MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 887
Uiva viva viva viva vivaaaaaaaaa CHADEMA tutafika tu hata mbuyu ulianza kama mchicha
kama nigeweza kukuona au kuonana uso kwa uso ningefurahi sana,hayo ndio maneno ya kujenga chama ,lakini usishangae akijitokeza magamba kupinga ushauri wako.
Umeongea mambo ya msingi sana, hivi sasa Uongozi wote wa juu wa magamba wanakosa usingizi kutokana na kasi kubwa ya moto wa M4C,kwa hiyo vikao vyao vya ndani wakati wote, wanapanga njama za kuivuruga Chadema. Lakini kwa bahati nzuri sana tofauti na siku za nyuma yaliyowakuta NCCR Mageuzi nyakati zake na CUF, Chadema wako makini sana kuwashughulikia mapandikizi na mamluki wanolipwa na magamba ili kukivuruga Chadema, ndiyo maana tabiri zao za mara Chadema kitakufa kesho,keshokutwa, mara mtondogoo,zote zinakuwa ndoto za alinacha na CDM inaendelea kuchanja mbuga kuelekea 2015,ambapo bila wasiwasi wowote itatwaa Dola kutokana na ridhaa ya wanyonge wa nchi hii watakawapigia kura za kishindo, na miongoni ya kura hizo watazipata hata kutoka kwa wana-CCM wanyonge ambaohuwa wanaambiwa CCM ina wenyewe,ambao ni mafisadi!! Cha msingi ni kuwa makini na kila mkakati unaopangwa na magamba,na kwa kuwa siku zote tunasema CDM tuna Mungu tunayemtumaini,wao CCM wana mabilioni ya pesa yaliyopatikana kwa njia za ufisadi wanayoyategemea kuwahonga mamluki ili waivuruge CDM!!Nikiri wazi kuwa hatua inazochukua CHADEMA za kukiweka chama kwenye mstari zinaonekana!ifahamike kuwa CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini kinachokinyima usingizi Chama Cha Mapinduzi CCM.Kila kichwa cha mwana CCM Muovu kinaiwazia mabaya CHADEMA ingawaje kuna wana CCM wachache wenye uelewa lakini kutokana na fursa chache za matumizi ya akili ndani ya CCM,wanazitumia kuisaidia CHDM.
Tujiulize wana jf hivi inawezekana mwan CCM kutoa maneno ya nasaha ya kuijenga CHADEMA?Ni kwa nini wakaweza kutugawanya sisi tulio amka na kuona mbele zaidi kwa hoja za kipumbavu? Mitego yote iliyowekwa na CCM juu ya CHADEMA Inaelekea kukosa nguvu!kadiri miaka inavyo kwenda watu wanaamka na kugundua mitego yote inayotengenezwa ya kuvidhoofisha vyama vya upinzani vinavyoonekana kuwa na nguvu ya kuhatarisha uhai wa CCM!Mbinu hiz zinaelekea kukosa nguvu baada ya mamluki na kauli za kukichafua chama kugundulika mapema.
NAWAPA HONGERA KURUGENZI YA INTELIGENSIA YA CHAMA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kubaini mamluki na kila aina ya uhaini unaofanywa dhidi ya CHDM,ni wakati pia kwa kujua uzito wa kazi walio nayo na challenge zinavyoongezeka nashauri kamati hii ya inteligensia iongezewe NGUVU NA VIFAA VYA KISASA!pia niwapongeze KAMATI KUU kwa mshikamano walio nao.
Nawashauri kuwa MAKINI ZAIDI KWANI BAADA YA PLAN HIYO KUSHNDWA WANAKUJA NA PLAN B ya kukidhoofisha CHDM.Wana CHDM,WANA JF NA WANANCHI WOTE wenye mapenzi mema tujikite katika kukijenga CHADEMA Kwa kusaidia kutoa taarifa zote za uhaini za kukihujumu chama .
Kamati kuu kaeni kama kuna tofauti miongoni mwenu mkosoane mjadiliane na mzimalize kiprotocal pasipo sisi wanachama kujua matatizo ya ndani ambayo siyo muhmu kwetu!
Nimetumia dakika hizi chache kuwapongeza na kuwashauri!naomba mchukue ushari zaidi.PONGEZI NYINGI TUTAPEANA BAADA YA SAFARI NGUMU YA 2015.
Asanteni!
Umeongea mambo ya msingi sana, hivi sasa Uongozi wote wa juu wa magamba wanakosa usingizi kutokana na kasi kubwa ya moto wa M4C,kwa hiyo vikao vyao vya ndani wakati wote, wanapanga njama za kuivuruga Chadema. Lakini kwa bahati nzuri sana tofauti na siku za nyuma yaliyowakuta NCCR Mageuzi nyakati zake na CUF, Chadema wako makini sana kuwashughulikia mapandikizi na mamluki wanolipwa na magamba ili kukivuruga Chadema, ndiyo maana tabiri zao za mara Chadema kitakufa kesho,keshokutwa, mara mtondogoo,zote zinakuwa ndoto za alinacha na CDM inaendelea kuchanja mbuga kuelekea 2015,ambapo bila wasiwasi wowote itatwaa Dola kutokana na ridhaa ya wanyonge wa nchi hii watakawapigia kura za kishindo, na miongoni ya kura hizo watazipata hata kutoka kwa wana-CCM wanyonge ambaohuwa wanaambiwa CCM ina wenyewe,ambao ni mafisadi!! Cha msingi ni kuwa makini na kila mkakati unaopangwa na magamba,na kwa kuwa siku zote tunasema CDM tuna Mungu tunayemtumaini,wao CCM wana mabilioni ya pesa yaliyopatikana kwa njia za ufisadi wanayoyategemea kuwahonga mamluki ili waivuruge CDM!!
Viva CHADEMA,Viva Tanzania.Mungu atupe nguvu ya kufika salama 2015 ili tuweze
kuondoa wezi wa mali za umma.
Chadema inakufa haya mambo ya kujifariji eti imeshinda majaribu na maneno ya kiroho ili hali kansa iko palepale. Huwezi kusulihisha ugomvi kwa kuwaweka wapenzi watatu kwa mtu mmoja. Inabidi tu wengine watalakiwe abaki mmoja. Sasa hapa kuna matabaka ambayo hayayumbishwi. Hakuna demokrasia ya kweli ndani ya chadema bali uteuzi unaofanywa na mzee mtei akisaidiana na mbowe na slaa. Eti wengine kazi yao ni kuitikia tuu piiipooo pwaaaaaaa hata kama haieleweki. What abaout people energy?? Wanawatuhumu wakina halima mdee zito na juliana eti wameanzisha chama ndani ya chadema kinaitwa m17 lakini hawawatuhumu wakina lema walioanzisha m4c. Vipi ile sangara maana yake nini?? Hapa kuna kazi watatafuta mchawi mpaka watatawanyika kushoto na kulia. Chadema haiwezi kusimama bila zitto na kundi lake. Hilo litakuwa pigo la mwaka kwa sababu zitto anawakilisha sura ya kitaifa ya chadema akikubalika na chadema kanda ya ziwa, magharibi na mashariki ya tanzania. Hakuna chama kinaweza kuwa na nguvu eti kwa kutegemea kanda ya kaskasizi peke yake. Pia utoaji madaraka chadema umeweka nguvu kubwa upande mmoja wa nchu ukianzia mwenyekiti katibu wa vijana, mwenyekiti wa wanawake na wafadhili wa chama. Wabunge hao tunaacha kwa sasa
Tunasubiri kwa hamu kiongozi,safi sanakwa bomu linalokuja naona utakata tamaa kabisa,Kwa sbabu bomu hilo linaianika chadema na michezo yao yote michafu inayofanyika kwa usiri mkubwa na kuwaaminisha watanzania kwamba ni serikali kumbe ni wao.
Yaani,nakuombea uwe hai ushuhudie mwaka huu watu wanavyoumbuka.Asante mungu kwa kufanikisha hatua zote kilichobaki ni kuweka kwa tv muone