HSC wanakampuni kibao za Clearing bandarini pale, wafanyabiashara wanalazimika kuwatumia hawa jamaa kutokana na kuwa na mkono TRA na wakubwa wa wizara ya fedha. Ukijifanya unatumia kampuni nyingine kwa wafanyabiashara wa nguo, viatu, pazia na vinginevyo utapigwa ushuru wa kufa mtu. Ila ukitumia HSC container la nguo au kitenge unalipa mil.28 tunaambiwa jamaa yeye anacheza na wakubwa wa TRA anasema container lina Tooth pick au toilet paper yeye analipa TRA mil.7 dah kumbe zigo linathamani ya dola 170,000/= ishu ya Mwakyembe kuanza kukagua container imeanza kumuumbua bwana HSC na wakubwa wa TRA imesababisha taharuki kwa wafanya biashara k.koo mizigo imezuiliwa na biashara imesimama. Serikali imepoteza sana mapato juu ya hawa jamaa HSC wanakula pia na polisi wanasindikiza toilet paper kumbe nguo au vitenge au tv au friji.
TUWE MAKINI NA KINACHOENDELEA TATIZO SIO HOME SHOPPING CENTRE WADAU
Kiukweli inasikitisha sana kuona watu wachache wanaosaidia wanyonge wanachukiwa kwa misingi yao ya kibiashara
mimi ni CHADEMA FOR LIFE ila kwa hili CCM haihusiki na watendaji wanamtia aibu MH.Jakaya hapa kuna mambo matatu.
1.Kariakoo ilishakuwa Dubai ya nchi zote kongo, burundi, zambia, malawi, rwanda! Leo wanaenda uganda na kenya
2. Kodi itapungua, ajira itapungua, sisi hatujasoma tutaenda wapi
3. Nchi hii wabaya sio viongozi, wabaya watendaji! Na sisi tukiumia chuki zote kwa viongozi na ccm wao hata ikija chama kingine watabaki tu.
Mkutano ulioitishwa na waziri kuhusiana na kukwama mizigo bandarini ni kutokana na bidhaa kuwekewa kodi kubwa sana ambazo hazilipiki mizigo iliyokwama sio ya HSC ni wafanyabiashara mbalimbali na mkutano uliwahusu hao wadau wote hali ni mbaya...
tuliyoyashuhudia katika mkutano huu ni kama yafuatayo nilihudhulia kama mfanyabiashara niliyeadhirika na hili
A. Sisi wafanyabiashara ndio tunaoumia na kulipa kodi kwa mizigo inayoingia nchini lakini ajabu kubwa ya kutoa maoni walipewa mawakala wa forodha kuongea badala ya sisi wafanyabiashara ambao ndio waadhirika wakubwa wa ucheleweshwaji huu, ambao kwa kiasi kikubwa pia unawaadhiri wafanyabiashara wadogo na wananchi wa kawaida ambo bidhaa zetu ni kariakoo sehemu ambayo hao makamishna na mawaziri hawaji kununua chochote mambo yao ni ulaya na maduka makubwa huko posta kariakoo yetu hawaijui.
B. Mawakala wa forodha katika mkutano huu badala ya kujikita kujadiri sababu za msingi zinazosababisha mizigo ichelewe kutoka bandarini wao walitumia muda mwingi kushambuliana wao kwa wao kuhusu nani anapata kazi nyingi (vita ya kibiashara) jambo ambalo halikuwa lengo la mkutano huu na wala hatudhani mizigo kuchelewa kutokana na kampuni moja kupata kazi nyingi kuliko nyingine bali ni matatizo ya kiutendaji kwa hili Mh.waziri hakuambiwa ukweli kabisa mi naomba afike kariakoo ajioneee mwenyeweee.\
NB: Kilio chetu kama wafanyabiashara kuhusu ucheleweshaji wa mizigo ni suala la uthaminishaji mizigo (valuation) ambao maafisa wa TRA wanaweka bei kubwa sana kuliko ukweli kusababisha kodiinayotolewa kuwa kubwa kiwango ambacho hakilipiki.