Home workout special thread (Uzi maalumu wa Mazoezi unayoweza kufanyia nyumbani)

Habari za muda huu wakuu......

Kila mmoja wetu anajua faida na manufaa ya kufanya mazoezi ya viungo na kuweka Sawa utimamu wa afya ya mwili na akili.....

Nimeonelea kuanzisha jukwaa hili ili tukutane wapenda mazoezi kuhamasishana, kufahamiana, na kupeana mbinu mbali mbali kuendelea kudumu kwenye mazoezi.......

Pia mwana jukwaa unaweza kutoa shuhuda namna mazoezi yalivyokusaidia kutoka hatua moja au nyingine lengo ni kuwavutia wengine nao wavutike kuingia kwenye utaratibu huu wa maisha wenye manufaa kibao.......

Karibuni wadau na watu wa mazoezi

NB;
Mods watarekebisha kwa namna ambayo itafaa ili ujumbe na lengo vitimie......
 
asante nayatumia sana haya mazoezi
 
Daah napenda sana mazoezi nadhani nishakuwa teja wa mazoezi kwa sasa nipo vizuri sana kweny push ups kukimbia si sana, squash, abs workout siku tano za wiki jmos na jpil napumzika.

Situmii kifaa chochote so mazoez yangu ni popote nitakapoenda sina kizuizi chakufanya.

Nilianza tangu mwaka 2009 mpaka sas sitaman kuacha kabisaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…