Homa ya Manjano (Homa ya Ini): Zijue athari, kinga na tiba za ugonjwa huu

Mtoa mada mbona unataka kupotosha watu hapa!!
Hiyo homa ya manjano uliyoizungumzia hapo mbona inatibika vizuri tu!!

Hiyo uliyoelezea wewe ni homa ya ini(HBV)
na sio homa ya manjano (yellow fever) ni vitu viwili tofauti kabisa.

Homa ya manjano haiambukizwi kwa hizo njia zako ulizoandika hapo Juu.
 
Huu uzi inabidi ufanyiwe editing, kuepuka kutoa elimu isiyo sahihi kwa wasomaji.
 
Mim ni kijana wa makamo tu ila miezi kadhaa nilikuwa nataka kumuongezea damu rafiki yangu kwa kuwa nina group O ndipo madaktar walipopima damu yangu ikagundulika ina vïrusi kwenye ini aina ya Hepatitis B.

Madaktari wakasema nianze kutumia dawa iitwayo Truvador ndani ya miezi sita nitapona lakini nimetumia mpaka kukamilisha dozi hiyo nikakaa miezi mitatu bila kwenda kupima tena nikiwa nafikiri nimepona kwa sababu sikuwa na hii elimu ya ugonjwa huu.

Nilipoenda kupima baada ya kuwa nasikia uchovu nilikuta bado homa ipo halafu daktari mmoja akaniambia kwa siri kuwa huo ugonjwa hauna dawa ya moja kwa moja ya hospitalini.

Hïvyo ndugu zangu naomba msaada mwenye kujua dawa hakika za kuponyesha anisaidie.

Maoni ya Wadau:

 
Huu ugonjwa unatibika nenda Muhimbili ama Mloganzila (sina hakika na jina) watakusaidia.

NB: Nenda Muhimbili
 
bill Shnky,
Inabidi uendelee na truvada kwa mwaka mzima.Una chronic Hepatitis B infenction. Saa zingine miezi sita ya tiba haitoshi. Picha acha kunywa pombe kama unakunywa.
 
Nadhani haipungui 20,000 japo sina hakika, na unapata mara tatu.

Chanjo ni muhim sana, ugonjwa upo na ni hatarii kweli
Kwa hosp niliyopitia chanjo kwa dozi 1 ni Tsh 50,000 japo inaenda mpk 75,000 so ni gharama kubwa.

Ni ushauri tu, watu tuchome as huu ugonjwa ni mkali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…