Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Hivi haya mambo ni ya kweli...?

Hivi huyu jamaa kweli alifanya yote haya anayotuhumiwa..?

Kama ndivyo, basi;

1. Huyu mtu alikuwa jambazi wala siyo kiongozi..!!

2. Huyu mtu alikuwa ni SHETANI katika sura ya BINADAMU...!!

This man deserves to be punished. He deserves to pay for his actions...
Umetaja sifa zote za mwendazake hao wengine wote walikua wanajifunza kwake
 
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.

View attachment 1818470
Hii yote aliridhi kwa mwendazake
 
Akili inaniambia kuwa pengine alikuwa na ngome ngumu zaidi ya hao polisi.

Alikuwa na ngome ngumu zaidi ya waziri mkuu.

Alikuwa na gome ngumu zaidi ya takukuru.

Hawa ngome hizi zote katika wakati ule zilikuwa zinacheza kwa step kweli kweli yaani.

Swali ni je ngome ngumu hiyo ni ipi ?
Ile inayochezea vitasa jehanam
 
Nchi ilikuwa mikononi mwa viongozi wanyanganyi, tutaendelea kuona vitu vya kustajabisha yaliyotendeka ndani ya utawala wa awamu ya tano ya Mwendazake.
 
Isee....kiwango cha ubinafsi bongo ni kikubwa mno😥
Kama kweli Lema alilifikisha kwa kiranja wa mawaziri na akawa kimya.....🤔🤔🤔
Halafu huko mbeleni kuna vilaza watakuja kuibuka kuwa huyu bwana anafaa kuwa rais wa bongo!!!
 
Daah, angalau sasa nchi yangu inaelekea kwenye haki ile hali ilikuwa sio, ashukuriwe mingi, daah
 
Huyu mjuba ingepaswa apewe hukumu ya kifo cha kupigwa mawe tu. Kisha awekwe kwenye eneo la wazi ili kila mwenye hasira naye akamrushie jiwe. Japokuwa hii hukumu bado itakuwa ndogo sana Kwa Uharamia aliofanya..
Na angewekwa pale Moshi mjini akagongwa mawe, watu wangesafiri angalau kurusha hata jiwe moja.
 
Bado Kuna mtu atasema mwaka 2015 tulipata mgeni mwenye maono...shubamiti[emoji24]..
 
Hivi ina maana huko PCCB hakuna aliyekuwa analijua hili? shame!!!SSH tuletee wazenj zaidi huku haya mengine ya huku bara ni majizi na manafiki tu.
Sawa kabisa Mie SASA hivi akiteua muislamu nakuwa na furaha maana tuna uhakika WA usalama. Awajaze Tu Sisi furaha mbele.
 
Mimi naamini nilichoambiwa kuhusu marehemu, ilikuwa ni kweli. Sidhani kama marehemu, wakati wote alikuwa katika ufahamu wake. Na yeye mwenyewe aliwahi kudokeza mara mbili:

"Itategemea hiyo siku nimeamkaje"
" Nimekuteua wewe Mpina kwa sababu wewe ni kichaa mwenzangu'
Daaaaah [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom