Pre GE2025 Hongera CHADEMA kwa uchaguzi huru na haki, sijasikia tukio la wizi wa kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa mtaendelea kujipigia kura, na kutojiibia mbwa nyie. Acha niende sesemu oyeee.
Umeambiwa CCM wanapokea waleviπŸ˜€?

Uchaguzi huu na ujao mitaa, madiwani, wabunge na Rais,

Hatutaki viongozi walevi Wala wapigakura walevi.
 
Kimara Uchaguzi imebidi urudiwe huko, kulikuwa na matatizo makubwa ya uchaguzi.

Ova
 
Umeambiwa CCM wanapokea waleviπŸ˜€?

Uchaguzi huu na ujao mitaa, madiwani, wabunge na Rais,

Hatutaki viongozi walevi Wala wapigakura walevi.
Sawa, Nimeambiwa nchi inaongozwa na sesemu, nyie mnajipa taabu tu, sasa sesemu, ndio wananilisha, wananivesha na kunipa pombe, wanasema mama anaupiga mwingi. Sasa, acha nikapokelewa nyumbani kura yangu wanaitaka. Nyie si mnaona sisi tunaohoji walevi hatufai sawa. Acha niende sesemu tu. Nyie bakini na watu wasio walevi. Haya.
 
Kwamba CCM wanakununulia pombe sio!!

johnthebaptist ya Kweli hayo?
 
Hujasikia jamani huko sugu aka moto chini katoa mpunga balaa. Yaani memba wakitoka hapo ni kununua fuso tu. Ila hiki ki NGO kinaboa
 
Hujasikia jamani huko sugu aka moto chini katoa mpunga balaa. Yaani memba wakitoka hapo ni kununua fuso tu. Ila hiki ki NGO kinaboa
Nilichosikia na kuthibitisha ni kuwa,

Sugu amemshinda Msigwa Kwa kura mbili pekee, 54 Kwa 52.

Na uchaguzi ulikuwa huru na HAKI,

Na Msigwa amekubali matokeo.

Source: Mwananchi media.

Wewe ndugu Mudawote chanzo Cha taarifa zako za kusikia ni kipi?
 
Tatizo halimalizwi kwa kulificha. Ila kwa kutatuliwa na kuzomewa hilo tatizo.

Ova
Sasa mbona wewe umeamua kulificha Badala ya kuliweka wazi?

Ungekuwa na Nia ya kuliweka wazi, ungetoa uthibitisho juu ya A- Z kuhusu tukio Hilo,

Karibu πŸ™
 
Kama kuna funzo muhimu zaidi kwa CHADEMA kutokana na zoezi lao hili, ni kutambua kwamba bado hawajafuzu kitu chochote.
Uchaguzi wao huu uchukuliwe kuwa kama 'mock' hivi kuelekea kwenye mtihani halisi hapo 2024 na 2025.
Mtihani wao huu wa 'mock' uwawezeshe kuwapata wanachama wao wenye sifa kushindana katika kila nafasi itakayokuwepo ya kuchaguliwa. Pasiwepo hata nafasi moja watakayowaachia CCM wapite bila ushindani, kuanzia kwenye nafasi za mitaa; kata; wilaya, mikoa hadi kwenye urais.

Lakini mtihani huu wa majaribio 'Mock' iwe ndipo chanzo cha kupanga mikakati ya kuzuia uharibifu unaofanywa na CCM katika chaguzi. Wajipange vizuri toka sasa, kuhakikisha kwamba hakuna kura ya mwananchi yeyote itakayoharibiwa kwa sababu CCM wanatafuta ushindi wasioustahili. Huu ndio mtihani wao mkubwa tokea sasa na kwenda mbele.
 
Sugu na Wenje wamewapiga bei kama matikiti,mara vurugu mara wagombea wajitoe yaani ni shida tupu 😁😁

Pesa haiwezi Kushindwa na omba omba πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Umenena vyema,

Kumbe CCM wamekuwa wakiingiza viongozi mapandikizi ambao huleta baadae wagombea wabovu ambao hujiondoa Ili kulipa CCM ushindi wa mezani.

Uchaguzi wa 2024&2025 utakuwa wa kipekee,

Sasa wanajiandaa kuajiri polisi wengi sana Ili wasaidie jahazi lisizame, Hilo nalo halitafanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…