Salaam, shalom!!
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu uchaguzi unaendelea wa Kanda, mchuano ni mkali na leo tumeshuhudia Mh Sugu akiibuka mshindi Kwa tofauti ya kura mbili pekee.
Jambo jingine, sijasikia kura kuharibika, hili linaonesha kuwa uelewa wa wapiga kura CHADEMA ni WA kiwango Cha juu.
Nimefurahishwa pia na kauli ya Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu TUNDU Lisu kukemea hadharani matumizi ya pesa chafu katika mchakato mzima wa uchaguzi wa chama chake.
Jambo lingine zuri ni kuwa, sijasikia matukio ya wizi wa kura, kura kuzidi idadi ya wapiga kura, Wala sijaona polisi wakisimamia masanduku ya kura Kwa mitutu ya bunduki.
NEC ijifunze DEMOKRASIA na uhuru wa uchaguzi uliooonyeshwa na CHADEMA. Kwa waliotegemea mkono uanguke kama fisi, pole Yao.
Kwa kilichotokea katika chaguzi hizi zinazoendelea za CDM, wananchi wanatakiwa KUIAMINI pasi na shaka CDM katika chaguzi zijazo Kwa kuwa wameonyesha matumaini ya kuheshimu SANDUKU LA KURA ambalo likiheshimiwa, hutoa viongozi Bora.
Mungu ibariki CHADEMA ✊
Mungu Ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
PIA SOMA:
- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa