Mleta mada ngoja na mimi nikujibu!
1. Mashabiki wa sasa tunaibeza Milan kwa kuwa hakuna ikifanyacho, yaani squad ni mbovu na mpira ni mbovu. Kwanini unajivunia historia wakati kwa sasa hakuna ufanyacho. Mkishuka daraja bado utajivunia Historia?
2. Kitu cha muhimu ktk soka ni Soka safi (kama Barca, Man City, Bayern n.k) Magoli (Madrid, Bayern, Barca n.) na Makombe (Barca, Man City, Bayern, PSG n.k). Hiyo Historia ni yako sababu watu tunaangalia mbele wala sio nyuma, ukitaka kubeba makombe jitazame sasa ulivyo kisha itazame na kesho na SIO kuangalia Historia. Kama unatazama Historia basi sajilini wachezaji wakubwa kama zamani, si mna historia wachezaji wakubwa kucheza hapo? Bebeni pia na makombe kama zamani, tumieni historia hiyohiyo kubeba makombe.
3. Hiko kipigo cha mbwa koko alichopata Barca kwa Milan, unadhani Barca hakumpa hiko kipigo Milan!? Hivi unajua baada ya Barca kumpa Milan hiko kipigo Milan wakaamua wasirudi tena mpaka UEFA, na ni kweli mpaka leo hajarudi. Kwa statistic, ni nani kati ya Barca na Milan anaongoza kumfunga mwenzie!?
4. Kutwaa tuzo bora na ubora wa timu tuviweke pembeni, maana timu kama Barca tangu 2007 inaingiza mchezaji au wachezaji ndani 3 bora na mara 5 mchezaji wao kabeba.
5. Hizo tripo R zote zimecheza Barca pia ila nasikitika kusema kuwa hizo Tripple R zilikuja Milan zikiwa zimechoka. Ronaldinho kaja Milan akiwa kachoka baada ya kutemwa na Barca, De Lima kaenda Milan akiwa kachoka japo sio sana kama Gaucho, na Rivaldo hivyo hivyo.
6. Milan mnajisifu kumficha Ronaldo ndani ya dakika 45!?
-Barca aliificha Man U timu nzima ndani ya dakika 80, hii ilikuwa final ya UEFA pale Ufaransa, hakuonekana Rooney wala Ronaldo wala ile mido yao inayoitwa Paul Scholes.
-Barca pekee iliwahi kumtetemesha Sir Alex pale kwake England, akwa anatetemeka kama anaumwa Dengu!!!
UKIWA UNAANDAA THREAD ZA KINAZI KAMA HIZI UJIPANGE.
****** Aleyn ******