Honda wamezindua 6th Gen Honda Prelude: Hii Coupé imerudi baada ya Civic na Accord coupés kusitishwa!

Honda wamezindua 6th Gen Honda Prelude: Hii Coupé imerudi baada ya Civic na Accord coupés kusitishwa!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Honda Prelude ni sport car iliyotengenezwa kutokea 1978 na kusitishwa mwaka 2001, na sasa inarudi officially.
IMG_3251.jpeg

Inakuja na 2.0 L engine, ikiwa imeunganishwa na dual-motor hybrid system, ambavyo kwa pamoja vitakupa 200 hp na efficiency ya 20 km/L average.
IMG_3254.png

Wanatumia CVT transmission ikiwa na Honda S+ new shift system ambayo kwa sasa Honda wanaiforce kwenye magari mengi mapya. Hii haina gear level ni mwendo wa buttons tu kuanzia D R P N.
IMG_3256.png

Kwa ndani, inakuja na 9 inch screen ikiwa na Android Auto na Apple CarPlay. Pia utapata safety features, adaptive cruise controls na lane centering pamoja na audio system ya Bose.
IMG_3255.png

Hii coupe ina seat arrangement ya 2+2 ikimaanisha mbele kuna seat mbili na nyuma mbili. Ingawa seat za nyuma sio rafiki sana kwa watu warefu, ila bado ni practical.
IMG_3252.jpeg

Kadude katamu kipindi cha summer, unaweka roof down unapiga misele highways.
IMG_3253.jpeg

Bei inakadiriwa (hawajasema official) itakua $38,000 hivi.
 
Natamani hii dunia ingebaki Kwanza kwenye hybrid car pekeyake kwasababu kama ni emission test hizi hybrid car ni zero energy kama ilivyo Kwa EVs..
Mwezi uliopita mkurugenzi mtendaji wa mercedes aliwaonya manufacturer wa ulaya kuwa hata itakapofika mwaka 2035 wasikubali kuingia moja Kwa moja kwenye EVs

Hybrid hata Sisi huku Africa zinatufaa zaidi kuliko EVs
 
Back
Top Bottom