Hoja za Waitara - Je, CHADEMA watajibu?

Kama kuna mtu atakua amekuelewa ulichoandika hapa atakua na kipaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupunguze ulimbukeni na likes, tafuta mada za Fahami Matsawili zote ni nzito za kujadili mustakabali wa taifa mfano sera ya elimu, sera ya uwekezaji lakini hutoona comment wala like hta moja then urudi hapa kusema HOJA ndio huzaa likes. Trust me unaweza andika mada kusifia miradi ya awamu ya tano ila comment ya kwanza ikiwa "kachukue buku 7" hapo utakuta likes hadi 100. Nachosema ni JF ya sasa imejaa ushabiki sio kujibu hoja, ndio maana wewe ukaishia kunikejeli tu badala ujibu hayo maswali yangu.

1. Nmekwambia kuthibitisha sijaona hta uki upload hapa Financial statement ya CHADEMA ila umerudi na porojo kma waitara.

2. CAG kupitia NAO hakagui tu financial reports bali hadi procurement procedures, anakagua mali za chama pia, pamoja na madeni!! Sasa akifika kwenye deni atauliza hii 50M hapa ya Mbowe evidence yake ikwapi? Alikopesha lini kwa wiring ipi? Kma hamna document hapo anaweka querry hivyo haiwezi kuwa hati safi tena.

3. Issue hapa sio kelele za Mwigamba au Zitto, obvious kwa siasa za TZ kila anayehama lazima atoe tuhuma lakini shida uthibitisho. Sasa waitara ni waziri kwanini asitumie hayo mamlaka kuamuru Mbowe akaguliwe hadi akaunti binafsi ili mambo yawe wazi? Kwanini hajaleta financial statements za chama ama biashara za Mbowe ili atafute huo wizi wake?

Issu sio Mbowe kuiba ama lah issue ni FACTS, kma hamna mie siwezi kuamini. Huyo waitara kma alishajua Mbowe mwizi kwanini aligombea kupitia CHADEMA toka 2010? Hawa wanasiasa wapo kimaslahi tu mkuu sio kupinga ufisadi wa Mbowe.
 
With due respect, naona kuna tatizo kubwa pahala. Waziri anapata wapi muda wa kumshambulia mtu badala ya kudeal na mambo ya wizara yake ambayo ina changamoto lukuki.

Watanzania tuna tatizo kubwa sana kwenye bongo zetu, kwa namna hii hatutaenda kokote. Waziri kabisa kabisa anatumia muda wetu walipa kodi kijinga nmna hii? Imenikerehesha sana.

Nimeanza kukubaliana na kauli za prof. Watson juu yetu watu weusi. Waziri wetu anatuhutubia ujinga huu bila hata soni, waziri kabisa? Badala ya kuja na mambo ya sera na utekelezaji anatuhutubia mambo ya Mbowe?

Hati chafu au safi za CCM na CHADEMA hazina manufaa kwetu. Pengine abadilishiwe nafasi apelekwe kwenye uongozi wa chama.

Waziri kabisa kabisa hapo na wewe uñajiona mchapakazi? Watanzania tujitafakarini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi ushawahi kuona mtu mwenye akili timamu anajibizana na chizi ?...!!
 
Mkuu, hata Ile kunyanyua mdomo wako kusema mambo ya jambazi sugu ni ujasiri uliopitiliza, Kwa Maana ni kujitoa mganga wewe mwenyewe
 
Mkuu, hata Ile kunyanyua mdomo wako kusema mambo ya jambazi sugu ni ujasiri uliopitiliza, Kwa Maana ni kujitoa mganga wewe mwenyewe
Ukiwa serikali huwezi ogopa jambazi sugu sababu unaweza amrisha hta JWTZ nzima imsake ila ukiwa huna jeshi kma wapinzani ndio lazima uogope kumsema "jambazi" sababu atakutumia wasiojulikana na wewe huna JESHI la kukulinda.

Sasa ikitokea waziri aogope jambazi nani sasa atakua mjasiri kuanika uhalifu?
 
Count down has started to the October elections, less than 150 days.
 
Mkuu zitto junior, hakika wewe na wanaokupa "likes" mmeamua, bila kupepesa macho na kumng'unya maneno, kutetea uovu unaofanywa na Mbowe na genge lake. Wanao mshutumu Mbowe ni viongozi wenzake waliokihama chama kwa sababu ya udhaifu wake kiuongozi. Je, hata huyu naye utamkosoa kwa lipi?

 
Mbowe na Chadema hawana muda mchafu kujibizana na mataahira ya CCM yaliyolewa mataputapu.
 
Ole Medeye alikua CCM maisha yake yote ni lini amekua kiongozi wa CHADEMA?

Anadai cjui aliahidiwa kiti CC, je anaweza prove hayo madai? Hana Copy ya MoU? Eti yye ndio alikua anakidhamini chama wakienda mikoani?

Unajua kutoa tuhuma ni rahisi ila kuthibitisha ndio mtihani.

Ssa kituko watu hamfuatilii mnachukua maneno kma yalivyo then tunajiita great thinkers

Mbowe angekua fisadi kma mnavyompaka hapa CCM wangeshampa kesi ya uhujumu uchumi kitambo tu
 

Hakuna anaye mpaka Mbowe tuhuma. Tuhuma zinazosemwa dhidi yake na genge lake ni nzito na zinatolewa na viongozi waliokuwa naye CHADEMA.

Maisha ya Ole Medeye CHADEMA amesimulia nwenyewe, kwenye hiyo video, akhojiwa maswali mazito, siyo yangu.

Wanaotoa tuhuma naamini wanao ushahidi, la, watuhumiwa wangekuwa au wanaweza kuwachukulia hatua. Ukimya wao ni dhahiri wamekubali tuhuma. Usiwasemee ya moyoni mwao.

Siwezi kufuatilia tuhuma ambazo hazikuelekezwa kwangu. Anayechafuliwa huwajibika kujisafisha.

CCM ni chama cha Siasa, kama CHADEMA, hivyo basi, kinashughulika kulinda na kutetea Katiba yake.

Tuhuma za ufisadi wa mali ya umma, km ruzuku, TAKUKURU imekwishaanza mchakato. Kuna tetesi ya Mbowe kuingia mini kujaribu kuharibu ushahidi. Chonde chonde, ninyi watetezi wake, msije kung'aka tena, ushahidi ukipatikana akapelekwa mahakamani kujibu tuhuma.
 
Huu ni unafiki wa wanasiasa wa TZ, kwanini walipokua CHADEMA hawakusema au angalau wangeiba taarifa wapelekee polisi ili wamkamate Mbowe? Kukaa kimya huku pesa zinaibwa miaka yote ina maana na ww ulikua mnufaika.

At least Zitto yeye alipambana hesabu zao zikaguliwe akiwa bado CHADEMA ila hawa wengine wakitoka ndio matusi bila ushahidi.

Mkuu mie nikwambie tu maadam haya wanayosema CAG hajawahi thibitisha itabaki ni kelele tu. Ilipaswa waje na nyaraka maana si wapo serikalini hawawezi nyimwa.

Mfano wanaposema Mbowe anajilipa madeni, basi wangekuja na financial statement za CHADEMA kuonyesha kweli Mbowe huwa anaidai CHADEMA mbona simple tu ingemuumbua asubuhi tu.

Shida mnakuja na maneno wakati ni serikali, bora hao TAKUKURU wafanye uchunguzi I hope watakuja na data za kueleweka kuliko hizi kelele bila nyaraka. Hazisadii kitu.

GT hupaswi kuamini maneno bila ushahidi, nakumbuka tuliambiwa CHADEMA wanalipwa na wazungu kumdhoofisha Magufuli ila mbona wakienda CCM wanapokelewa na kupewa uwaziri? Leo Mbowe akienda CCM na kupewa uwaziri utaweka wapi sura yako mkuu? Usikubali kupotoshwa na wanasiasa fanya tafiti zako binafsi.
 

Nakubaliana na wewe huenda zikawa porojo za kisiasa kama hizo za viongozi wa upinzani, wanachama na wafuasi wao, wanazozipaza kwa viongozi wa CCM na Serikali yake.

Kwa kuwa tunaelekea Uchaguzi Mkuu, tuhuma hizi zikipuuzwa, zitatumiwa na wapinzani wa CHADEMA. Athari zake ni kwa wagombea wa CHADEMA kutumia muda mwingi wa kampeni kumsafisha Mbowe, na chama chake kwa ujumla, badala ya kunadi sera za chama.

Isitoshe msimamo na mtazamo wa viongozi wa CHADEMA kuhusu masuala mazito ya kitaifa km ujenzi wa miundo mbinu, moja ya nguzo za kukuza uchumi na uboreshaji wa huduma za jamii, kukejeli kuwa ni maendeleo ya vitu, pia ni chsngamoto kwa wagombea kutetea hoja ya chama kuwa maendeleo ya watu ni demokrasia.

Kwamba, viongozi wa CHADEMA, kwa vitendo walijifungia kama njia sahihi ya kudhibiti maambukizi ya COVID-19, pia itawapa shida kujitetea. Km iwapo Jeshi la Polisi, ambalo naafisa wake hukabiliana na jamii kila mara, lingamua nao wajifungie siku 14, usalama wa raia na mali zao ungekuwaje?

Kwa hiyo, Mkuu zitto junior, usichukulie shutuma hizo kama unafiki wa wanasiasa wa TZ. Hakika viongozi wa CHADEMA wanakabiliwa na mengi ya kujibu ikiwa ni pamoja na fedha za ruzuku kutokujenga hata ofisi moja ya chama, kama ukumbusho. Kumbuka awamu hii ya utawala wa nchi hii, chama kilipata wabunge wengi na kuongoza halmashauri za miji mikubwa nchini, hivyo kuwa na uwezo mkubwa kifedha na donge nono la ruzuku. Kama viongozi wake wameshindwa kufanya hivyo, kamwe chama kitakuwa na ofisi hata ya chumba kimoja.

Tunahitaji vyama vya siasa vyenye viongozi wenye kubeba dhamana ya wanachama kwa maendeleo yao na ya mama Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…