Holiday season imewadia, wazee wa safari ndefu huu ndiyo mwezi wetu wa kumwaga moto

Holiday season imewadia, wazee wa safari ndefu huu ndiyo mwezi wetu wa kumwaga moto

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
10,786
Reaction score
35,916
Wakuu..

Katika kipindi hiki cha mwezi December watanzania wengi wanakuwa katika hekaheka za kusafiri sehemu tofauti wakifurahia maisha baada ya miezi 11 ya purukushani za kutafuta riziki.

Wewe mwana-jamiiforum umejiandaaje na safari za mwisho wa mwaka? Mimi nilijiandaa Toka mwezi January nikijichanga pesa Fulani ili niweze kusafiri mwezi (Hii tunafanya Sisi wenye kipato cha kuungaunga).

Kwa wale wazee wa kumwaga moto barabarani huu ndiyo msimu wa kuacha papara barabarani kuliko kipindi kingine barabarani kumbuka kipindi hiki madereva wazembe wanakuwa wengi Sana barabarani huku wengine wakiendesha Kwa mashindano.
Nimeona vijana wengi hapa kariakoo wasio wazoefu na barabara wanataka kufanya safari kipindi hiki, tunawasihi Tu Huko barabarani kuheshimu Sheria Tu

Madereva wanaotumia masaaa 5 kutoka DAR -DODOMA watakuwa wengi Sana barabarani.
Kila la kheri madereva wenzangu
 
20241022_205441.jpg
 
Mkuu ilitakiws utume picha za ajali ili kuwaamsha akili vijana wapya walionunua magari nakufanya safari za mara ya kwanza kwenye highways! Hao ndio madereva hatari sana kipindi hiki cha sikukuu.

Kama tu vile wanavyo piga picha ya mapafu yaliyoharibiwa na cancer kwenye pakti za sigara.

Picha yako hii ya mkeka kwenye katafunua za mwidu! Zinawashawishi vijana kkuona speed ya 150 inawezekana kirahisi nchini
 
Mkuu ilitakiws utume picha za ajali ili kuwaamsha akili vijana wapya walionunua magari nakufanya safari za mara ya kwanza kwenye highways! Hao ndio madereva hatari sana kipindi hiki cha sikukuu
Kama tu vile wanavyo piga picha ya mapafu yaliyoharibiwa na cancer kwenye pakti za sigara
Picha yako hii ya mkeka kwenye katafunua za mwidu! Zinawashawishi vijana kkuona speed ya 150 inawezekana kirahisi nchini
Upo Sahihi kabisaa mkuu ngoja niweke na video
 
Mwezi Disemba Nchini watu wengi mnafikiria kurudi vijijini kusherekeha sikukuu ya Kristamas,haswa wenyeji wa Kilimanjaro. Nyakati hizi ajali za barabarani huwa zinakuwa nyingi sio kwa sababu Mwezi Disemba ni mbaya, Ila kwa sababu ya kukosa nidhamu na uzoefu/barabarani

Umetoka chuo,umekopa gari na route zako ni Mwenge,Masaki,night Clubs, unafikiri wewe ni dereva makini. Huko highway na big sound na Jameson kichwani na Video Call. UTAKUFA. Wazazi wana kusubiri Kijijini mfurahi sio kupokea maiti. Kuwa makini acha Yada Yada. Endesha Gari kwa nidhamu

Godbless E.J. Lema
Dec 19, 2022
 
Huu mwezi mpaka inaogopesha kusafiri, nafikiria kupanda basi tu mambo yasiwe mengi!
You are by far better off with that, December inazingua sana haswa njia za kuelekea kaskazini.
Shida mabasi nayo yanajaa sana miezi hii kwa hiyo kama ni mtu uliyezoea uhuru wa ndinga yako unaeza ona ni safari ya mateso pia
 
Vipi kwenye ule uzi ulokua unatushauri tutembee usiku ushaenda kuukanusha?!
Hahahaha 😆 😆 😆 😆
Mkuu sikuhizi nimezeeka hata kuona kwangu Kwa shida usiku .
Pia nitaenda kuwapa ushauri kwenye Uzi wangu juu ya kutembea usiku kama
 
Back
Top Bottom