Home of AC Milan, Official Thread

Home of AC Milan, Official Thread

Nakuonea huruma sidhani kama utaonekana kuanzia j5 vs Barca na j2 hasimu wako Inter,vichapo vitakukukimbiza,ila u cant run away from yourself,au sio?
 
kawaulize mashabiki wa soka catalunya kitu inaitwa CATENACCHIO uone watakavyokupopoa mawe!barca zote hata ziwe nzuri namna gani zimekuwa wahanga wa hii football style ya italia.ukisikia mtaliano kafungwa na mspanish basi ujue aliamua kucheza mfumo mwingine.kwa jinsi milan walivyo na average players sasa hivi,ni wazi hawatajisumbua na open football,sasa wakicheza catenacchio bhaaas!hamna cha messi wala iniesta,inawekwa fomesheni ya 8-1-1,mtahangaika nyie wee,wao wanawatazameni mkiingia target anapewa pande sniper mmoja kama el shaarawy au montolivo,ananyamazisha ngoma za catalunya.na mashabiki wa barca wanaijua shughuli hii ndio maana wakimuona mtaliano kapaki basi nyuma huwa wanajua kuwa hilo ni treni wanakaaga kimya uwanjani.mwaka jana iliwakuta shughuli na messi wao uwanjani,palikuwepo mtaliano mmoja tu uwanjani,anaitwa di matteo,akapaki treni lake nyuma,messi,iniesta hangaika wee,dk za mwisho watu wakamtupia AK47 sniper wao Torres,shughuli ikaisha!huyo alikuwa mtaliano mmoja tu na alikuwa nje ya uwanja,sasa muziki mzima wa milan na jinsi allegri anavyotafuta wa kumpunguzia stress zake!nasema hivi,milan akicheza catenacchio,and it is likely,hakuna barca yoyote ya kuwasumbua waitaliano,awe milan,juve,inter,napoli,lazima barca akalie!

gutierez unakakumbuka haka kapost?
 
Milan 2-0 Barca...
Thanx to former Portsmouth and Ghana Duo...
 
Barcelona walizidiwa ujanja na umakini katika kukaba! Milan walikuwa makini sana katika kukaba, kiasi kwamba Fabregas, Pedro, Xavi na Iniesta hawakuwa na uhuru wa kucheza na mpira kama kawaida yao. Pia uamuzi wa AC Milan kucheza 4-3-3 huenda umechangia sana kuwachanganya mabeki wa Barca, kwa sababu walikuwa wanavutika sana pembeni na kuacha matundu katikati!
Pia Milan walitumia nafasi zao vizuri. Barca walikuwa wame-panic sana jana!
Siku hazifanani..na huenda mwaka huu Barca wakatoka hatua hii!
 
Kwanza nawapa hongera AC Milan kwa kutufunza adabu jana,sawa nimekubali matokeo,ila kocha hatuna,kikosi kilekile hadi wamekariri,sikati chenga twawala lakini tulifungwa,ila goli la kwanza refa aliwasaidia mkono walikuwa 12,maana aliunawa kabla Prince kufunga goli,sawa sikatai,ila mimi namlaumu kocha hakuwa na mbinu,mechi ya jana Xavi ilitakiwa asingemaliza angewapa nafasi Thiago na hata Song maana AC Milan walijaza waafrika wengi so Song angesaidia,maana ukichunguza listi ya jana ndio ileile aliweka vs Granada yaani hata AC Milan walijua kabisa listi itakuwa hivi na hata Gang Chomba akapanga utadhani nae alikuwa na wana La Masia,hata mechi ya marudiano siwezi kusema lolote maana wapo frustrated na listi kocha hana mbinu kama Mourinho na Fergie,binafsi Milan wamenifunga ila siwakubali kiukweli hata kama watatutoa,imeniuma tumefungwa na timu mbovu yaani afadhali ningefungwa na Arsenal kuliko AC Milan maana kocha hata angeamua kuwasurprise angewaweka watoto kina Tello,Cuenca,Montoya,Adriano,Thiago nk AC Milan walikuwa wanafungwa palepale kwao kikosi cha jana walikisomea mwezi mzima na ukichunguza sawa kocha inabidi ubadilishe,ndio maana hata Mourinho sasa anaanza kuijua Barca maana kashasoma wachezaji wanaocheza ni walewale,Xavi namuheshimu ni mzuri ila kwa sasa hatakiwi kumaliza 90 zote kama Guardiola alivyokuwa anafanya na hata Del Bosque La Furia Roja timu ya taifa,haya mambo ya kukariri kikosi kila siku wachezaji hao hao mechi za kila kombe kama timu zote za bongo asipocheza fulani basi kocha anaingiliwa ndio inamponza huyu msaidizi Jordi Roura,nimemkumbuka Tito Francesc Vilanova i Bayo,binafsi nasema tena nimekubali nimefungwa ila hata kama tutatolewa kombe natabiri mshindi wa mechi ya Man UTD vs Real Madrid ndio anabeba maana makocha wana mbinu,zaidi ya yote Gang Chomba hongera najua ni party ya kufa mtu kwenu kumfunga mbabe wa soka duniani,ila yote 9 msijisahau sana lakini ni half time ila zaidi sasa tunasubiria mbinu za huyu mimi namuita msimamia mazoezi hana mbinu,wewe utaona tena ktk ligi kikosi kitakuwa hicho hicho,inabidi achanganya kumfanya mpinzani wako asikujue,binafsi imeniuma sana kufungwa na AC MIlan ni bora hata Arsenal ingenifunga kuliko vibonde Milan.Nimemkumbuka sana Josep Guardiola i Sala,yaani in the words of broken heart is just emotion taing me over!
 
Gutierez nimeongea obrigado lkn bado sipati wewe kwi kwi kwii!
sijalala jana kutwa nzima nalia stress,maana iliniuma kama unapomfunia mwenza wako ambae unampenda na anasifika kwa tabia nzuri sasa unamkuta LIVE bila kuhadithiwa na mtu,nimefungwa na timu mbovu bora hata Swansea ingenifunga,na yote ni kocha hatuna yule ni msimamia mazoezi,kikosi watu walishakariri mwezi mzima hichohicho,na refa nae kawapa bao la kwanza la mkono,poa hatusemi sana ila hongereni anti-Barcelona wote.
 
Back
Top Bottom