ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Holiday ikiwadia, kila mtu anakuwa na mawazo ya kupumzika. Mitandao ya kijamii imejaa maudhui ya safari resort, fukwe, hoteli za kifahari na picha za vinywaji pembeni ya bwawa. Ndipo nikawaona tangazo: “Safari ya Zanzibar, siku 3, bei poa kabisa. Lipa leo, safari kesho.”
Bila kusita, nikawasiliana na yule “wakala.” Aliongea vizuri, nikatuma picha za hoteli, tiketi za ndege (zilizoonekana halisi), na akaongeza presha: “Nafasi zimebaki mbili tu.” Nikatuma hela, nikapiga screenshot, moyo wangu ukajaa furaha.
Alijibu haraka, kwa kujiamini, akatuma picha za hoteli, ratiba ya safari na hata tiketi za Boti, kisha akaongeza presha; “Nafasi zimebaki mbili tu, dada.”
Kesho yake… simu haikupatikana. WhatsApp ticks moja tu. Nilipoingia Instagram, nikagundua account imepotea. Ndipo ukweli ukagonga holiday yangu imegeuka mkasa.
Wakati wengine walipokuwa wanapost picha za kupumzika, mimi nilikuwa nikipost status ya onyo: “Holiday sio holiday bila akili. Tahadhari na matapeli!”.