Home of AC Milan, Official Thread

Home of AC Milan, Official Thread

Habari wadau. Leo nmekuja kwenu mimi Interisti wa Nerazurri kuwakaribisha wadau wenzangu wa Inter na Italy kwa ujumla katika mahala hapa ambapo kila kitu cha Inter nntakua nakimwaga. Karibuni sana watani wangu kutoka Kaskazini wale wa Juve, Majirani zangu wa Milan, wale wa Kusini kutoka Naples(Napoli), wale wa karibia na Vatican, As Roma, Lazio , wa Genoa na mikoa yote ya Italy karibuni sana. Hapo baadae tutammaliza Sampdoria na Presidaa wetu mpya Tajiri Erick Thohir atakuepo uwanjani baada ya kumpokea Moratti aliepiga kazi sana kwa miaka 18. Karibuni saaana.

Forza Inter. Forza Nerazurri. Forza La Beneamata.

195172.jpg
 
Naona Berlusconi ameingilia kati na kumrudisha Galliani ,inasemekana Barbara alitaka kumleta Paolo Malini awe Technical Director
 
Teh teh Milan kazi wanayo. Inter tunachanja mbuga tu. January lazma kikosi kiimarishwe.
 
Naona Berlusconi ameingilia kati na kumrudisha Galliani ,inasemekana Barbara alitaka kumleta Paolo Malini awe Technical Director

Namuheshimu Maldini...ila kwa kazi ile anayoifanya Galiani basi yeye baado sana mchanga...
Anatakiwa kwanza asome njia za Galiani na aone watu aliowaleta pale Galiani kisha ndo avae viatu hivyo
 
Inter ushuzi tu kwa sasa...
ndo maana hata Masimo ameamua kuitia sokoni.
mkono usiokulisha ya nini kuubusu?
 
Ningeshangaa sana kama Gang Chomba asingekuwa mtu wa kwanza kukanyaga hapa.
 
Last edited by a moderator:
Gang Chomba,nini kinaendelea pale Milan?sielewi elewi mara Uncle Festa,mara aunty barbara,mara Seedorf,Maldini,Prandelli,..aargh kunani?kama mmemchoka uncle Festa tangazeni ndani ya masaa 24 mtasikia katua Turin!eti Barbara anataka kumchukua Fabio Paratici wa Juve,ammwache Galliani,yaani huyu Paratici tutawapeni buree mkitaka na Marotta tutawaongezeni mtupe babu "para moto" wetu muone tuwalize tena kama tulivyofanya kwa Pirlo!yaani familia ya Belursconi ni utata mtupu!kaka ya mtu bange,dada ya mtu yule nae sijui anatumia kuberi?anyway hongera kwa kumlamba Catania,huwa anakusumbua sana!sie tunaua pundamilia wenzetu leo!watch and learn!
 
Mie naona Galiani wanamuonea tu.
Mpuuzi wa kutimuliwa pale ni Alegri.
Galiani amekaa pamoja nasi kwa muda takriban miaka 28.
Yupo pale kwa vipindi vyoote, kadumu na Milan ilioporomoka na kadumu na Milan iliokuwa inapanda.
Sasa kwa nini anabebeshwa zigo la Nnya?
 
Last edited by a moderator:
Team hii sijui imepotelea wapi tangu Mourinho atoke, hata UCL hawapo.
 
We Mourinho mie pale Italy timu ninalolichukia zaidi ni hilo linaitwa Inter...
Na hata hili jukwaa sijui kama ntaandika jema la hawa watu.

Nalijua hilo kwa dhati,
Mie napenda style ya Nge/ scorpion, "kiss of death", I smile to and kiss my enemy before I smoke his A.S.S out
 
Inter mtuache tupumue. Co mbaya bado tupo nafasi ya nne point kumi juu ya Milan na Thohir kasema January lazma tujenge kikosi.
 
Back
Top Bottom