais SSH.
Kwamba kila kodi ya Mtanganyika kuna kiwango kinakwenda Zanzibar !
Kwanini wazanzibar wanaajiriwa kwenye nafasi zisizo za muungano Kama mkuu wilaya, waziri wa uchukuzi na katibu wake na wameshiriki kuuza bandari za Tanzania bila kuzigusa za Zanzibar.
Ni kwasababu wana nafasi 21% na hizo hazitoshi wao katika mambo ya Muungano. Siku hizi RAS , DC Wakurugenzi wa Tanganyika ni Wazanzibar ! kule Zanzibar huwezi kuingiza hata kipande cha ndizi achilia mbali ajira
Time ya Nyalari, tume ya jaji Kissanga na tume ya Warioba zote zilipendekeza serikali tatu nao walikuwa wajinga.
Pascal Mayalla anawaita hawa wazee Vitimbakwiri
Kwanini Tanganyika ndio ibebe gharama ya muungano zaidi wakati Zanzibar ndio wanufaika wakubwa.
Hili nalo ni neno na jambo la kujiuliza, ni kwa faida ipi
Zanzibar waliondoka kinyemela swala la gesi na mafuta kinyemela baada ya kuhisi wao Wana vitu hivyo na uongozi wa rais wa muungano atakuwa mtanganyoka Ila tumeona Samia mkataba wake wa kwanza akiwa rais wa muungano ulikuwa wa gesi kwenda Kenya.
Siyo hilo tu kuna video ya Mzee Warioba akiongea na Buholela wa ITV, alishangaa na kuuliza jinsi mambo yalivyoondolewa na Zanzibar ! Yaliyobaki ni Tanzania a.k.a shamba la bili
Ni swala la muda serikali ya Tanganyika kurudi ndio maana jaji Warioba alisema ni heri watanganyika wakapewa serikali yao kabla ya kuidai.
Na kama hawatarudisha, Muungano utafikia hatma katika muda mrefu

Hizi mbinu za kutuma watu wapotoshe Federation ya Tanzania na Zanzibar hazitafanikiwa
 
Kwamba hiyo elimu ya uraia uliipata wewe peke yako kutoka mbinguni na ukaielewa kwelikweli?Unazeeka vibaya aisee!Unaiishi dunia ya medieval ages.Unawachagulia watu kitu wasichokitaka au mfanane mawazo kivipi?Jikite kwenye kueleza faida zake.Labda,labda visokorokwinyo na vizabizabina wako watakuelewa.Kwani wewe unakufaidisha nini huo muungano?Au upate sifa tu kwamba.."tumemuona Pascal Njaa anautetea muungano hasa"...!🤣🤣🤣
TUPIGE KURA tuulizwe,kama uendelee au tuachane nao,,Hilo nalo mtakataa
 
Magufuli alimsoma siku nyingi huyu mtu na kusema Mayala mtu ni njaa kwa mtu mwenye akili huhitaji nguvu nyingi hata kuliona hili na kumpuudha hoja zake ila historia itamuhukumu siku moja kwa haya anayoandika.

Ki ukweli Muungano ni mzuri ila kuna mapungufu tu address mapungufu tutafute solution tuende mbele sio kuuvunja hilo hapana halikubaliki.

Mayala wewe ni wakili naomba jibu la hili swali Kati ya katiba ya Muungano na ya Zanzibar ni katiba ipi ipo juu ya mwenzake ukijibu hili nitakuuliza swali la pili...
 
Magufuli alimsoma siku nyingi huyu mtu na kusema Mayala mtu ni njaa kwa mtu mwenye akili huhitaji nguvu nyingi hata kuliona hili na kumpuudha hoja zake ila historia itamuhukumu siku moja kwa haya anayoandika.
Ki ukweli Muungano ni mzuri ila kuna mapungufu tu address mapungufu tutafute solution tuende mbele sio kuuvunja hilo hapana halikubaliki.
Mayala wewe ni wakili naomba jibu la hili swali Kati ya katiba ya Muungano na ya Zanzibar ni katiba ipi ipo juu ya mwenzake ukijibu hili nitakuuliza swali la pili...
Hawezi kuwa na jibu la maana, atuambie mtanganyika ananufaika vipi na huu muungano?
 
Dhumuni la Muungano kwa mawazo ya mwalimu Nyerere ilikuwa ni kujenga nchi moja ambayo ni JMT ( Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania), na ndio mana serikali ya Tanganyika ikajisalimisha kwenye serikali ya JMT mapema sana ila shida imekuwa kwa Hawa ndugu zetu wazanzibar, hawa wanataka kujitenga na JMT, mana mpaka Sasa wanakatiba yao, Wana rais wao, wana mamlaka yao ya mapato , na sisi bara tuna ya kwetu ambayo ni TRA ,
Hii TRA sio Tanzania revenue authority ila ni Tanganyika revenue authority, ndo mana ukinunua bidhaa zenji ukiingia nayo bara unakatwa Kodi,
mana JMT na SMZ sio nchi moja,
Wazanzibar Wana vitambulisho vyao vya uzanzibar.
Lissu, Mbowe wako sawa tuwaunge mkono kuidai Tanganyika yetu
Ni mjinga pekee anaweza kudhani tuna muungano huku watanganyika tunanyonywa
 
Nafikiri mada yako ingejikita kwanini wanasiasa wanatumia hoja ya utanganyika na Zanzibar.
Hoja kuu aliyotumia mwalimu Nyerere kuzima hoja ya G55 mwaka 95 ni kwa sababu wale walikuwa wabunge wa ccm, na sera ya CCM ilikuwa serikali mbili hivyo hoja yao ilikuwa batili kwani ilitakiwa ianzie ndani ya chama.
Kwanini watanganyika wanadai serikali yao?
Sababu kuu ni uvunjanji wa katiba unaofanywa na viongozi wakati CCM ambayo inaunda serikali imejaa kimya.
Hivi rais wa Zanzibar anapata wapi mamlaka ya kugawa uraia.
Rais Samia alitumia vigezo vipi kuongeza kiwango cha asilimia ya misaada kwenda Zanzibar .
Kwanini serikali ya Zanzibar haichangii gharama za kuendesha muungano lakini wakati huo huo wanapata asilimia 2 ya mapato ya muungano, wanapata mapato ya payee ambayo hawachangii hata senti tano.
Kwanini wazanzibar wanaajiriwa kwenye nafasi zisizo za muungano Kama mkuu wilaya, waziri wa uchukuzi na katibu wake na wameshiriki kuuza bandari za Tanzania bila kuzigusa za Zanzibar.
Time ya Nyalari, tume ya jaji Kissanga na tume ya Warioba zote zilipendekeza serikali tatu nao walikuwa wajinga.
Kwanini Tanganyika ndio ibebe gharama ya muungano zaidi wakati Zanzibar ndio wanufaika wakubwa.
Zanzibar waliondoka kinyemela swala la gesi na mafuta kinyemela baada ya kuhisi wao Wana vitu hivyo na uongozi wa rais wa muungano atakuwa mtanganyoka Ila tumeona Samia mkataba wake wa kwanza akiwa rais wa muungano ulikuwa wa gesi kwenda Kenya.
Ni swala la muda serikali ya Tanganyika kurudi ndio maana jaji Warioba alisema ni heri watanganyika wakapewa serikali yao kabla ya kuidai.
Ni mjinga pekee ambaye hadai Tangayika huku tukinyonywa na Zanzibar
 
ni muhimu zaidi kuwatoa ujinga vitimbakwiri hawa. Kuacha kufanya hivyo ni kuwatelekeza, jambo ambalo si zuri, watazaliana na ujinga wa kibaguzi kudai kitu kisichokuepo utaongezeka zaidi 🐒
Unaandika kama aliyepata ajira wakati wa samia
 
Ntarudi kuchangia maana ndo natoka hapa arusha the hub lounge .Ukweli kuna mzanzibar nilikutana nae last week zanzibar nina kitu alinieleza ntashare.mada za msingi kama hizi sio za kuchangia na hangover.
 
Wanabodi

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na kwa Maslahi ya Taifa, kila Jumatano kwenye gazeti la Mwananchi na Jumapili kwenye gazeti la Nipashe na kwenye kipindi cha KMT on Channel Ten TV, kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku na marudio Jumatano saa 9:30 alasiri.

Hoja ya leo ni hoja za Utanganyika na Uzanzibari ambazo ni hoja muflis zinazosababishwa watu wanaitwa vitimbakwiri kujivunia uraia ambao haupo kutokana na ujinga tuu wa ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu uraia wa Tanzania. Kwenye uraia, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, tuna uraia mmoja tuu, Mtanzania. Swali ni jee tuwatoe ujinga hawa vitimbakwiri muflis wanaotaka kutubagua kwa Utanganyika na Uzanzibari kwa kuwaelimisha elimu ya uraia, au tuwaache tuu na ujinga wao kujisikia sifa kujinasibisha na kujivunia Utanganyika na Uzanzibari?.

Hili ni Nipashe la Leo.
View attachment 2994081

Ukosefu wa Elimu ya Uraia Kuhusu Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, ndio umesababisha, huu ubaguzi wa Utanganyika, na Uzanzibari, watu wakielimishwa kuhusu uraia, hawa vitimbakwiri muflis wanaoleta ujinga wa ubaguzi wa kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, ujinga huu utawatoka, wataerevuka na tutakuwa na Utanzania pekee!.

Hivi karibuni, kumeibuka hoja za kibaguzi za baadhi ya wanasiasa, kutoa kauli za kibaguzi za kuwanyooshea watu vidole na kuwaita “Wao Wazanzibari”, “Sisi Watanganyika”. Miongozi mwa watu wanaotoa kauli hizo ni baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, waliofilisika kisiasa, na baadhi ya wanaolaani kauli hizo, ni baadhi ya viongozi wa chama tawala, ambapo nimemsikia mmoja wa viongozi hao, akilaani vikali kauli hizo bungeni kwa maneno makali kabisa!, huko pia ni kufilisika kisiasa.

NB. Aliyesema wanasiasa wanaojinasibisha na Utanganyika na Uzanzibari, dini zao, kanda zao, au kabila zao, ni watu muflis, waliofilisika kisiasa, sio mimi ni Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na akaiandikia kitabu kinaitwa “Nyufa”. Mwalimu alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, ni kama kula nyama ya mtu, ukiishakula huwezi kuacha!.

Uraia ni hoja ya kikatiba na kisheria. Kabla ya Muungano, tulikuwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, hivyo tulikuwa na uraia wa Tanganyika, na uraia wa Zanzibar. Baada ya muungano, tukaungana kuwa nchi moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwa na uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania.

Baada ya Muungano, majina ya nchi hizi zote mbili, nchi ya Tanganyika, na nchi ya Zanzibar, yalibadilika na kuwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, hivyo jina la Tanganyika likafutwa, ila jina la Zanzibar, liliendelea kuwepo, kutokana na uadimu na uadhimu wa huu muungano wetu.

Uadimu wa Muungano
Miungano ya nchi zote duniani ni miungano ya aina mbili kuu,

1. Muungano wa Union, ambapo nchi mbili zinaungana na kuunda nchi moja. Zile nchi zote mbili zilizoungana , zote zinakufa na kuunda nchi moja mpya. Hivyo ndivyo ulivyo muungano wetu kimataifa, ni muungano wa Unioni, ile nchi ya Tanganyika imekufa, ile nchi ya Zanzibar imekufa, imezaliwa nchi moja mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye urais mmoja tuu, uraia wa Tanzania. Hakuna tena uraia wa Tanganyika, wala uraia wa Zanzibar, kuna uraia mmoja wa Tanzania. Tanganyika haipo nafasi yake imechukuliwa na Tanzania Bara, na Zanzibar japo ipo, ila sio nchi ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye utawala wake wa ndani, lakini hakuna uraia wa Zanzibar, uraia ni mmoja tuu wa Tanzania.

2. Muungano wa Federation, ni nchi mbili au zaidi, zinaungano kuwa nchi moja, lakini zile nchi zote mbili zinaendelea kuwa utawala wake wa ndani, na serikali zao, chini ya utawala mkuu wan chi ya federal state, kama Marekani. Vivyo hivyo muungano wetu kwa ndani ya muungano ni muungano wa federation yenye nchi mbili, Tanzania na Zanzibar, yenye marais wawili, Rais wa JMT “mwenye R kubwa, na rais wa Zanzibar mwenye r ndogo, zenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya SMZ, mabunge mawili, Bunge la JMT na BLW, na zenye mahakama mbili, Mahakama ya JMT na Mahakama ya Zanzibar, ila kwenye uraia, bado ni uraia mmoja tuu wa JMT, ila kwa Zanziar, wana ukaazi, ule ukaazi sio uraia ni utambulisho tuu wa wakaazi wa Zanzibar lakini wote ni Watanzania.

Hivyo muungano wa Tanzania ni muungano adimu pekee duniani ambao kwa upande mmoja ni muungano wa union na upande wa pili ni muungano wa federation, hakuna muungano wa aina hii popote duniani.

Uadhimu wa Muungano.
Muungano wetu licha ya kuwa ni muungano adimu, pia ni muungano adhimu, wenye dhima ya kuungana milele!. Miungano yote duniani unaundwa kwa mikataba ya kisheria ya muungano. Mikataba hiyo inakuwa na kipengele cha jinsi ya kuivunja miungano hiyo. Kwenye zile Articles of Union za Muungano wetu, hakuna kipengele cha jinsi ya kuuvunja, muungano, hivyo zile Hati za Muungano sio mkataba wa muungano, ni makubaliano ya muungano, (not a contract, but an agreement) yenye dhima ya muungano wa milele, na ndio maana tunasema “muungano tutaulinda kwa gharama yoyote”.

Tangu tumeungana, na mimi tangu nimezaliwa na kupata akili, sikumbuki hata mara moja, kusikia vipindi vya elimu ya uraia kuhuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, hali inayopelekea Baadhi ya Watanzania kuanza kujinasibisha na Utanganyika wao, na Uzanzibari wao.

Kwa vile Tanganyika ilifutwa na jina la Tanganyika kufutwa, utanganyika nao ukafutika, Watanganyika tunajisabisha kwa Utanzania wetu, lakini kwa vile kwa vile jina la Zanzibar, halikufutwa, na kuna Uzanzibari ukaazi, hivyo baadhi ya Wanzanzibari, wanajinasibisha kwa Uzanzibari wao kama uraia wa Zanzibar, badala ya kujinasibisha na Utanzania wao, kungekuwa na vipindi vya elimu ya uraia kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu, kusingekuwepo, vitimbakwiri wowote, wanaojinasibisha kwa Utanganyika wao, au Uzanzibari wao kwasababu, uraia wa JMT ni uraia mmoja tuu, hakuna uraia wa Tanganyika, wala hakuna urais wa Zanzibar, kuna uraia mmoja tuu, uraia wa JMT.

Wiki ijayo, nitaendelea na kuwaletea hizi chokochoko za kuuchokoa muungano na kuanza kunyoosheasha vidole vya ubaguzi wa “Utanganyika na Uzanzibari” zilianzia wapi, dawa yake ni nini na tiba ya kudumu ya kuitibu sumu hii na kuiangamiza kabisa.

View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=fPhb1_0doZmgD7T4
Wakati huo huo, naendelea na darasa langu la elimu ya uraia kuhusu katiba, sheria na haki on Channel Ten kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Karibuni.

Paskali

mi swali langu ni kama Tanganyika ilifutwa kwanini zanzibar haikufutwa ili ibaki Tanzania? na kwanini kuwe na zanzibar ukaaz na hakuna tanganyika ukaaz? kwanini zanzibar wana katiba wana rais ambayo ni serikali kamili lakini tanganyika haipo? kwann mzanzibar anaruhusiwa kumiliki ardhi tanganyika lkn mtanganyika haruhusiwi kumiki ardhi? kama zanziba wana serikali yao kwanini tanganyika haina serikali yake?? naomba na mimi nitoe ujing ili nielewee urai vzr
 
Unaandika kama aliyepata ajira wakati wa samia
jambo la muhimu na maana zaidi ni kufuatilia vipindi na makala vya masula ya uraia na sheria ambavyo muungwana comrade Pascal Mayalla anakusudia kuitoa for free to the paplics....

hii ingine,
ya ajira si jui ya nani ilikua lini, ni mihemko tu ya kawaida out of point. Tafadhali usikate tamaa, hapana kususa wala kuzira katika kutafuta ufahamu na uelewa zaidi juu ya mambo haya muhimu zaidi kwa maslahi mapana kwa usalama, umoja na mshikamano wetu kama Taifa 🐒
Twende pamoja bila mihemko.....
 
Back
Top Bottom