Ujue ugonjwa wa homa ya ini
*Utangulizi kwa kifupi*
Hepatitis b (Homa ya Ini) ni maambukizi ya virusi kwenye Ini(Liver) .
Ini likiambukizwa hatuna matibabu kamili na yakueleweka Tanzania. Hepatitis (Homa ya Ini) imekuwa tishio kwa miaka hii na hasa kwa vijana.
JINSI HOMA YA INI INAVYOENEA
1.Ngono isiyo salama
2.Kuchangia nguo(Jasho na maji maji)
3.Romance(maji maji)
4.Kuchangia vifaa vyenye ncha kali
DALILI ZAKE NI ZIPI?
Dalili zake hutokea wakati wa hatua za mwisho za kuharibika kwa Ini. kwa hiyo hakuna dalili za awali za ugonjwa huu.
1.Macho na mwili kuwa vya njano
2.Tumbo kuvimba
3.Kutapika damu
4.Kukosa hamu ya kula kabisa
5.Tumbo kuvimba(Abdominal distention)
6.Tumbo kuuma linapokugwa hasa sehemu ya ini(Epigastric pain on palpation)
MATIBU YAKE YAKOJE?
Bado ni changamoto na hasa kwa Tanzania kwani ni wachache sana wanaopenda kupima afya na kujua hali zao za Ini na hivyo kuchukua hatua .Kwa kuwa dalili hujitokeza dakika za mwisho za kufa kabisa kwa Ini kwa hiyo tiba kamili ni kubadilisha Ini kitu ambacho mazingira yetu ni changamoto sana.
Note: Ini liko moja tu tofauti na figo ambazo ziko mbili kwahiyo hata kubadilisha ina mhitaji mtoaji afe ili mgonjwa aishi.
CHANJO YA HOMA YA INI
Siyo wote wanaweza kupata ugonjwa huu,ukipata chanjo uko salama kwa asilimia 100%
NANI YUKO HATARI KUPATA UGONJWA HUU?
1. Wanaofanya ngono uzembe pasipokuwa na chanjo.
2. Wafanyakazi wa Idara ya afya hasa wauguzi na madaktari wanaogusa wagonjwa mara kwa mara pasipo kuwa na chanjo!
3. Watoto wanaozaliwa na mama mwenye vimelea vya virusi vya homa ya Ini.
MABARAZA YA DUNIA YANASEMAJE KUHUSU UGONJWA HUU TISHIO.
1. Kila mjamzito anaye anza kliniki kwa mara ya kwanza lazima apime ugonjwa huu ili kumlinda mtoto anayezaliwa.Kwa Bahati mbaya wanao pimwa ni wale wenye uwezo na wenye bima za afya ambao hujifungulia kwenye hospitali kubwa na zenye vifaa; Aga khani, Mihimbili, TMJ, KAIRUKI, Hindu mandal, Mbeya rufaa, Bugando, Selian,n.k
Note: Kiwango cha vifo vya vijana wa kiume kwa ugonjwa huu ni kubwa sana ukilinganisha na wanawake.
UFANANO NA UTOFAUTI WA HOMA YA INI NA UKIMWI.
A. UFANANO
Hepatitis ina fanana na ugonjwa wa ukimwi kwa muktadha huu,
1. Jinsi Ukimwi unavyo enea ni sawa na Hepatitis.
2. Hakuna tiba rasmi kwa magonjwa haya yote mawili.
B) UTOFAUTI
1. Homa ya Ini inachanjo, Ukimwi hauna.
2. Ukimwi una dawa za kurefusha maisha,Hepatitis haina unapewa dawa za kupunguza maumivu ukisubiri kuondoka!
3. Virusi vya Homa ya Ini hukaa kwenye maji maji ,Mate(Denda) ,Jasho na damu. Wakati virusi vya Ukimwi hukaa kwenye damu tu.
4. Virusi vya homa ya Ini hukaa nje ya mwili(Kwenye nguo,wembe n.k) kwa siku saba,wakati virusi vya ukimwi hukaa dakika 30 tu.
5. Ugonjwa wa Ini ukiona dalili zake baada ya miezi sita mgonjwa hufariki, Wakati ukimwi ukiona dalili na ukawahi hospitali una ishi miaka zaidi na zaidi.
Dr.Dyumurushi,(B.E,MD,MPH).