Honda Fit ni kagari kazuri nje na ndani, bei rafiki, mafuta kananusa, lakini watu hawakanunui. Kwanini?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Sijui kwanini Watanzania wameikataa hii gari kutoka Japan, Honda Fit.

Siongelei Honda Fit za miaka ile zina shape za ajabu, naongelea hii Honda Fit Hybrid ya mwaka 2014 hadi 2017, ambayo ni Fit 3rd generation.

Hii gari ni nzuri kuanzia nje muonekano wake. Ni kadogo, karibia sawa na IST (2nd gen) kwa size.

Screenshot_20240808-004306.png

1280px-2017_Honda_Jazz_EX_Navi_i-VTEC_CVT_1.3_Front.jpg

1280px-2017_Honda_Jazz_EX_Navi_i-VTEC_CVT_1.3_Rear.jpg

Ndani pia kuanzia mbele imekaa kisasa sana. Kuanzia full options kwenye steering wheel, cluster gauge ikiwa na LED screen, infotainment screen ikiwa na touch-buttons za AC na audio control.

images (2).jpeg

Pamoja na kwamba Honda Fit ni gari dogo, ila ina nafasi kubwa. Kwahiyo seat za nyuma nafasi ipo na mtu anaweza kukaa kwa amani.

images (6).jpeg

Ukichukulia ni hybrid, hii gari ina options tatu za kuendesha. Sport mode, Eco mode na full EV mode kutegemea na power unayoitaka. Kwa matumizi ya Eco mode, Fit inaweza kwenda hadi 35+ km/L kutegemea na uendeshaji.

Engine yake ni 1.5L ikiwa na DCT (transmission), na inatoa hadi 130hp. Pamoja na engine kuna hybrid battery na 20hp zingine zinatoka kwa electric motor inayosaidia kuongeza nguvu.

Technology yake ya hybrid kidogo iko complicated sio kama ya Toyota, ila ni kongwe na nzuri na ndio unaipata kwa Honda Vezel na Grace.

Bei sio mbaya. Kutoka JP unaweza kuipata kwa CIF $5,000 ilio katika hali nzuri sana.

Screenshot_20240808-010640.png

TRA kidogo wanakatisha tamaa, kwakua same car mwaka jana ilikua under Mil 5.5 ila sasa naona Mil 7+ ila fresh.

Screenshot_20240808-010807.png

Kwa kuchukulia sifa za magari ya JP, hii ni moja ya gari bora na imara sana na itafaa kuimiliki one day kwa kuzingatia trend ya gharama ya mafuta.

Sasa kwann watu wasichukue wapigie ata Uber au Bolt?

Sijawahi kaa nayo zaidi ya siku moja, ila nimeendesha masaa kadhaa. Nilipenda interior yake, cabin noise ni ndogo (nikifananisha na gari nyingine za segment yake ukiendesha ni kama upo nje makelele), ulaji wa mafuta mzuri, ilavyoshift kutoka EV kuja kutumia Engine ni smooth sana sio inashtuka kama Prius (3rd gen).

Screenshot_20240808-004306.png
 
Attachments

  • 2009_Toyota_Urban_Cruiser_outline.png
    2009_Toyota_Urban_Cruiser_outline.png
    25.7 KB · Views: 28
Hiyo gari ndio IST ya Botswana wanaielewa kuliko maelezo peleka gari yeyote ile hawataielewa zaidi ya hiyo mpaka huko Pandamatenga nimeona wadogo wakifata Durban hizo gari ni kweli ni gari nzuri na mafuta inatumia kidogo kuliko gari nyingi ndogo na pia ina balance na comfort pia imo...
 
Wabongo wakiipenda gari fulani wanaipenda aswa,wakiichukia ni kpaka akili ziwarudi ndio watailewa,Rav 4 waliwahi kuisema ni gari ya kike miaka ileee ya early 2000.
Gari za injini ya VVTI zilipata shida sana kueleweka nchini.
Tukirudi kwenye mada yako tatizo ni hilo la Kuwa hybreed

Tatizo la pili brand ya honda Iimekaponza,the same car ingekuwa Toyota ingeuzika
 
Sijui kwanini Watanzania wameikataa hii gari kutoka Japan, Honda Fit.

Siongelei Honda Fit za miaka ile zina shape za ajabu, naongelea hii Honda Fit Hybrid ya mwaka 2014 hadi 2017, ambayo ni Fit 3rd generation.

Hii gari ni nzuri kuanzia nje muonekano wake. Ni kadogo, karibia sawa na IST (2nd gen) kwa size.
View attachment 3064211
View attachment 3064212
View attachment 3064213

Ndani pia kuanzia mbele imekaa kisasa sana. Kuanzia full options kwenye steering wheel, cluster gauge ikiwa na LED screen, infotainment screen ikiwa na touch-buttons za AC na audio control.View attachment 3064214
Pamoja na kwamba Honda Fit ni gari dogo, ila ina nafasi kubwa. Kwahiyo seat za nyuma nafasi ipo na mtu anaweza kukaa kwa amani.

View attachment 3064216

Ukichukulia ni hybrid, hii gari ina options tatu za kuendesha. Sport mode, Eco mode na full EV mode kutegemea na power unayoitaka. Kwa matumizi ya Eco mode, Fit inaweza kwenda hadi 35+ km/L kutegemea na uendeshaji.

Engine yake ni 1.5L ikiwa na DCT (transmission), na inatoa hadi 130hp. Pamoja na engine kuna hybrid battery na 20hp zingine zinatoka kwa electric motor inayosaidia kuongeza nguvu.

Technology yake ya hybrid kidogo iko complicated sio kama ya Toyota, ila ni kongwe na nzuri na ndio unaipata kwa Honda Vezel na Grace.

Bei sio mbaya. Kutoka JP unaweza kuipata kwa CIF $5,000 ilio katika hali nzuri sana.
View attachment 3064218

TRA kidogo wanakatisha tamaa, kwakua same car mwaka jana ilikua under Mil 5.5 ila sasa naona Mil 7+ ila fresh.

View attachment 3064217

Kwa kuchukulia sifa za magari ya JP, hii ni moja ya gari bora na imara sana na itafaa kuimiliki one day kwa kuzingatia trend ya gharama ya mafuta.

Sasa kwann watu wasichukue wapigie ata Uber au Bolt?

Sijawahi kaa nayo zaidi ya siku moja, ila nimeendesha masaa kadhaa. Nilipenda interior yake, cabin noise ni ndogo (nikifananisha na gari nyingine za segment yake ukiendesha ni kama upo nje makelele), ulaji wa mafuta mzuri, ilavyoshift kutoka EV kuja kutumia Engine ni smooth sana sio inashtuka kama Prius (3rd gen).

View attachment 3064211
Kwa hiyo hako kagari kununua plus Kodi ndio karibu 20mln? 😆😆
 
Honda Fit Ni gari Nzuri na ngumu mno, tofauti na Toyota IST au vitz... Mi nina miliki ya 2010 ya kawaida sio hybrid. Full tank Ni lita 32 tu unatembea zaidi ya km 500.
Tangu niwe nayo mwaka wa 3 sijawahi kupata shida yoyote zaidi ya service za kawaida za oil.
Ni nzuri kwa town trip au zile safari fupi fupi. Mapungufu niliyoyaona ni kwa safari ndefu (nilisafiri nacho zaidi ya km 650) ni kuwa siti zake zinaumiza sana mgongo. Kuna siku pia nilisafiri umbali wa KM 200 kwenda kurudi, mgongo pia ukawa uunauma.
Labda hilo tatizo la siti wamerekebisha kwenye hizo za 2014-2017 otherwise Honda Fit is the best vehicle.
 
Niuzie hako mkuu
 
Back
Top Bottom