Mtu hata mwenye uadilifu mdogo sana, anayethamini uhai wa mwanadamu, na thamani ya mwanadamu, hawezi kufanya kazi na muuaji, mtekaji watu na mdhulumaji wa mali za watu.
Rais Samia kwa kumteua na kuamua kufanya kazi na muuaji anapeleka ujumbe kwa watu kuwa naye yupo tayari kufanya uchafu wa kila aina, hata kama ni kuwatumia wauaji ili kuyatafuta madaraka.
Walaaniwe wauaji na vizazi vyao. Roho za waliokatishwa uhai wao na hawa mashetani zipumzike kwa amani. Kisasi dhidi ya wauaji wao kipo mikononi mwa Mungu.