Honda HR-V.

Honda HR-V.

specialist88

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
1,140
Reaction score
618
Salaam ndugu zangu.

Naomba kuulizia uwezo wa hii gari katika kusafiri masafa ya mbali maana nimevutiwa na ulaji wa mafuta(1.6L ingine size) pia bei yake si mbaya (mfano gari ya mwaka 2000 inauzwa kwa FOB -2000 USD.) Zaidi ina umbo/size kubwa ukilinganisha na magari mengine yenye ingine size hiyo(1.6L).

Zaidi naomba nijuzwe upatikanaji wa spare za hii gari na bei ya hizo spare zake.....


Nashukuru na Karibuni.
 
Sikushauri mdau. litakugharimu kwenye spare. na wakati wa kuliuza itakuwa shida. Tafuta gari jingine. naongea kutokana na uzoefu.
 
ok,nashukuru lakini linaweza kulamba masafa marefu?
 
nunua ndugu yangu kuliuza utapata wakulinunua kama wewe ulivonunua kwa mapenzi

haya rubii,ninachohitaji nikujua linaweza kusafiri umbali mrefu kama dsm to Nairobi au Dsm to mbeya?
 
Mkuu ulizia kingine na siyo swala la masafa marefu, enzi hizi magari yote yanakwenda masafa marefu vinginevyo hilo gari liwe bovu kwenye cooling system. Bajaj yenyewe inasafiri masafa marefu, itakuwa gari!
 
Hii gari hata mimi nimeilewa ila tatizo haya maneno ya spea ndio msala
 
Mtoa mada umefanya vema, ngoja niwe around nipate kujua zaidi kuhusu hii model ya CRV hapa Tz kuitunza kwake inakuaje. Kikubwa ningependa kujua garage zake za uhakika tukichilia zile kubwa kubwa.

Pia sio mbaya waliowahi kumiliki wakatueleza kuhusu matatizo yanayowakumba mara kwa mara.
 
ni gari nzuri unaweza tembe nayo zaidi ya 1000km bila kupumzika wala eng haichemki ni gari zuri kwa kweli
 
Mkuu ulizia kingine na siyo swala la masafa marefu, enzi hizi magari yote yanakwenda masafa marefu vinginevyo hilo gari liwe bovu kwenye cooling system. Bajaj yenyewe inasafiri masafa marefu, itakuwa gari!

Bajaji Dar-moro
 
Back
Top Bottom