Home Theater, Sound Bar na HI-Fi Music kilicho Bora kwa Wapenda music Majumbani

Home Theater, Sound Bar na HI-Fi Music kilicho Bora kwa Wapenda music Majumbani

Nunua soundbar ya JBL uendane na ukisasa zaidi hasa zenye wireless speaker 5:1, kwa maana utakula movies, mziki mzuri pia mzito

Ila kwenye HT mfano sony hakikisha ni OG from Malaysia maana copy ni nyingi sana saivi watu wanalia wanakufa sana saivi
 
JBL bei gn maana watu wanasema ni kalii sn bei ss ndio sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza tujue kuwa home theatre systems si kwa ajili ya muziki bali ni kwa ajili ya movie ingawa watu wengi wanazitumia pia kwa ajili ya muziki.
System hizi hazitengenezwi kwa ajili ya kutoa power output kubwa inayohitajika kwa ajili ya muziki kwa kuwa muziki kwenye movie unakuwa wa chini chini(underground) ili kuruhusu mazungumzo kusikika vizuri pamoja na kuhandle effect sounds.
Kwa hiyo tunaondoa home theatre systems kwenye discussion.
Tukija kwenye sound bars. Hizi systems pia ni kwa ajili ya movie ndio maana zimeundwa zikiwa na baadhi ya spika zenye uwezo wa kurusha sauti (forward firing) yaani spika za sound bars zikiwekwa kwa kuangalia juu zinarusha effect sounds juu darini halafu sauti inashuka kwa mtazamaji ikitokea juu na sio mahali ilipo spika. Halikadhalika sound bar speakers zinazowekwa mbele zikiangalia nyuma zitarusha sauti kwenye ukuta wa nyumba na kurudi kwa mtazamaji ikitokea nyuma. Hizi ni sound bars zilizowezeshwa kwa teknolojia ya surround sound mfano DTS na/au Dolby Digital. Kwa hiyo hizi nazo tunaziondoa.
Lakini kuna sound bars ambazo ni stereo. Hizi ni 2 channel systems kwa hiyo hazina sifa ya kutumika kwa movies
Sasa tulinganishe hizi na hifi systems.
Zote zinafaa kwa muziki ila zinatofautiana power output. Sound bars zina spika ndogo zilizopangwa kwenye miche(bars). Kwa sound quality ni nzuri lakini kama una sebule kubwa zinaweza zisikidhi haja yako na pia kama una party zinaweza kukuanguisha kwa sababu power output ni ndogo. Zinafaa zaidi kwenye visebule vidogo. Lakini kuna watu wanazipenda kwa sababu hazihitaji nafasi kubwa halafu hazionekani sana sebuleni mgeni anasikia muziki anahangaika kujua unatokea wapi kwa kuwa haoni spika pengine wamezipachika mahali ambapo pana kagizagiza.
Hifi systems ndio hasa mahali panapofaa kwa suala la muziki kwa sababu zina spika kubwa zinazotoa power output ya kutosha. Kama una uwezo wa kifedha basi nunua hizi.
Pia siku hizi kuna hifi systems ambazo zimewezeshwa na surround sound tech. Yaani unaswitch kati ya stereo na surround. Ingawa gharama ni kubwa pia lakini kama unaweza bora kutafuta hizi mfano mmoja ni LG DM7630 DVD Mini Audio HiFi.
Kwa hiyo kuchagua kati ya sound bar na hifi inategemea bajeti yako na mahitaji yako.
 
Ukiambia uchague moja kati ya hifi, home theater, sound bar basi wewe chagua home theater kwa sababu zinakua na mini hifi ndio maana hata kwenye kuset utambiwa music au movie unataka ipi. Hifi ni uwezi kuangalia movie.
NB: hapa nazungumzia home theater km za sony zingine zina uzoefu nazo
View attachment 2233235
 
Hizo ni teknolojia ya kizamani pia sio za kistaarabu sound bar ni better
 
Hizo ni teknolojia ya kizamani pia sio za kistaarabu sound bar ni better
Nani kakwambia Hifi ni ya kizamani Boss???? Sema tu nchini kwetu tunaenda na upepo. Tulihamia kwenya HT na Subwoofer za kichina na sasa tunajaa kwenye sound bars. Ila huko Duniani Hifi inapendwa sana na imeboreshwa sana. Na asikwambie mtu ulinganishe Music wa HT na Hifi, Hifi ni habari nyingine, special for music. Hata kwa bei tu HIFI za miaka hii ni mkasi kuliko HT

Usiniambie huyu mwamba SONY shake X70D umweke na SONY HT BDV-N9200W / N9200WL
1653147464488.png
1653147648209.png
 
Nani kakwambia Hifi ni ya kizamani Boss???? Sema tu nchini kwetu tunaenda na upepo. Tulihamia kwenya HT na Subwoofer za kichina na sasa tunajaa kwenye sound bars. Ila huko Duniani Hifi inapendwa sana na imeboreshwa sana. Na asikwambie mtu ulinganishe Music wa HT na Hifi, Hifi ni habari nyingine, special for music. Hata kwa bei tu HIFI za miaka hii ni mkasi kuliko HT

Usiniambie huyu mwamba SONY shake X70D umweke na SONY HT BDV-N9200W / N9200WLView attachment 2233260View attachment 2233265
Za kizamani hata iweje huwezi fananisha na soundbar uliza ilio ni teknolojia ya miaka 20 nyuma angalia hata bei chukua ht watts1000 ya sony angalia na sound at watt iyo Kwa bei utaelewa.

Nilikuwa na HT moja nilinunua laki 8 kitu kama icho miaka ya 2019 spika kibao halilet mvuto getto nikienda kwa wana Wana soundbar zile za 1000watts yaani kwanza pale kweny tv showcase hapana uchafu kuna lile spika lake kichwa na bar iko mounted kweny ukuta chini ya tv
Spika za pembeni ni wireless zimepiga kweny Engle ndogo wakiweka movie hatar na tv kitu cha lg OLED we acha watu wanaishi
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] sounds bars kwa ajili ya TV, huwezi linganisha HiFi na sounds bars.
 
Back
Top Bottom