Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Hivi ina maana huko PCCB hakuna aliyekuwa analijua hili? shame!!!SSH tuletee wazenj zaidi huku haya mengine ya huku bara ni majizi na manafiki tu.
Ishu sio kulifahamu, kama hadi PM, aliambiwa lakini hakufanya lolote, unategemea nini?nguvu iliyokuwa nyuma ya sabaya ilikuwa kubwa sana!!ni Mungu tu ndio angeweza kuamua vingine!!
 
Huyu mjuba ingepaswa apewe hukumu ya kifo cha kupigwa mawe tu. Kisha awekwe kwenye eneo la wazi ili kila mwenye hasira naye akamrushie jiwe. Japokuwa hii hukumu bado itakuwa ndogo sana Kwa Uharamia aliofanya..
Kama adhabu ya Sabaya aliyepora milioni 25 ni hiyo aliyepora T 1.5 yeye adhabu yake ni ipi ?
 
Bila shaka ulimaanisha uthubutu wa kitenda uovu.
Ukilisoma bandiko, utaona nimesema ni uthubutu wa nini.

P
 
Wanachelewa sana kumfunga huyu ndumku,afungwe angalau kosa moja la kifungo cha maisha ili lifidie yote
 
Ni kwanini polisi, Takukuru na a Waziri Mkuu walishindwa kumsaidia mzee Lyimo?
Akili inaniambia kuwa pengine alikuwa na ngome ngumu zaidi ya hao polisi.

Alikuwa na ngome ngumu zaidi ya waziri mkuu.

Alikuwa na gome ngumu zaidi ya takukuru.

Hawa ngome hizi zote katika wakati ule zilikuwa zinacheza kwa step kweli kweli yaani.

Swali ni je ngome ngumu hiyo ni ipi ?
 
Ukilisoma bandiko, utaona nimesema ni uthubutu wa nini.

P
Uthubutu bila maadili ni jehenamu kwa waathirika wa uthubutu wa mthubutu.
 
Maagizo yote yameyeyuka umebakia wewe vs sheria na kosa jinai.....Mungu hadhihakiwiii
 
Back
Top Bottom