Hoja za Waitara - Je, CHADEMA watajibu?

Well said,congrats!
 
Hebu tukubushane pale kiongozi wa juu nchini alipo ulizwa analipa kodi kama wananchi wengine jibu lake lilitoka mpaka leo? Huwezi kumfananisha Waitara na hio list ulio itaja hivyo vichwa vikubwa.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hivi mlevi huyu alikuwa na ubavu wa kufanya kampeni kwa hela ipi,hata kujaza mafuta gari kuzunguka jimboni angeweza?
Hata perfume kupiga wanajifunzia cdm wameingia mikono mitupu wamevuna mamilioni kwamba hata wangekuwa wameajiriwa wasiyeyapata.
Thus tunataka ubunge iwe kazi ya wito Kama zingine ili tupate watu wenye uchungu na Jamii.
Mbunge anapewa maslai yote hayo ya nn kwa kazi ipi aliyofanya kwann usiwe ni kazi ya wito
 
Tw
Two wrongs don’t make it right. Usitafute uovu mmoja ili kutumia kutetea uovu mwingine.
 
Mkuu,ukiona mwehu anakimbia uchi barabarani anakutaka ujiunge utakubali kisa umetakiwa kufanya hivyo?
Kwahiyo kwako hizo tuhuma za kwenye chama cha umma ni sawa mwehu kukutaka mkakimbie naye uchi? Mbona kama mnatumia michezo ya mbuni kujificha kichwa wakati mwili uko nje.
 
Kwahiyo kwako hizo tuhuma za kwenye chama cha umma ni sawa mwehu kukutaka mkakimbie naye uchi? Mbona kama mnatumia michezo ya mbuni kujificha kichwa wakati mwili uko nje.
Unajua tuhuma na nini kinatakiwa kuziondoa? Si kila tuhuma ni ya kufanyiwa kazi.Mkeo akikuchoka na kukutangaza kuwa ni "mwanamke" utachukua hatua zipi kudhihirisha kuwa ni mwongo? Si kila jiwe likirushwa ujibu,unaweza kuwa unaishi nyumba ya vioo!
 
Kwa chadema hii ni ngumi ya pumbu, wanajikaza tu Ila tumbo lazima liume, wakubali wakatae hii press Ni pigo kwao tena heavy.
Na wakimjibu ndio wataharibu zaidi Mana jamaa anaonekana ana mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwamba hawataki kujibu hawajui kama kuna watu wanapiga pesa
 
Unajua tuhuma na nini kinatakiwa kuziondoa? Si kila tuhuma ni ya kufanyiwa kazi.Mkeo akikuchoka na kukutangaza kuwa ni "mwanamke" utachukua hatua zipi kudhihirisha kuwa ni mwongo? Si kila jiwe likirushwa ujibu,unaweza kuwa unaishi nyumba ya vioo!
Tuhuma tumezisikia, mapokeo ya wahusika yameonekana na watu wazima tumeelewa. Wacha tuendelee kutakasa mikono kwa sabuni na maji tiririka.
 
Aisee Waitara kamaliza kila kitu sidhani kama chadema watajibu hizo hoja

Hoja za Lijuakali ukijumlisha na hizi za Waitara zinashawishi kuonyesha kuwa huko CHADEMA kuna matatizo makubwa ya matumizi ya pesa.

Hivyo ni muhimu kwa CHADEMA kujibu hizi hoja kwa ushahidi wa stakabadhi, juu ya matumizi ya pesa wanazopata toka vyanzo mbalimbali.

Wasi wasi wangu mkubwa si matatizo yanayotokea katika hicho chama, bali ni pale kitapofanikiwa kuingia madarakani na kuiharibu nchi kwa kuifilisi mpaka kile kidogo kunachorambaramba. Kimsingi kimefanikiwa kuwashawishi kiasi kikubwa cha watanzania kuamini kuwa CHADEMA ndio chama mbadala. Hivyo kama watanzania tukateleza na kuwachagua wasije wakatuharibia nchi.

Cha msingi ni kwa wale viongozi waliochadema kuunda timu na kuyasema hayo wakiwa ndani ya CHADEMA. Wanapoyasema nje ya chadema, hayana uzito sana uzito kwani tulio nje tunafikiri kuwa kwa vile mmefukuzwa ndio mnalipiza kisasi.

Kinachonishangaza ni kimoja tu, yaani kwa makosa yote mnayoyaeleza mnashindwa kuunda umoja ndani ya CHADEMA utaofanya mapinduzi humo ndani bila ya kungoja kutoka nje. Hilo litakuwa jambo jema sana hasa kwa waliobaki CHADEMA, vinginevyo ni vigumu sana kuaminika. Na kwa udhaifu huo yawezekana ndio huyo Mwamba anawashinda kirahisi sana. COME ON!!!!!!
 
Hili zee ni la njaa vibaya mno....

Haya ndiyo kati ya mazee yatakayopata wakati mgumu sana
ndani ya CCM wakati baba yao akishandolewa uwenyekiti....

Yaani jitu linapita bila kura za maoni afu wafia chama mpo mnachekacheka tu...wakati. chama chetu kinadhalilishwa majukwaani na hawa jamaa hamkusikia??

Leo wanakuja CCM na vyeo juu wanapewa..ina maana sisi wafia chama hatufai siyo!!
 
Vyama vingi vyenye ushawishi mkubwa kama NCCR na CUF vilifuatiliwa kwa propaganda na kupandikizwa wasaliti mpaka baadaye vikafa ama kupunguzwa nguvu. Inaweza kuwa ni kweli kuwa Mbowe ana mapungufu yake lakini ushawishi mkubwa wa kiasiasa alionao kwa wanachama na wananchi wengine unawapa kazi sana ccm namna ya kumwondoa ili kufanikisha lengo kama lililofanywa kwa vyama vingine ili ccm isiwe na upinzani mkubwa.

Kwa maoni yangu naona Mbowe akiondoka au kuondolewa uenyekiti basi CHADEMA nacho kitafuata nyayo za NCCR na CUF kwani imagine watu hao wanao hama ndiyo wangekuwa wenyeviti. Chama nafikiri kina waanzilishi wenye uchungu navyo na pengine wale ambao wana affiliation na waasisi wanaweza kuwa na uchungu na chama kuliko wengine ambao pengine malengo yao hayaeleweki na yanaweza kuyumbishwa na ushawishi wa kifedha ambapo wanaweza hata kutumiwa kuua chama.

Mzee Mbowe kama yasemwayo ni kweli pengine kuna haja ya kujirekebisha na kuruhusu demokrasia ishamiri. Mifumo pia ya kiutawala iwe wazi ikiwemo ya manunuzi ambayo ina ushawishi mkubwa wa kifedha. Nafikiri pia Chadema inatakiwa kuwa na Kamati ya Tenda pamoja na mtaalam wa ununuzi ambaye anatakiwa atumie kanuni za wazi za ununuzi (Best practices).
 
Umewahi kumsikia magufuli anazungumzia matrilioni ya ununuzi wa ndege na ujenzi wa airport chato na upotevu wa zile 1.5tn?.......
Tuanzie hapo kwanza kwa maslahi ya taifa
 
Kuna pia hoja za Wabunge wawili wanawake, pamoja na madai ya matumizi mabaya ya fedha, kuna rushwa ya ngono. Mh Mbowe atumie busara kuweka wazi matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kupitia Baraza Kuu la chama, kabla ya kuanza mchakato wa kuteua wagombea wa chama kwenye Uchaguzi Mkuu. Asipofanya hivyo atawapa mtihani wagombea hao kujibu tuhuma dhidi yake, wakati wa kampeni. Hakuna shaka wagombea wa upinzani watabeba tuhuma dhidi ya Mbowe kama agenda.
 
Mimi sishangai, nilishasema muda mrefu Mbowe ni msanii!
Najua kwa akili yake ndogo anafikiri akilipa vijana watukane JF na kumtukuza yeye basi atapata uraisi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…