Hongera Daniel Chongolo kwa kuwa muwazi na kuukataa mfumo dhalimu

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Viongozi wengi hung’ang’ania madaraka mpaka watolewe lakini angalau umeonesha njia nyingine kwa wenzako CCM.

Umeonesha kuwa hupendi kukokotwa kama punda kwa maslahi ya wachache.

Umeonesha hukupenda utendaji wa hovyo wa viongozi wa CCM akiwemo Makonda na Samia.

Umeonesha kuwa CCM kuna mgogoro unaendelea.

Umeonesha kuwa CCM bila kuwa mcheza rafu huwezi kuongoza chama hicho.

Pamoja na shinikizo la kuwa bado CCM tunajua umeanza kuuchoka mfumo CCM, ni mwanzo mzuri.

Hongera!
 
20231102_070714.png
 
Atakuwa ameshinikizwa si kwa utamu wa madaraka ulivyo kisa kusemwa semwa mitandaoni na watu ambao hata uhusika wao haujui. Katibu mkuu alipoa sana tena sana ni kazi bure. Kiwekwe chuma kikisimama kutema cheche wanachama wanasikia/kutekeleza na wapinzani wanahofia pia. Vita iko karibu 2024 mitaa na 2025 uchaguzi mkuu.
 
Mtu hata mwenye uadilifu mdogo sana, anayethamini uhai wa mwanadamu, na thamani ya mwanadamu, hawezi kufanya kazi na muuaji, mtekaji watu na mdhulumaji wa mali za watu.

Rais Samia kwa kumteua na kuamua kufanya kazi na muuaji anapeleka ujumbe kwa watu kuwa naye yupo tayari kufanya uchafu wa kila aina, hata kama ni kuwatumia wauaji ili kuyatafuta madaraka.

Walaaniwe wauaji na vizazi vyao. Roho za waliokatishwa uhai wao na hawa mashetani zipumzike kwa amani. Kisasi dhidi ya wauaji wao kipo mikononi mwa Mungu.
 
Ingizo la Bashite kwenye chama litasababisha mvurugano mkubwa sana ndani ya hicho chama chao wakati huu, na pia wakati ujao.

Kamwe Wahafidhina na wafuasi wa Jiwe hawawezi kuishi pamoja. Maana hawawezi kuyasahau kirahisi tu yale maumivu waliyopitia kipindi kile, na hivyo kufanya kazi na watu wake wa karibu; akiwemo huyu Bashite.
 
Ukiingiza kivuruge au ibilisi mahali popote, lazima amani ipotee.
 
Ingizo la Bashite kwenye chama litasababisha mvurugano mkubwa sana ndani ya hicho chama chao wakati huu, na pia wakati ujao.

Kamwe Wahafidhina na wafuasi wa Jiwe hawawezi kuishi pamoja. Maana hawawezi kuyasahau kirahisi tu yale maumivu waliyopitia kipindi kile, na hivyo kufanya kazi na watu wake wa karibu; akiwemo huyu Bashite.
Ukiingiza kivuruge au ibilisi mahali popote, lazima amani ipotee. Yaani umuingize muuaji awaongoze ba awasemee wasiopenda uuaji, utegemee kuwe na amani?
 
Ingizo la Bashite kwenye chama litasababisha mvurugano mkubwa sana ndani ya hicho chama chao wakati huu, na pia wakati ujao.

Kamwe Wahafidhina na wafuasi wa Jiwe hawawezi kuishi pamoja. Maana hawawezi kuyasahau kirahisi tu yale maumivu waliyopitia kipindi kile, na hivyo kufanya kazi na watu wake wa karibu; akiwemo huyu Bashite.
Kaenda kukimaliza chama cha haya majangili
 
Back
Top Bottom