Wamarekani hawajui mpira, wamekuwa kutafuta faida na umaarufu. Wanaangalia zaidi faida lakini wanasahau faida inahitaji uwekezaji, Kuna timu kama Ajax, Borusia, zile zinafanya biashara ya kukuza vipaji na kuuza na Kuna timu kama Real Madrid, ac Milan zile zilipata umaarufu kwa kuchukua vikombe. Kitendo Cha kumuuza Sandro Tonali wakati timu inajengwa ni upuuzi na usaliti mkubwa kwa mashabiki wa ac Milan hasa baada ya timu kufika nusu fainali pia kitachochea wachezaji wengine kama Theo Hernandez, Raphael Leao, Mike Maignan kuomba kuondoka baada ya kupewa ofa kubwa