Honest and humble man needed

Honest and humble man needed

Hahaha I love JF jamani kuna watu wako smart humu ndani duh nikweli nilimefanya kila njia nimesali sana nikaamua nimsamehe na nikamuomba tukae chini tuyaongee ili tutengeneze ya yeye aniambie yanayo muuzi niyaache na mie nimwambie yanayoniuzi ayaache ila imeshindikana ni kweli anaomba msamaha lakini habadiliki jamani nimeamua kubwaga manyanga nadhani na,mimi ni wakati sasa niwe na maisha ya amani kama Mungu akinipa kibali ndo nnachotamani waungwana

Very Good.. Mpendwa nisamehe kwa kuwa serious na hii thread yako, kwa kuwa ina funzo kubwa ambalo kwa namna moja ama nyingine inaweza ikaponya wengi humu, na Maisha nikusaidia kwa vitu vingi likiwepo la kupeana ushauri wa kujenga kwa wale wanaotakia mema wenzio. Mimi ni mmojawapo nisiyependa mtu aumie au asononeke mbele yangu ilihali nina uwezo wa kuongea neno moja tu na likaweza kutibu.

Mpendwa, Kwa umri wako hakika una haki ya kufanya chochote ilimradi kikupe amani na Furaha ya Moyoni. na Ni kweli kuwa inafika mahala unatamani uwe ni mtu wa furaha muda wote.

Sasa Lini umeamua kubwanga Manyanga kiujumla? Je wewe unatafsiri nini Juu ya Msamaha kwenye Mahusiano?

Mungu akubariki na tuendelee kufunzana mwisho tutafika tuendako. Relationship has got no Formula Japo mimi naamini Kila Kitokeacho kinatokana na three Newtons Laws of Motions hasa ile ya Tatu inayosema.

''To every action there is equal and oposite Reactions''

Karibu Mpendwa.
 
Hahaha I love JF jamani kuna watu wako smart humu ndani duh nikweli nilimefanya kila njia nimesali sana nikaamua nimsamehe na nikamuomba tukae chini tuyaongee ili tutengeneze ya yeye aniambie yanayo muuzi niyaache na mie nimwambie yanayoniuzi ayaache ila imeshindikana ni kweli anaomba msamaha lakini habadiliki jamani nimeamua kubwaga manyanga nadhani na,mimi ni wakati sasa niwe na maisha ya amani kama Mungu akinipa kibali ndo nnachotamani waungwana
Mmeachana officially au? Nabarikiwa nawe.
 
Hili ni tatizo la mabinti wengi wanaojichanganya wakiwa kwenye 20s na kufikiri mwanaume wa nani wakati "naweza kuishi mwenyewe". Muda unakwenda na apodunda miaka ya late 30s wale waliokuwa wakimshobokea wanaanza kupotea taratibu. Hapa ndo wanaanza kugundua kosa walilofanya..na mfano.mmojawapo ni mleta uzi huu. Kila la kheri mungu akutangulie maadam umetambua makosa uliyoyafanya. Linalonitatiza ni kwamba hili jambo litaendelea kujirudia kwani wale ambao hawajapitia hali hii ni wagumu kuelewa na huwa wanalazimisha kuyapitia maisha ya mleta uzi. Naomba usaidie kuwapanua mawazo wanawake wenzako watakaoweza kukusikiliza ili haya yasiwakute ingawa najua ni kazi ngumu.
 
Mimi msamaha ninatafsiri kama kumsahe mtu na kumuachilia moyoni kama mie mwanzo nilikuwa namchukia ilembaya kwa mambo anayofanya lakini badae nikamsamehe na kuanza kumuombea na kumuhurumia kuwa hajui atendalo na pia kutonipenda na kutoniheshimu isiwe sababu ya kumchukia labda moyo wake haukuumbiwa mimi kwahiyo nisilazimishe kwakuwa yeye ni mtu mzima na maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua hivyo ndo alivyochagua nisilazimishe kisicho riziki hakiliki
 
Asante natamani tuendelee kuchangia lakini nitaonekana naenda kinyume na Lengo la Mada Yenyewe, Asante na nakutakia kila la kheri
 
I love single mama, lakini kuna jambo naliogopa.
Umri kikwazo kwangu.
Mungu akuheshimu kwa nia yako ya dhati.
 
Hahaha I love JF jamani kuna watu wako smart humu ndani duh nikweli nilimefanya kila njia nimesali sana nikaamua nimsamehe na nikamuomba tukae chini tuyaongee ili tutengeneze ya yeye aniambie yanayo muuzi niyaache na mie nimwambie yanayoniuzi ayaache ila imeshindikana ni kweli anaomba msamaha lakini habadiliki jamani nimeamua kubwaga manyanga nadhani na,mimi ni wakati sasa niwe na maisha ya amani kama Mungu akinipa kibali ndo nnachotamani waungwana
Kweli umeongea ukweli inaonekana wewe ni mama unayemaanisha
 
Mimi nina miaka 45, ni single man, sijawahi kuoa na wala sijawahi kuingia kwenye mahusiano[emoji53][emoji53][emoji53].......... je nakufaa?

Mkuu;
Hivi ni kweli usemayo au?? Basi, huenda una tatizo kwani hata kama ni domo zege lakini kwa muda huu tunaouishi, mbona tunatongozwa hata na vitoto ambavyo bado vinanuka kojoo. Weye una sura mbaya kiasi gani hata usionwe nao??
Nina mvi kila mahali lakini kasichana ka jirani yangu kananisarandia mpaka nikitaka kurudi nyumbani humuomba mke wangu aje nipokea stendi ili tu nisikutane na haka kabinti peke yangu. Mwe! 45 huna wala hujawahi. Maajab ya JF haya.
Bila chenga namwambia mhusika, hufaiiii atajililia bure baada ya kukutana na weye. 45 hujawahi hata kutumbukiza mbegu mahali,leo ukakutane na limama lenye watoto. Haya endelea uone cha moto.
 
Hahaha I love JF jamani kuna watu wako smart humu ndani duh nikweli nilimefanya kila njia nimesali sana nikaamua nimsamehe na nikamuomba tukae chini tuyaongee ili tutengeneze ya yeye aniambie yanayo muuzi niyaache na mie nimwambie yanayoniuzi ayaache ila imeshindikana ni kweli anaomba msamaha lakini habadiliki jamani nimeamua kubwaga manyanga nadhani na,mimi ni wakati sasa niwe na maisha ya amani kama Mungu akinipa kibali ndo nnachotamani waungwana

Anayebadilisha Mtu ni Mungu halafu kumbuka huyo Mungu unayedai kumuabudu anachukia kuachana. Na ukisoma Biblia haikupi mamlaka ya kuolewa tena unapotengana na mumeo ni kifo tu kinawatenganisha. Kuna laana unapoachana na mke/mume wa ujana wako. Mungu habadiliki jamani hata mimi nilikuwa mlevi lakini hakuna mahali mke aliniacha Mungu ndiye aliyenibadilisha. Kumbuka ndoa yenu ni hadi kifo jump in jump out hutopata utakacho kwakuwa Mungu amekiweka kwa mumeo. Soma

Malaki 2:13-16
[13]Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
[14]Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
[15]Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
[16]Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
Zingatia hayo mama zingatia sana usije kujuta mbeleni
 
Let me talk to my big brother, it might be his last straw asee. Jimaz, vipi kuhusu huyo ulieyekuwa nae hapo kabla, mmeachana jumla? Tusije kuunganisha kumbe bado kuna mabaki ya hisia kwake tukazidi kuharibu mambo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Habari zenu,

Maisha ni safari ndefu sana na inamilima na mabonde. Kwa upande wangu mimi ni mwamamke umri miaka 43 nina watoto. Katika maisha haya nimepitia mambo mengi sana na nimejifunza mengi mno ila nimegundua hakuna kitu kizuri na kitamu kama kuishi maisha huru ya amani na upendo.

Yani natamani umri huu niliofikia maisha yangu yaliyobaki niyatumie katika maisha ya furaha na amani. Nipate mwanaume ambaye ni mcha Mungu mkristo umri from 43 and above ambaye anajitambua ambaye nayeye anajielewa na anataka kuishi maisha ya furaha na amani, tuwe wawazi kwenye mahusiano, no michepuko uwe financial stable, mimi pia sio ombaomba niko poa namshukuru Mungu.

Uwe unapenda ibada maana bila Mungu mahusiano huwa ni balaa tupu. Uwe huna mke tafadhali, uwe mmeachana, umefiwa. Hapa ni urafiki na company kwanza mengine baadae sana maana mie ni mtu wa slow motion dont get exited.

Mbarikiwe sana
Sasa kama uhuru umeufurahia mume wa nini??? Ujana ule mwenyewe afu tugawane uzee labda uwe na pesa za kutosha otherwise ata shetani atakataa ombi lako..!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Babu Asprin wahi huku
Mpenzi, ahsante kwa kujali maslahi yangu. Ila huyu si kasema "asiwe na mke?" Asa nani wa 43+ asiyekuwa na mke?? Boya??

Laiti angesema yuko tayari kuwa mchepuko... mimi babu yenu mimi ningekoma kutafuta michepuko... Hivi unajua Salt wangu kuwa mwanamke akifikisha 40+ years anakuwa ana bikra ndogo???

huyu ndo alipaswa kuwa chaguo langu... chaguo la babu... Ni vile hajui tu...
 
Hahaha I love JF jamani kuna watu wako smart humu ndani duh nikweli nilimefanya kila njia nimesali sana nikaamua nimsamehe na nikamuomba tukae chini tuyaongee ili tutengeneze ya yeye aniambie yanayo muuzi niyaache na mie nimwambie yanayoniuzi ayaache ila imeshindikana ni kweli anaomba msamaha lakini habadiliki jamani nimeamua kubwaga manyanga nadhani na,mimi ni wakati sasa niwe na maisha ya amani kama Mungu akinipa kibali ndo nnachotamani waungwana
Hebu njoo PM mzee mwenzangu tuyamalize mama. Kilio chako kimepata mfariji.

Njoo tuyajenge mama...

Wajukuu mkae kimya wakati babu akiongea na bibi yenu...

Sawa???
 
Mkuu kuna Thread ulizianzisha Humu Ukiomba Ushauri juu ya Mume wako wa Ndoa Kulewa sana na Kuchelewa kurudi naomba niziandike vizuri kuzilink nimeshindwa.

  1. Mrejesho- hii uliiandika 2015
  2. Ushauri-Mwanaume Anakunywa Pombe mpaka hawezi kufanya tendo la Ndoa.
  3. Hivi inakuwaje hii Wanaume Jamani
  4. Wanaume kuweni wa wazi kwa wake zenu.
Mama Katika Thread zako inaonekana ulifika Mahala ukakubaliana na Maisha ya Mumeo na hukupenda kabisa kugombana naye kwa kuwa kila jitihada zote ulizofanya ni kama vile ulikuwa unachochea kuni. Yaani Kama ni Uhuru Ulimpa vya kutosha Pia Kama ni Kuitunza Familia alikuwa Vizuri Pia.

Mpendwa naomba utusaidie uliamua kubwaga Manyanga au unatafuta wa Pembeni?

Asante na Mungu akubariki sana.
Link mojawapo hii hapa...
Ushauri: Mwanaume anakunywa pombe mpaka hawezi kufanya tendo la ndoa
 
Mpenzi, ahsante kwa kujali maslahi yangu. Ila huyu si kasema "asiwe na mke?" Asa nani wa 43+ asiyekuwa na mke?? Boya??

Laiti angesema yuko tayari kuwa mchepuko... mimi babu yenu mimi ningekoma kutafuta michepuko... Hivi unajua Salt wangu kuwa mwanamke akifikisha 40+ years anakuwa ana bikra ndogo???

huyu ndo alipaswa kuwa chaguo langu... chaguo la babu... Ni vile hajui tu...
Mdanganye babu wanawake bila uongo, ni sawa na chai bila sukari
 
Khaaaa hii ni perception problem au..mnk 43 nadhan si umri wa kutafuta mume bali ni umri wa kuenjoy ulivyobarikiwa km ni watoto,mali,Mungu au..nadhan ni umri ambao tyr ushajua furaha haipatikani kwa mtu bali ndani yako...you must be lonely kweli kweli..au unafanya haya kwa ajili ya watu fulani
 
Hebu njoo PM mzee mwenzangu tuyamalize mama. Kilio chako kimepata mfariji.

Njoo tuyajenge mama...

Wajukuu mkae kimya wakati babu akiongea na bibi yenu...

Sawa???
hahhhhahaa!
babu we ndo honestly and humble man???

[emoji124] leo naenda kulala kwa bibi aisee...
 
Yaelekea hata kwenye 6*6 huna papara.
Unaweka, unaisikilizia, kisha mwaaaa ! Halafu unachomoa.
Wesh ü all the lucky
 
Back
Top Bottom