Honda Fit ni kagari kazuri nje na ndani, bei rafiki, mafuta kananusa, lakini watu hawakanunui. Kwanini?

Honda Fit ni kagari kazuri nje na ndani, bei rafiki, mafuta kananusa, lakini watu hawakanunui. Kwanini?

Sijui kwanini Watanzania wameikataa hii gari kutoka Japan, Honda Fit.

Siongelei Honda Fit za miaka ile zina shape za ajabu, naongelea hii Honda Fit Hybrid ya mwaka 2014 hadi 2017, ambayo ni Fit 3rd generation.

Hii gari ni nzuri kuanzia nje muonekano wake. Ni kadogo, karibia sawa na IST (2nd gen) kwa size.
View attachment 3064211
View attachment 3064212
View attachment 3064213

Ndani pia kuanzia mbele imekaa kisasa sana. Kuanzia full options kwenye steering wheel, cluster gauge ikiwa na LED screen, infotainment screen ikiwa na touch-buttons za AC na audio control.View attachment 3064214
Pamoja na kwamba Honda Fit ni gari dogo, ila ina nafasi kubwa. Kwahiyo seat za nyuma nafasi ipo na mtu anaweza kukaa kwa amani.

View attachment 3064216

Ukichukulia ni hybrid, hii gari ina options tatu za kuendesha. Sport mode, Eco mode na full EV mode kutegemea na power unayoitaka. Kwa matumizi ya Eco mode, Fit inaweza kwenda hadi 35+ km/L kutegemea na uendeshaji.


Engine yake ni 1.5L ikiwa na DCT (transmission), na inatoa hadi 130hp. Pamoja na engine kuna hybrid battery na 20hp zingine zinatoka kwa electric motor inayosaidia kuongeza nguvu.

Technology yake ya hybrid kidogo iko complicated sio kama ya Toyota, ila ni kongwe na nzuri na ndio unaipata kwa Honda Vezel na Grace.

Bei sio mbaya. Kutoka JP unaweza kuipata kwa CIF $5,000 ilio katika hali nzuri sana.
View attachment 3064218

TRA kidogo wanakatisha tamaa, kwakua same car mwaka jana ilikua under Mil 5.5 ila sasa naona Mil 7+ ila fresh.

View attachment 3064217


Kwa kuchukulia sifa za magari ya JP, hii ni moja ya gari bora na imara sana na itafaa kuimiliki one day kwa kuzingatia trend ya gharama ya mafuta.

Sasa kwann watu wasichukue wapigie ata Uber au Bolt?

Sijawahi kaa nayo zaidi ya siku moja, ila nimeendesha masaa kadhaa. Nilipenda interior yake, cabin noise ni ndogo (nikifananisha na gari nyingine za segment yake ukiendesha ni kama upo nje makelele), ulaji wa mafuta mzuri, ilavyoshift kutoka EV kuja kutumia Engine ni smooth sana sio inashtuka kama Prius (3rd gen).

View attachment 3064211
kweli kila mtu na namna anavyoina kitu haka kagari hata sikaangalii mara mbili ukichanganya na wenzake passo vitz ist glanza na viuchafu vingine vidogo dogo vinavyosifika kwa kutokula mafuta..... unaendesha gari kama karatasi dah kwangu hapana
 
Ndoa yao ilidumu miaka karibu 15 nadhani sasa hivi Mazda wapo na Toyota pana parts zilikua zinaingilia kwa mazda na Ford na pia zipo Nozel unafunga mazda na Ford kwa gari za diesel..vile vi Bantam na madza za kizamani vilikua sawa vitu vingi..
ok mkuu nimeelewa nilikuwa silijui hilo kabisa.
 
Dadeki wabongo ni zaidi ya wehu, Kodi inazidi bei ya gari, pumbaf kabisa
Yani Bongo kuna udalali wa kufa mtu, sasa sipati picha kama hayo magari tungekuwa tunayatengeneza Sisi tungetoza VAT kiasi gani kama kuyapokea tu tunatoza Kodi kubwa kiasi hicho
 
Gari inayotrend sasa hivi bongo ni Mazda cx-5, na imekaa fresh sana nimekaa nayo siku nzima imetulia sana,, gari ambazo hazinunuliki kwa sasa hivi ni dualis na jike kidogo na rumion
 
Hako kagari nakatumia sana Johannesburg kwa safari za ndani mafuta hata sijutii kwa umbali wowote...
20240514_084432.jpg
 
Back
Top Bottom